RC Shinyanga na M/Kiti BAVICHA Iringa,mabishano yenu kuhusu hali ya Corona Hospitali ya Shinyanga hayana tija

RC Shinyanga na M/Kiti BAVICHA Iringa,mabishano yenu kuhusu hali ya Corona Hospitali ya Shinyanga hayana tija

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Baada ya M/Kiti wa BAVICHA Iringa ,Ndugu Vitus Nkuna kualalmika kuwa Hospitali ya Mkoa ya Shinyanga ina Scarcity ya mitungi ya gesi ya Oksijen na wagonjwa wa Corona kuwa wengi, hatimaye mkuu wa mkoa wa Shinyanga naye amekuja juu na kumtuhum kwa upotoshaje. Pia alikwenda mbali zaidi kwa kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Ndugu Vitus. Lakin baaaye tena Katibu huyu wa BAVICHA naye amerudia kauli yake ileile na kumtaja DC wa Shinyanga kuwa anajua kila kitu kuhusu tatizo hilo . Namnukuu hapa chini:

"Narudia tena Hospital ya Mkoa wa Shinyanga Kuna wagonjwa wa #Coronavirus .kuna utata wa Mitungi ya Gesi, Wizara_afyatz na MSD fuatilieni, DC wa Shinyanga Mjini analiewa vizuri. Tunatoa taarifa hizi Kuokoa Maisha ya Ndugu zetu,nimemsikiliza RC wa Shinyanga yy anaokoa ajira yake."- Vitus Nkuna

Ningependa nitoe Rai kwa RC wa SHY kuwasiliana na Ndugu Vitalis apate hizo taarifa kamili , na yeye kwa mamlaka yake afuatilie na kuzifanyia kazi au kuja na feedback ama kukanusha, na si kuhasamiana au kutishiana kuwa watachukuliana hatua. Vivo hivyo namshauri Bwana Vitus ajaribu kuwasilisha kwa mkuu huyo wa mkoa findings zake. Yawezekana kama kawaia yetu kuwa RC anapotoshwa na wasaidizi wake wakati hali ni mbaya.

Tatizo ni letu sote, na tunapaswa kushirikiana kwa kupeana taarifa na kusaidiana kutafuta ufumbuzi na si kulumbana.

Pia soma > RC Sengati: Kiongozi wa CHADEMA aliyesema Shinyanga imeelemewa na wagonjwa wa corona achukuliwe hatua kali za kisheria

E6G3FLYXIAEd0-s.jpg
E6GpVK9XEAYhWE9.png
 
Viongozi wengi wanapenda kupata taarifa sirini ili wajipange kwa mabosi wao. Hilo ni tatizo
 
Mbona ni siri iliyobayana! Ka una 60,000 ndg yko anapewa mtungi wanakwambia mitungi imekata serikali ifatilie itajua ukweli
 
Cha maana wanajibishana wao! Sie haituhusu! Kwani si juzi walisema Hakuna Corona nchi nzima, and now they revert back kwenye matapishi yao!
 
Kwani source ya Oxygen ni mitungi tu?
Ngwini wanabishana wakati wataalamu wametulia
 
Swali bwana Shujaa Mwendazake , Corona ipo au haipo hapo Shinyanga?
Corona ni kama kipindupindu. Hata kama mtu mmoja anayo ni tatizo maana inasambaa haraka sana na kuua.
 
Mitungi tu ya Oksjeni? Hakuna kingine?
Sitaki niamini hivyo.
Hii mitungi ya Okisjeni ndio munaiita Ventilator au ?
 
Huyo mwenyekiti aache upuuzi,taarifa rasmi ni ya serikali,full stop
 
Back
Top Bottom