RC Songwe atembeza kichapo kwa wanafunzi waliochoma shule ya sekondari ya Wavulana ya Oswe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
bakora.JPG

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela mapema leo amewachapa viboko wanafunzi watano waliohusika katika tukio la kuchoma moto shule ya sekondari ya Wavulana ya Oswe na kusababisha hasara ya Zaidi ya shilingi milioni 26.

Brig.Jen. Mwangela amefikia hatua hiyo mara baada ya kamati aliyoiunda ya kuchunguza chanzo cha ajali ya moto uliotokea shuleni hapo Julai 3 mwaka huu kubaini kuwa wanafunzi wawili Naftari Nganga na Collin Kisinga ndio waliochoma mabweni ya shule hiyo huku wenzao watatu wakiwa na taarifa za mipango hiyo na hawakuripoti.

Amesema wanafunzi hao walianza mpango wa kuchoma moto mabweni mnamo Juni 28 kwa kununua vifaa vya kuchomea, ilipofika Julai 2 walijaribu kuchoma bweni lakini halikuwaka, Julai 3 walichoma bweni likawaka na kusababisha hasara hiyo na Julai 6 walifanya jaribio lingine tena la kuchoma moto ghala la chakula lakini halikuwaka moto.

Brig. Jen. Mwangela ametoa miezi mitatu kwa wazazi wa Naftari na Collin kila mmoja alipe shilingi milioni 7,300,000/= Mmiliki wa Shule pia alibainika kuwa na uzembe wa kuweka vifaa vya kuzimia moto hiyo alipie shilingi milioni 7,300,000/= huku mwalimu wa zamu siku ya tukio, mlinzi na Patroni nao wakitakiwa kulipa shilingi milioni 4 ili kufidia hasara iliyotokana na ajali hiyo ya moto.

Chanzo: ITV
 
Inawezekana taarifa ya kamati ndiyo ilishauri kuwa mwl wa zamu na patron nao wapewe adhabu. Sidahini km RC amekurupuka tu
 
Zitumike busara zaidi ya ubabe.
 
Kwa hiyo huyo RC ndiyo mahakama ashaamua kua walichoma moto na ametoa hukumu ya viboko na kuwaambia wazazi walipe?
Huu u******** hivi Tanzania imejaa ma zero brain tu? Huyu RC ana elimu? Kufany mambo kumfurahisha jiwe kumewachizisha sana hawa jamaa, utadhani m***** kaona shilingi mia wtf.

Kama watoto wamechoma moto bweni peleka mahakama iamue wakikutwa na hatia mahakama itadeal na hao wahalifu, huwezi chapa viboko ukasema wazazi walipe, its so stupid. Next time watachoma moto huku kuna mtu ndani wauw kabisa

Hawa ndio watu jiwe kapanga hadi namuona na yeye chizi kati yao, Tanzania nchi ya kijinga sana vilaza wengi hadi aibu
 
Huko Tanganyika kila kitu ni makamera tu!

Hata mtu ukienda kunya unaweza kushangaa umepigwa makamera yakatupwa mtandaoni.

Viboko ni adhabu ya KUTWEZA UTU na kudhalilisha haifai kabisa. Lakini bado na makamera nayo humo humo!

Tukisema tunaambiwa ooooohhh "unajifanya mtetezi wa haki za binadamu".

Mradi tu dunia inazidi kuzunguka kwenye muhimili wake, wacha siku zisonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom