Reading in between the lines & listening in between the words. Ikitokea kuna kitu amekinoti lakini hakukisema, ukikijua kuna ubaya tumseme?

Reading in between the lines & listening in between the words. Ikitokea kuna kitu amekinoti lakini hakukisema, ukikijua kuna ubaya tumseme?

Wanabodi,

Hili ni Bandiko la swali, kuhusu moja ya zile mada ngumu za psychoanalysis, ambayo hoja zake ni vitu vya kufikirika tu na havijatamkwa rasmi, lakini vitu hivyo, vikisemwa na kujadiliwa kwa uwazi, vitalisaidia taifa.

Watu tumeubwa tofauti tofauti, wengine ni good observers na wengine ni just too notty, mimi ni mmoja wa watu hawa, through observations nilikuja kunote kuwa kuna vitu viongozi wetu hawapendi kusikia au kuambiwa, hivyo walio wazunguka, watawaambia yale tuu mabosi wao wanapenda kusikia, hivyo ukiwa mkweli too much wa type yangu, unakuwa hupendwi!. Miongoni mwa vitu nilivyo muomba sana Mungu ni "anifundishe kunyamaza".

Kwenye hotuba za viongozi, sometimes kuna vitu vingi ambavyo kiongozi havipendi lakini havisemi, kwasababu tangu kabla hajaingia kwenye uongozi, alivikuta ndio vinafanyika hivyo.

Sisi wasomaji wa in between the lines na wasikilizaji wa the inner voice, kama umemsikia Mama, akizungumzia jambo fulani, na wewe through analytical and logical progression thinking ukabaini kuwa kuna jambo halipendi lakini hawezi kulisemea kwasababu siku zote jambo hilo, hivyo ndivyo linavyofanyika, ikitokea, ukalijua, kuna ubaya kulisema au kumsemea mama ili jambo hilo libadilishwe?, au ukimsemea Mama jambo ambalo hajalisema huku kutakuwa ni kumlisha Mama maneno?.

Kwa vile hii ni hoja ya psychoanalysis, wengi wetu wamemjua Samia baada ya kuwa rais wetu, lakini akina sisi tuliomfahamu Samia kabla hajawa rais tunazidi kumfahamu zaidi na zaidi as days go by, hivyo nakushauri anza kwa kumfahamu Samia kupitia mabandiko haya mawili haya Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...


Hii humbleness ya huyu Mama, na being down to earth, nimeiona tena jana, kwenye kuhitimisha Nane Nane Mbeya.

Baada ya kukamilisha kuhutubia, wakati anaondoka, badala ya kuelekea direct kwenye gari, akatuzungukia wananchi huku tukipo, mimi nikamwamkia kwa sauti, akageuka, akanitazama, akaijibu shikamoo yangu, tena I think, naomba nisimalizie maana.

Na wakati anahitimisha hotuba yake kuhitimisha Maonyesho ya Nane Nane Viwanja vya John Mwakangale, Mbeya kuna kitu sio cha kawaida, Rais Samia amekifanya, hakijawahi kufanywa na rais wetu mwingine yoyote, ukimuondoa Nyerere.

Siku zote kwenye matukio rasmi, viongozi wanatayarishiwa hotuba kwa kuandikiwa na Viongozi huhutubia ama kwa kusoma hotuba alioandikiwa, ama kwa kutumia talking points.

Lakini licha ya rais kuandikiwa hotuba, kuna baadhi ya vitu huwa anavisema kwenye hotuba ni vyake mwenyewe kutoka moyoni na sio kuandikiwa,

Wengi wa wenye uwezo wa to read in between the lines, pia wana uwezo to listen in between the world's hivyo Mama anapohutubia, ma psychoanalysits wenye uwezo wa kubaini hili ni ameandikiwa na hili ni lake kutoka moyoni.

Kwenye hotuba ya jana kule mwisho, aliwashukuru madereva.

Ukimuondoa Nyerere na hotuba zake za kulihutubia taifa kwa njia ya redio, hii ndio mara yangu ya kwanza kumsikia rais wetu yoyote akiwashukuru publically madereva!

Wasio na jicho la roho, jicho la ndani, wanaweza kuona this is a small thing!. It's not!.

Hii shukrani kwa madereva kila mtu huwa anaitoa kwa dereva wake akifika salama, lakini ile shukrani kuwashukuru madereva publically for the first time, japo inaonekana ni shukrani tuu, kwa sisi ma psychoanalysits, sio shukrani tuu, ile ni shukrani ya appreciation ya being arrived safely out of.

Kwenye shukrani hizi, kuna kitu hapa Rais Samia amekisema bila kukitamka, uwezo wa kumwelewa rais wetu bila hata kutamka kitu ni plus kwenye utawala wa nchi.

Katika shukrani hizi za rais, Rais Samia kawasifu na kuwapongeza madereva wa msafara kwa umahiri wao na car control.

Sijui ni wangapi kati yetu wana uwezo wa kusoma body language na facial expressions wakati mtu akiongea!, Rais Samia wakati amewashukuru madereva kwa kuwafikisha salama, kauli na mdomo ni kuwashukuru madereva, lakini ishara ya mikono ni kumshukuru Mungu kufika salama!.

Kitu ambacho Mama Samia hakukisema ni the speed of msafara was very high, mnamuweka Mama Roho Juu!.

Kwa vile tumetawaliwa na wazungu, watu wetu wa usalama wanafunzwa msafara kwenda kwa kasi ya ajabu hivyo hivyo na wao kuiapply hivyo hivyo hata kama in reality Tanzania haina security threat kwa rais wetu kivile!.

Kwenye msafara wa rais kuna rake 3, kabla ya msafara, hivyo madereva wanakimbiza msafara kwa speed ya ajabu for what?

Halafu unaambiwa eti wanakijiji au wananchi wa eneo fulani wamezuia msafara!.

All and all, asante sana Mama kuonyesha concern for this.

Hata hii democrasia tunayoitumia ni imposed democracy, kama sasa tunaotumia the African Democracy ambapo nchi ya vyama vingi vya siasa, vinaweza kufanya uchaguzi Mkuu na chama kimoja kikashinda Kwa 99% na uchaguzi huo ukawa huru wa haki na wa kidemocrasia, tuachane na imposed security protocols, to embrace African security protocols, viongozi wetu wakimaliza kuhutubia wanasalimia na kujichanganya kidogo na watu tuna amkuana, kisha ndio anaondoka!.
NB- alipopita karibu na mimi, nilimuamkia kwa sauti, aligeuka akanitazama na alijibu! shikamoo yangu!.

Paskali.
Nimekuelewa... Unakerwa na uongo wa wanavijiji kuzuia misafara. Unakerwa na misururu ya magari ya kifahari yaendayo kasi kwenye msafara wa SSH!
Mwisho unakerwa na msururu wa vikosi vya kumlinda SSH!
Kama psychoanalyst, naungana na wewe!
Najua yote ni michongo ya wajanja wachache ili wajustify kula hela za Ikulu!!
 
Ulinzi wa viongozi ni taaluma ya watu, hata kiongozi mwenyewe anaweza asielewe vizuri sababu za mambo fulani fulani lakini ni vema akaheshimu na kuwaamini wazalendo walioapa kumlinda kwa gharana yoyote, hata ikibidi kupoteza uhai wao.

Tuwaache wafanye kazi yao.
Mkuu Mzalendo Uchwara , naunga mkono hoja, hizo ni fani sa watu ila sometimes wana over do things!. Mwenzetu umeisha wahi ona speed ya msafara kwenye barabara ya vumbi?.
P
 
halafu kuna kitu nimenote toka akiwa VP , umekua na heshima kubwa kwake sijui kwa nini
Sababu mbona niliisha ziweka humu.. Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? halafu ukakuta mtu mwenyewe ni hivi Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” utaanzia wapi?.
maana hata maandiko yako hujawahi kumponda Rais Samia sijui kuna nini
Mkuu chotera , huyu ni Mama, heshima mbele, ila ukiona hivyo ujue Mama yuko perfect, ila siku akiboronga ni spana tuu kama kawa Ila ni spana za kuheshimu heshima kama hivi Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

P
 
"pascal mayala"

Kwamba kulikuwa na HATARI fulani lakini ameokoka kwenye HATARI Hiyo Sio!!?

Yeye afuate MAAGIZO ya wale waliomweka!!

"The state wamesema apewe Muda"!

Hilo tu!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Nimekuelewa... Unakerwa na uongo wa wanavijiji kuzuia misafara. Unakerwa na misururu ya magari ya kifahari yaendayo kasi kwenye msafara wa SSH!
Mwisho unakerwa na msururu wa vikosi vya kumlinda SSH!
Kama psychoanalyst, naungana na wewe!
Najua yote ni michongo ya wajanja wachache ili wajustify kula hela za Ikulu!!
Mkuu Jp Omuga kiukweli nafarijika sana kila nikutapo wana jf wenye uwezo to read in between the lines
P
 
Back
Top Bottom