Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Kwa sehemu ile na aina ya nyumba bei siyo kubwa. Sema wabongo wengi tumezoea ''nyumba'' za milioni ishirini. Nikuhakikishie kuwa nyumba nyingi tunazoishi hazina hadhi ya kuitwa nyumba. Nyingi ni muunganisho wa matofali na sementi na bati juu. Hakuna utaalam wowote kwenye kujenga.
Kwaiyo mkuu wewe unamiliki nyumba ya million mia ngapi?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama kipindi hicho fremu, hasa katikati ya jiji na maeneo yaliyochangamka, zina very high demand kwa nini watu wasiongeze supply kwa kujenga mafremu mengi? Biashara ilikuwa kubwa na wanunuzi wengi mpaka kutoka nchi jirani. Cha kujiuliza ni why biashara zinakufa...
Mbona sababu ziko wazi? Watu wanauliza as if hawajui mambo yanavyokwenda (Kodi nyingi while purchasing power ya wananchi ni ndogo). Wanauchumi waliokuwa na guts especially wa ulinzani walishauri na kushauri lakini hakuna hatua zilizokuwa zikichukuliwa. Serikali inayojiona imejikamilisha kilakitu ndio serikali idondokayo.
 
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.

Kwa wakazi wa Dsr es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.

Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.

Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.

Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.

Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.

Je hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?
Kwa hiyo maoni yako ni yapi? au nio umbea tu unakusumbua?
 
Mkuu hii biashara imeanguka ghafla bin vuu, kuna watu walitia pesa nyingi wakidhani mambo yatakuwa kama yalivyokuwa , walipomaliza majengo ndo wanakutana na huu mdororo, naukute ilikuwa ni pesa ya benki ndo balaa
Hiyo ndio Watoto wa Mjini wanaiita Mbuzi kameza condom
 
Ngoja mirad mikubwa ya kukamuana ya kukamuana kodi za kila aina iishe, ndipo hapo mkanda unawezwa kulegezwa kidogo..labda 2030 hivi.
 
Kariakoo ya sasa mbona wenye frem watakugombea kama mpira wa kona? Ile jeuri yote imeisha. Kwanza zilijengwa nyingi kupita mahitaji. Zimebaki sehemu chache zenye movement nzuri ya wateja ndiyo labda kidogo frem inaweza kuwa shida.

Kuna sehemu kama pale Mwenge stendi miaka ya 2010 mpaka 2015 mtu ulikuwa hugusi frem na wenye nyumba walikuwa na jeuri ya ajabu. Mwenye nyumba akikohoa kidogo kama umepangisha kwake unakimbilia kumuuliza kama unaweza kumpa msaada. Kwanza kupata frem ilikuwa ni kama kushinda bahati nasibu ya mamilioni. Nenda siku hizi uone... frem hazina watu
Toka jiwe ashike madaraka hakuna sekta yoyote yenye unafuu, Japo Mataga hawawezi liona hili.
 
Ucumi imara unapimwa na vitu viwili muhimu.
1.Financial system
2.Stock Market
Hiyo number 1 ndio mjumuisho hadi wa real estate financing,kw anchi hiii financial system iko hoi kweli kweli,ikimaanisha uchumi uko hoi pia..
Umeongea sahihi mkuu labda nami niongezee nyama katika hili. Kosa kubwa serikali ililofanya ni kuua Financial markets. Ni Kama vile tumejisahaulisha umuhimu wa financial market katika kukuza uchumi wa nchi. Hii imesababisha investments even foreign direct investment FDI kuwa garama na ngumu (Unfavourable environment for investment).
Hakuna maendeleo pasipo uwekezaji wenye tija. Nchi zilizoendelea vizuri (Well - Developed countries ambazo ni marafiki Kama France ( Tumeona mwezi uliopita Waziri Kabudi alikuwa kule kwaajili ya kustrengthen mahusiano Kati ya nchi hizi mbili) zinapaswa ziifund serikali yetu kunyanyua uwekezaji.
Serikali inapaswa kuhakikisha masoko ya kifedha yanakuwa imara (Decentrolise
Financial market). Hii hupelekea taasisi za kifedha kujiitosheleza na kuwa na mizizi mizuri ya kifedha zikisimama na kurahisisha transactions kati ya economic agents( wazalishaji na watumiaji) na vyanzo vya kifedha.
Hii hurahisisha mzunguko wa pesa kukua na uwekezaji ulio na tija kuongezeka kwasababu wafanyabiashara wanakuwa na uwezo wa kutanua biashara zao na biashara mpya kuanzishwa. Sasa hizi sera tunazozifuata sasa hivi napata mashaka sana.
 
Yatakuwa na faida baadae kwani life time yake ni miaka mingapi? Watz wanaendelea kuongezeka na tunaendelea kufyatua wengine.
Kwahiyo mnataka kuwazulumu wenye nyumba hizo halafu bado munataka mwekezaji mwingine aje ajenge?
 
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.

Kwa wakazi wa Dsr es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.

Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.

Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.

Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.

Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.

Je hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?
Hii ni ishara kuwa mafisadi wana hali ngumu sana...
 
Back
Top Bottom