Salamander
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 28,536
- 15,746
- Thread starter
- #3,901
Huyu jamaa bana kaishiwa kabisa. Alibahatika kuwa na ile golden generation ya barca + El Guaje + Torres + Madrid, aka-copy na ku-paste alichokuwa anafanya Pep, akaishika dunia, akalemaa.
Ungeona game waliocheza jana, manaake ile formation kama nilikuwa naiangalia Real Madrid ile inayoumiza kichwa, wanacheza mpira saa zote wanaingia mpaka ndani ya 18 bado wanapeana pasi hazina hata akili. Sasa hivi Del Bosque anamtegemea Morata, ndio silaha yake, dogo anacheza vizuri lakini kumpa majukumu ya taifa bado sana. Waholanzi wanadefend timu nzima, hawaachii gape na hawajafanya hata mistake moja. Wa-espñol enzi yao imekwisha.