Kwa miaka ya hivi karibuni ndani ya Santiago Bernabeu alikuja Mourinho na akaamsha ushindani mkubwa sana dhidi ya Barca. Watu wakawa wanamwangalia Mourinho atatua mbinu gani dhidi ya Barca na timu kwa ujumla.
Wengi walitaraji timu itacheza kwa kuzuia zaidi bila kufunguka sana, yaani timu inafunguka kwa kushtukiza. Na ni kweli ikawa hivyo lakini mbinu hii haikumsaidia sana Jose. Mwisho wa siku akaondoka na kutaja sababu za kijinga, mara ooh waspain hawampendi, mara ooooh mashabiki wanampangia kikosi n.k
Akaja Ancelot, ujio wake mimi ulinishtua sana na nilitegemea Barca wasingempa kazi Tata Martino na kumpa huyu Ancelot. Na ni kweli kuna uvumi ulivuma ila Barca hatukufanikiwa, jamaa akaenda Madrid.
Jamaa alikuja kufumua kile ambacho Mourinho alipanda, akina Alonso, Khedira, Alberoa wakawa wanasubiri namba na kama aliwapa basi aliwapa ilimradi tuu na afadhali Alonso yeye alicheza sana kuliko hao wengine ambao waliaminika sana na Jose. Jamaa hakutaka kabisa timu ikabe kwa muda mwingi, hakuona sababu ya kuwapanga Alonso na Khedira na kucheza formation ya 4-5-1. Tangu Ancelot achukue timu sijawahi kumuona akipanga hii formation endapo timu ikawa haina majeruhi, na kama alipanga basi nimesahau. Kiukweli Madrid ilibadilika sanaaaa, yaani jamaa walikuwa wanaposses mpira na wana kasi kubwa mno ajabu. Nionavyo mimi niliona Jamaa amejaribu sana kuipangua Madrid na kucheza soka la kuvutia mbali na Madrid ya Mourinho.
Leo hii 85% Ancelot anakwenda, na mpaka sasa ni Benitez ndo anatajwa sana kuwa mrithi wake, Je, Benitez ataendeleza Falsafa ya Soka safi kama lile la Ancelot, sitaki kuja kuona Madrid inacheza kama timu ya EPL, siipendi Madrid pale ambapo inakaribia kugusa maslahi ya Barca ila kisoka kiujumla naikubali sababu tunatoka Spain lig bora kabisa duniani.
Benitez kama unakuja tambua unakuja kukutana na Barca, Sevilla, Valencia na Atletico. Karibu!!!