Hili suala lipo tokea tuanza msimu na sioni Ancelloti alibadilisha hii hali., kwasababu ni muoga wa mabadiliko, team ina shida ya kutengeneza nafasi kwa washambuliaji, viungo wanaocheza huo uwezo hawana., kwasababu Valverde hana hizo skills, Bellingham nae ni mfungaji mzuri ila hana mipango., Modric anaweza ila umri umemtupa mkono, ila ana option ya kumchezesha Arda Güler, huo uwezo anao ila sasa Mzee Ancelloti anaogopa kujaribu kitu kipya.,
Anaweza kuanza na Camavinga, ubavu mmoja akampa Modric/Valverde/Ceballos na Mwingine Bellingham., juu ya hao akampa Arda kazi moja tu ya kutengeneza mipango kisha kule mbele aamue kuanza na Vinicius na Mbappe ama Rodrygo, wawili hapo.
Kwenye beki hatuna option zaidi ya wale wawili, ama ampe nafasi Tchouamen acheze na Rudiger., kwasababu Militão bado akili haijakaa sawa.,
Mkuu tatizo la Arda hawezi kufanya defensive duties, sasa kwenye timu kuna Mbappe na Vini ambao wote ni wavivu unafiki ni salama hapo kuengeza na mtu wa tatu? kocha yupo sahihi kwenye hilo.