Tchou ni mzuiaji mzuri ila sio passer mzuri, kwahyo kucheza kama beki wa kati anaweza tena akicheza kama beki 4 ila hafai kucheza kama beki wa mwisho.
Diaz ni kipaji kikubwa.
Endrick ni mzuri ila binafsi naona anakurupuka sana kama ulivyosema hakai kwenye nafasi na kwenye maamuzi yake anakurupuka sana.
Vini kadekezwa sana na carlo jana kamuonesha utoto kaka mkubwa Modric.
Mkuu Tchou kwa position yake hakuna ulazima wakuwa passer mzuri, kazi yake ni kukaba maeneo, kunyang'yanya na kuachia mpira kwa ma CM na AM wafanye vitu, na anaifanya kwa kiwango kizuri kabisa. Tatizo linakuja timu kukosa ma CM na AM wazuri wanaposhindwa kufanya kazi zao washabiki uchwara wenye ueleo mdogo ndio huanza kumshutumu yeye kwa kitu ambacho yeye halazimiki kuwa nacho. last two seasons alipokuwa akicheza na Kroos na Modric pamoja hatukuwahi kusikia malalamiko ya aina yoyote.