Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

nilitaka kuuliza asilimia 18 zimeenda wapi? Halafu Redet walituambia wamempa kura 71 JK na Synovate wakasema wametoa 61%. Sikucomment katika Redet kwakuwa watu walishasema vya kutosha kuhusiana sample selection ya hiyo kwanza nani amefanyiwa hiyo interview na watupe hapo 2000 walikuwa wanachama wangapi wa CCM, CUF na Chadema na NCCR Mageuzi etc. Pia kwanini wachukue march badala ya kuanzia ilipoanza kampeni mwezi August hadi Leo? Ukiangalia hiyo period waliochagua walikusudia kutengeneza matokeo fulani wakijua fika mgombea fulani ndie atakayepewa nafasi kubwa ya kushinda (No doubt alikuwa Kikwete kwani ndie aliyeeonekana anategemewa kugombea tena urais , akina slaa na wengine wamejitokeza kwenye mwezi saba na wasita kuwa wanagombea). Hivyo REDET waendelea na politics zao ila wakae wakijua ukimdanganya mtanzania mara ya kwanza atakubali ila akishagundua hata ukitoa utafiti wenye uhakika aina gani hakuna mtu anayeweza kuuamini tena.

Synovate nao wamekuja na kali, wanasema kuwa wamepata matokeo yenye kuonyesha Kikwete amepata 61% Dr Slaa amepata asilimia 16 na Lipumba asilimia 5 sasa naomba niwaulize wanaweza kutupatia sample selection yao? Period gani wametumia? Wakishatupatia hivyo nawaomba wasirudie usanii wa Redet watupe mchanganuo walichagua vipi hao watu wa kuwainterview? na kama kweli walichagua watu basi watu waende huko walikochukua hizo data watu warudie hayo matokeo tuone kama tutapata matokeo yale yale.

Nilikuwapo!!!!
 
CD4 za ccm zimeshuka sana kiasi kwamba ARV aina ya REDETE na SYNOVATE zimeanza kutumika kwa huyu mgonjwa, lakini virusi aina ya Slaa bado vinaushughulikia mwili wa huyu mgonjwa mpaka octoba 31 ambapo huyu mgonjwa anayejiita KIKWETE atakuwa mfu. Ndugu jamaa na marafiki wajiandae na maombolezo baada ya oktoba 31.
 
CD4 za CCm zimeshuka sana kiasi kwamba ARV aina ya REDET na SYNOVATE zimeanza kutumika kwa huyu mgonjwa , lakini virusi aina ya Slaa bado vinaushughulikia mwili wa huyu mgonjwa mpaka octoba 31 ambapo huyu mgonjwa anayejiita KIKWETE atakuwa mfu. Ndugu jamaa na marafiki wajiandae na maombolezo baada ya oktoba 31.
 
hahaha.. baada ya october 31st mtakuja kukataa hivihivi...
 
Si walisema hawafanyi utafiti wowote wa namna hiyo? au maji yamewafika shingoni inabidi wafanye hivyo ili kuwabeba wazee wa sisi m.
 
Syno = sina
vate = vyeti

they say nothing and nobody is listening anyway!
 
Kama utabili wa hawa researcher njaa ni sahihi basi Jakaya atulie nyumbani Msoga, asijihangaishe kuendelea kuomba kura kwani kisha shinda urais!! Akiendelea tu hiyo ni ishara tosha kuwa hizi tafiti zimechakachuliwa na hata naye haziamini!! Angekuwa kweli anaongoza huu mshawasha wa kuwatumia messages watu za kumponda mgombea wa chadema usingekuwepo kwani wangekuwa na uhakika wa ushindi.
 
Kama utabili wa hawa researcher njaa ni sahihi basi Jakaya atulie nyumbani Msoga, asijihangaishe kuendelea kuomba kura kwani kisha shinda urais!! Akiendelea tu hiyo ni ishara tosha kuwa hizi tafiti zimechakachuliwa na hata naye haziamini!! Angekuwa kweli anaongoza huu mshawasha wa kuwatumia messages watu za kumponda mgombea wa chadema usingekuwepo kwani wangekuwa na uhakika wa ushindi.

Atatulia nyumbani wakati anataka kupata zaidi ya asilimia 80 aliyopata 2005?

Opinion poll iliyo sahihi ni ile ya 31/10/2010. Hizi zingine zinasaidia tu kuonyesha wapi wahusika waongeze nguvu.
 
Sasa ni ipi kati ya Redet na Synovate ya kuaminika? It's all nonsense kwani hatujui kama kweli watu wanaulizwa au wanajipangia tu results wakiwa mezani. Za kuaminika bila shaka ni zile za mitandao -- kwani ni watu halisi wanapiga kura -- ingawa nayo pia ina mapungufu yake. Kwa hivyo ningeshauri watu wazi-shit hizi opinion polls.

Je Kinana atakuwa mbogo kesho kwa kupunguziwa tena 10%?
 
Nawahurumia hawa Synovate watakuja kuaibika zaidi. Kuna ripoti kwamba wamewahi kufanya kazi (assignment) fulani -- ya kifisadi -- na kitengo cha Ikulu cha Salva. Hilo bomu linakuja maana walikuwa wanasubiriwa watoe hii. I pity them!!!
 
Sasa ni ipi kati ya Redet na Synovate ya kuaminika? It's all nonsense kwani hatujui kama kweli watu wanaulizwa au wanajipangia tu results wakiwa mezani. Za kuaminika bila shaka ni zile za mitandao -- kwani ni watu halisi wanapiga kura -- ingawa nayo pia ina mapungufu yake. Kwa hivyo ningeshauri watu wazi-shit hizi opinion polls.

Je Kinana atakuwa mbogo kesho kwa kupunguziwa tena 10%
?


Kwenye red: Nakubaliana kwamba hizi ni lazima kuzi-shit. In one week, CCM wamapungukiwa na 10%! Hii ina maana at that rate, katika wiki tatu zilizobaki, watapoteza tena 30% kufanya jumla ya 40% kutoka 71% za REDET. Peleka hizi 40% kwa Slaa -- hivyo kwake zitakuwa 52% (12+40).

These are just bloody f****** opinion polls!!
 
Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze 1992 sijaona mwamuko wa kisiasa kama ninaoshuhudia leo, hii ni ishara ya mabadiliko makubwa kutokea siku ya kupiga kura ambapo wananchi wote watashirikishwa kufanya utafiti tofauti na utafiti wa REDET na Synovate unaowahusisha watu 2000 tu. People will prove REDET and Synovate wrong na aibu itaenda kwa mashirika hayo. Nina kila sababu:

Kukubalika kwa vyama vya upinzani hasa vijijini tofauti na miaka ya nyuma ambapo vilikuwa vinajulikana mijini tu, wananchi kuanza kuwakataa waziwazi wabunge wasiowataka ni ishara kubwa kuwa elimu ya uraia imefika kwao.

Vyama vya upinzani vilianza maandalizi ya uchaguzi mapema refer Operation Sangara ya Chadema na Operation Zinduka ya CUF. Kwa mara ya kwanza upinzani umeweka wagombea ubunge karibu majimbo yote hivyo kuonyesha ukaribu wake kwa wananchi.

Kuweka wagombea wanaouzika hasa ujio wa Dr. Slaa ulivyowashangaza wengi hata CCM hawakutarajia kwa hiyo hawakujiandaa kupata upinzani mkubwa. Imesababisha
- CCM kuanza kutumia mbinu chafu badala ya kutangaza sera mfano kuzungumzia maisha ya ndani ya Slaa.
- CCM kulitumia jeshi la wananchi badala ya Polisi ni dhahiri wameona nguvu ya upinzani ni kubwa.

Kwa mara ya kwanza viongozi ndani ya chama tawala kupinga wazi tena mbele ya vyombo vya habari utawala na uongozi wa Kikwete eg
- Tamko la MNF-kushindwa kuchukua maamuzi magumu
- Kutengwa kwa Kikwete na wanamtandao waliomuingiza ikulu
- waasisi wa chama hicho kujitenga na kampeni na kuiachia familia ya Kikwete.

Udhaifu wa kiutendaji wa Kikwete kwa miaka mitano na udhaifu wa kiafya(inajieleza).

CCM is not united again
- makundi yanayoendelea chini kwa chini na mengine waziwazi.
- maandalizi hafifu ya kura ya maoni ya CCM imebomoa badala ya kujenga chama
- wanahujumiana wenyewe kwa wenyewe

Kuvuja mapema kwa siri za wizi wa kura, mbinu gani kina nani wako wapi tofauti na miaka iliyopita, baadhi ya TISS kuhusishwa.

Jamii na wanaharakati wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuhamasisha waumini wao kujitokeza kupiga kura na baadhi ya ibada kubadilishwa.
- mfano makanisa ya Kakobe kusali Jumamosi badala ya Jumapili
- baadhi ya makanisa kufupisha ibada
- baadhi ya wanaharakati kutumika kujibu matamko refer Ananilea Nkya kumjibu Nsimbo.

Kama ilivyozoeleka wapinzani kuanzisha fujo safari hii CCM ndiyo imekuwa kinara wa kuanzisha vurugu(matukio ya hivi karibuni).

Kikwete kuzikataa hadharani kura za wafanyakazi na ujio wa kizazi kipya ambacho hakikupiga kura mwaka 1995 ni ishara kitafanya mabadiliko yatokee.

Pamoja na mambo mengine, haya ni baadhi ya mambo kwa mawazo yangu na uzoefu wangu kwenye mambo ya siasa huenda mwaka huu kukatokea mabadiliko makubwa Tanzania.

Angalizo: Mabadiliko hayo yanaweza kutokea kwa njia ya sanduku la kura endapo NEC watataka iwe hivyo au madadiliko hasi kwa njia mbadala.

Naomba kutoa hoja.
 
Wataleta tafiti nyiiingi la msingi trh 31 watazimia.mlaniwe enyi wanafiki wa REDET NA SINAVYETI..aka synovate.mtakimbia trh 31.kwa sasa chakachueni tu.hamna hata haya.Sisi tutakutana na nyie trh 31

angalizo: HATA mngetoa al 100 kwa mkwere.hakika nawambia hakuna jinsi mtaweza kuzuia nguvu ya mabadiliko,yamekuja na yamewafika shingoni mtajijua..slaa ni Rais as frm nov 1
 
CD4 za ccm zimeshuka sana kiasi kwamba ARV aina ya REDETE na SYNOVATE zimeanza kutumika kwa huyu mgonjwa, lakini virusi aina ya Slaa bado vinaushughulikia mwili wa huyu mgonjwa mpaka octoba 31 ambapo huyu mgonjwa anayejiita KIKWETE atakuwa mfu. Ndugu jamaa na marafiki wajiandae na maombolezo baada ya oktoba 31.

Hivi ni sawa kutumia masuala haya kwenye siasa...huu sio unyanyapaa nao????
 
u know what.....
REDET waliona hali mbaya wakachelewa kutoa matokeo. SYNOVATE, walishafanya utafiti wao muda mwingi wote DR slaa akawa anaongoza kwa mbali tu, wala si 45% wailvyosema'
the funny thing time was running out na hakuna cha kufanya, SYNOVATE wakategea REDET watoe halafu wafuatilie kwa nyuma, of which YOTE NI UONGO, MAAJABU NDIO HIYO 31 OCT, wananchi wa sasa they know kila kitu, so SYNOVATE, REDET are CROOKS, wamechakachua ile mbaya, ile mwisho 31 oct, DR GOOOOOOO
 
Nyie mnaangalia statistics au mnachangia tu? NAFIKIRI HAKUNA MTU MAKINI...Au undecided ni 18%? Kwa leo sina neno
 
Back
Top Bottom