Chama changu kinasikitisha, kila kitu kikiwa tofauti na wengi watakavyo basi kita nangwa. Kwa muono sahihi ni CHADEMA tuu?
Tutoe miwani ya mbao, ni silka kwa binadamu kukosea au kupishana muono na wengine na bado wewe au wenzako wakawa sawa.
Na ikitokea tukakubali ubora wa CCM, kama taasisi ya kisiasa bora Africa ndio siku ushindi utapatikana kwa kuwa tutatafuta silaha sawasawa zitakazo kumuangamiza adui CCM.
Hata Tume ya uchaguzi ikibadilishwa wakati sisi hatubadiliki matokeo yatabaki hivi hivi.
Kundi la Nyani lile lile kitakacho badilishwa ni msitu.
TUNA KAZI KUBWA MBELENI.