Redio zetu zimetawaliwa na vipindi vya michezo

Redio zetu zimetawaliwa na vipindi vya michezo

Unapata wapi muda wa kusikiliza redio masaa matatu achilia mbali kipindi cha michezo? sikiliza dakika kumi au nusu saa endelea na mambo mengine achia wengine nao wasikilize ndio maana ya kipindi kuwa muda mrefu au mara kadhaa kwa siku.
 
Mpira ni pesa Dogo, mpira. Ni biashara kubwa saana, Mpira unaweza kua. Na nguvu zaidi ta dini. Acha wachambue, ndio kitu tunapenda, unataka wachambue bongo Fleva au maigizo? [emoji23]
 
Radio Tanzania kipindi cha michezo saa 2 kasorobo mpaka saa 2 kamili.

Robo saa inatosha kipindi cha michezo. siku hizi radio inakipindi cha michezo asubuhi masaa matatu na jioni masaa mawili na kila kipindi cha katikati kina segment ya michezo.

Yaani unaangalia mechi azam tv ikiisha unaangalia highlight ya mechi hiyo hiyo ikiisha unaangalia uchambuzi wa mechi hiyo hiyo. Ukimaliza unaweka wasafi fm unaskiliza uchambuzi, then unahamishia clouds unasikiliza.

Then asubuhi unasikiliza wasafi fm wanachambua, masaa matatu. Mchana ETV wanachambua masaa matatu, mwishowe inakuwa nchi ya wachambuzi [emoji2]

Maisha ya Tanzania Bara ni michezo tu
Na wachambuzi wa mpira ndo wanaongoza kwa kuwa na mishahara mikubwa
 
Baba yake Konso kashona virakaaaa...
'Matacone' mwake vinaulizanaaaaa...
Umekuja liniiiii...
Nimekuja janaaaa...
Kushinda leooo....oooo...
Titiiitiiii, tititiiiiiiii, tiiiiiiiiiiiii...

Hapo umetulia tuli ukisubiri sauti za kina Abdallah Majura, Nazir Mayoka, Sekioni Kitojo na wengine wengi...
 
Umenena kiongozi wachambuz kibao na a.k.a za kimagumashi wanatia kiingereza za kudownload kupamba wanajiona wamemaliza
 
Achana na hiyo, unamsikiliza mchambuzi anatoa maneno mepesi ambayo hata mtu wa kawaida ambaye kwake soccer ni jambo la mara moja anajibu. Unachambua kona ya Mesuit Ozil dakika 40 😂😂😂😂😂
 
Watu wanatofautiana muda wa kufanya kazi, basi kwa mantiki hiyo basi vituo vya redio visirushe kabisa matangazo asubuhi kwasababu watu wanafanya kazi.

Naona umetumia same reasoning iliyotumika kuzuia bunge live eti mida hiyo watu wanafanya kazi muda wa kutazama tv wanautoa wapi.
Reasoning za ki Magufuli
 
Achana na hiyo, unamsikiliza mchambuzi anatoa maneno mepesi ambayo hata mtu wa kawaida ambaye kwake soccer ni jambo la mara moja anajibu. Unachambua kona ya Mesuit Ozil dakika 40 😂😂😂😂😂
Wanachambua hadi demu wa Pogba kavaa nini, anaishi wapi, anafanta nini na marafiki zake ni akina nani,
 
mmm shida tu.yaani niliacha kusikiliza mimi,Nikisikiliza redio basi ni BBC , DOCHEVELE au sauti ya AMERICA.redio zetu hazina mvuto michezo muda wote.yaani redio mbongo kwisha kabisa
 
Radio Tanzania kipindi cha michezo saa 2 kasorobo mpaka saa 2 kamili.

Robo saa inatosha kipindi cha michezo. siku hizi radio inakipindi cha michezo asubuhi masaa matatu na jioni masaa mawili na kila kipindi cha katikati kina segment ya michezo.

Yaani unaangalia mechi azam tv ikiisha unaangalia highlight ya mechi hiyo hiyo ikiisha unaangalia uchambuzi wa mechi hiyo hiyo. Ukimaliza unaweka wasafi fm unaskiliza uchambuzi, then unahamishia clouds unasikiliza.

Then asubuhi unasikiliza wasafi fm wanachambua, masaa matatu. Mchana ETV wanachambua masaa matatu, mwishowe inakuwa nchi ya wachambuzi [emoji2]

Maisha ya Tanzania Bara ni michezo tu
Wachambuzi/ wachambaji wa simba na yanga. Wao timu nyingine haziwahusu.
Wanachambua hata mchezaji kufuta picha kwenye mtandao??? Pumbavu. Mechi inachambuliwa usiku, asubuhi na usiku tena.
Inakera kwelikweli
 
si afadhali na hizo,
kuna wale wa mchongo pesa..yaani kuanzia asbh hadi jioni vipindi vyote wanachezesha bahati nasibu.
 
Raia wengi wanapenda mambo mepesi yasiyo na faida kwao, kuchwa kutwa wanazungumza mpira!
 
Hata ukiangalia BBC news unaweza kukuta habari ni zile zile kwa masaa mengi sana mpaka ije breaking news, logic ni kuwa watu mbali mbali wanaangalia news kwa muda tofauti.
BBC wanafanya hivyo kwa sababu wanatangaza katika mabara na nchi tofauti zenye time zones tofauti. Hapa hata karedio cha wilaya kanatangaza mambo yalayale ya mpira asubuhi mchana na jioni!
 
Back
Top Bottom