Refa Omar Artan aliyezuiwa kuingia Marekani ateuliwa na UEFA kuchezesha Fainali ya Super Cup kati ya PSG na Aston Villa

Kwa nini wameandaa kombe la dunia kama kuna sheria dhidi ya kundi la watu flani?
Russia na mataifa mengine yaliyoandaa mashindano ya kombe la dunia hawajawahi kuzuia watu kuingia kushiriki mashindano.
Kuandaa kombe la dunia hakuifanyi nchi kuwa dampo la kukusanya kila anayekuja kwa kigezo cha kuangalia au kushangilia bali sheria na taratibu za kiusalama lazima zifuatwe kama zilivyopangwa na mamlaka husika.......

Hata kule Qatar baada ya kuandaa sheria na utaratibu za nchi hazikusimama ziwe za kiusalama au utaratibu wa maisha ya kila siku ya watu wa Qatar na ndio maana kulitokea malalamiko hasa katazo la kunywa pombe viwanjani......

Marekani kama nchi zingine zenye utaratibu na sheria kama kusimamia usalama au watu wanaoingia nchini mwao na wao kwa vigezo vyao kutoka kwenye taarifa za intelejensia zao wamejiridhisha kuwa hafai kuingia nchini mwao!!

Mimi na wewe hatujui lakini mtu kuwa refa hakumfanyi kuwa msafi kwenye maisha yake mengine ya nje ya soka!!!
 
Kuna watu wa itikadi fulani wanaponda saana hii michuano kufanyika US tena walivyo wajinga wanadai Trump katumia ubabe na ushawishi kupeleka mashindano huko.

Jamaa hawajui kuwa kabla hata Trump hajaingia madarakani tayari ratiba ya michuano ya WC ilishapangwa ifanyike huko.
 
Kisa yule mwanadada seneta ilhan omar ndio sababu Artan kazuiliwa kuingia

Ni ishu ya kisiasa na chuki tu utawala wa Trump
 
Reactions: Cyb
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…