Reginald Mengi aahidi milioni 20 Kila mchezaji, Serengeti Boys ikishinda mechi 2

Reginald Mengi aahidi milioni 20 Kila mchezaji, Serengeti Boys ikishinda mechi 2

Mzee Mengi amewaahidi vijana Tshs 5,000,000 kwa goli litakalofungwa kwanza. Magoli yamepatikana (manne) kama ya Netball vile, ambayo hayana manufaa kwetu kwani tumefungwa mengi.... Namshauri Mzee Mengi atoe Tshs 5,000, 000 kwa kila mchezaji atakayezuia goli kuingia upande wetu katika mechi zinazofuata.
⚽🥇🏟🇹🇿🇹🇿
 
Mechi ya jana sijaiona lakini Mtangazaji anasema kipa alifanya makosa yakapatikana magoli mawili ya wanigeria . Nafikiri uwezo wa Kocha ni mdogo kutojua golikipa mzuri ni Yupi . Yule ramadhani kabwili wa Yanga anachezea timu gani ya vijana?
Wakifanya mchezo watakosa kila kitu . Mechi ya majaribio ya Rwanda walitoka sare Rwanda akisawazisha dakika ya mwisho na Rwanda ni timu ndogo kuliko Angola na Uganda.
Ndiyo maana timu kubwa za ulaya zina jopo la makocha kusaidiana mawazo hapa tanzania kocha ni mmoja akichemsha mawazo timu imechemsha
 
Ahadi hiyo imetolewa na Mlezi wa timu ya vijana Serengeti Boys Dkt.Reginald Mengi pamoja na Kamati ya kuhamasisha ushindi wa timu hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, es salaam, Paul Makonda.

Michuano ya vijana ya AFCON inatarajia kuanza April 14, Tanzania ikiwa ni mwenyeji.

Serengeti Boys inahitaji kushinda mechi mbili ili kujikatia tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini Brazil mwaka huu.
View attachment 1069517

Sent using Jamii Forums mobile app
ndo washazikosa saas==
 
Nionavyo alishakipima kile kikosi akaona hakiwezi fika popote na ndio maana akatoa ahadi kubwa kiasi kile.
 
Hivi kweli mungu kwenye michezo yote iliyopo duniani akuna ata mchezo mmoja ambao ninaumudu kisawasawa kwamba ningeucheza ningeweza kuliletea sifa taifa? Yani ata draft kweli?

Si umejaliwa uchawi ndugu? Kuwa muwazi bwana
 
Nionavyo alishakipima kile kikosi akaona hakiwezi fika popote na ndio maana akatoa ahadi kubwa kiasi kile.
Itakuwa aisee alipima kina cha maji na fimbo kabla ya kuyakanyaga (kutumbukiza miguu).
 
Itakuwa aisee alipima kina cha maji na fimbo kabla ya kuyakanyaga (kutumbukiza miguu).
Umeonaeee. Sababu kikawaida ukipiga mahesabu kikosi kizima kile wachezaji zaidi ya 18 halafu kila mmoja umpe 20M na gari ni pesa ndefu mno hiyo ambayo mwisho wa siku kwa usawa huu tungebaki kushangaa tu.
 
Hizi ahadi ndio ziliharibu saikolojia ya madogo. Wakawa wanacheza wakiwazia m. 20 miguu inatetemeka akili hazifanyi kazi kisa mpunga. Nashauri hizi ahadi zisirudiwe zinawachanganya watoto hata wanakosa umakini. Mbona wakiwa nje ya nchi hucheza soka nzuri?
 
Point
 
Nionavyo alishakipima kile kikosi akaona hakiwezi fika popote na ndio maana akatoa ahadi kubwa kiasi kile.
Mh..Mengi hana utaalam na soka kiasi cha kuwa na uhakika 100% eti vijana hawapiti..Hata makampuni ya kubeti hayana uhakika
 
Back
Top Bottom