Rekodi yako ya muda mfupi sana wa safari kuendesha gari (private drive)

Rekodi yako ya muda mfupi sana wa safari kuendesha gari (private drive)

Makongo juu (enzi za makorongo barabara mbovu to Kijichi 30min) saa tano usiku
 
Mm rekod yangu ilikua hapa hapa mjini japo ilikua ni usiku...nilitoka tabata Hadi buza kwa dakika 9.... Na hyo ndo ilikua Mara ya kwanza kukimbiza gar hovyo bila kuwa na sababu za msingi
 
Uyole saa sita mchana ubungo shelly saa tatu usiku,gari ni coaster 12H-T kwangu ni muda mfupi hasa ukiangalia na gari lenyewe kwa kweli kumbukumbu hii sitasahau!
 
Ulitumia njia ipi kwenda kibada kwa dakk 20 maana ni kipengele! [emoji28] Na muda gani njia ilikuwa wazi hivyo!

Maana pale pa kulipia tickets darajani lazma ungekula dakika 2! Sina shaka hukufuata taa mkuu!
Gari ilikuwa na mbawa kama mbayuwayu
 
Nilitoka Moro to Dom (259km) kwa masaa 2 na nusu halafu jioni jioni hivi, nilikuwa na kitu cha Nissan Dualis. Weee weeee hiki kigari ni noma kinanyanyuka balaa haga ukitembelea Manual.
 
Kumbe jf wengi wenu mna magari alafu zikija nyuzi za majobless na wasio na ajira na ninyi mnachangia kulalamika[emoji23][emoji23]..SIJAPENDA KWAKWELI
 
Dodonma to Mwanza ni kama kilmeta 700; sawa na kwenda kms 100 kwa saa ili utumie masaa saba
Inamaana umeendesha klm 120 kwa saa hiyo 20 imekuwa ya kufidia pale ulipo punguza mwendo hivyo ulikuwa kasi sana.
Kukimbiza gari hutegemea hali ya chombo chako/gari, Barabara unayopitia, hali ya hewa/mvua, muda wa kuendesha ( mchana au usiku), unapita pita mjini au mashambani; na mwisho UNAJITAMBUA au unajitoa ufaham to kuendesha tu kama vile umesha kamilisha siku zako za kuishi
Binafsi sishabikii mtu anayekimbiza gari sana bila sababu za msingi mf: mtu anakimbiza gari kuwahi nyumbani kulala? unakimbiza gari wakati huna issue yeyote ya msingi inakusubiri?
USALAMA KWANZA!
Hesabu gani umepiga?? Dom mwanza 686km kwa masaa saba ni kama avg ya 98kph

Kuwa na average hio kwa gari ndogo ni mtihani
 
Hizi ni assumptions tu...uhalisia hakuna na wengi wenu mnasema ilikuwa usiku...sasa nashindwa kuelewa kama mlikuwa na akili timamu au pombe ndio ilikuwa leader
 
Mimi
Bukoba-Dsm 18 hrs
Safari ilianza saa 12 asubuhi dsm nimefika saa Sita Usiku.
 
Dar-Shinyanga. Kuondoka saa tano asubuhi, nikaingia saa sita usiku. Niliendesha mwenyewe na gari ilikuwa nisasan Serena.
 
Back
Top Bottom