Reli ya Dar-Tanga-Kilimanjaro-Arusha imeanza kujengwa; Dec, 2018 kuanza kazi rasmi, Kenya kuathirika

Tufanye mambo yetu kwa kuangalia maslahi yetu kama nchi badala ya kuangalia Kenya au Rwanda sijui!
 
Mbona mnaanza kuleta siasa wakati hii ni kodi yetu lazima itekelezwe
 
kwanza wameshalipalile deni la kukomboa bombadier zetu?
KONOIKE wameshalipwa?
Hiyo reli itakuwa(?) SGR au ni ile ile alioacha mkoloni?
NDOTO ZA AWAMU YA VI-WONDER KILA KITU CHA MOTO.
 
Kama anaikumbuka na reli ya nyumbani; ngoja na mimi nimpe kura yangu panapo na majaliwa! Wenye malori nao sasa watalazimika kutufikishia huduma huku vijijini kwenye matunda yanayoharibika kwa kukosa usafiri wa uhakika. Na nyie halmashauri mjitahidi basi kutuwekea japo changarawe magari yapite vizuri. Hongereni wafanikishaji wa haya.
 
Hivi ni kujengwa ama kuikarabati!!?
Safi sana,mambo mazuri.
 
Sukari ya tpc sasa itaanza kusafirishwa na reli bila kusahau soda za cocacola. Magufuli Vivaa

Usiseme Magufuli Vivaa sema ‘Mwl Nyerere wa Pili Vivaa’!!! Kama Majaliwa K Majaliwa angalikuwa kama Edward Moringe Sokoine, nchi ingefika mbali na Dr Magufuli hangekuwa na haja ya kufukuzana na mawaziri au watendaji wazembe kazini!!
 
Hii reli haiwezi kuwa profitable kwa sasa bora nguvu ielekezwe Tanga musoma, yaani mizigo na abiria wepi wa kutoka Arusha au Dar watapanda treni,,huku ni kupoteza pesa labda bdye sana ikijakuwa electric
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…