Reli ya standard gauge ya Rwanda na Tanzania ni kaburi la uchumi wa Tanzania

Reli ya standard gauge ya Rwanda na Tanzania ni kaburi la uchumi wa Tanzania

Mawazo ya kijinga sana haya, bado uko kwenye ujima.
Reli lazima iboreshwe iendane na kasi ya sasa. Muda ni muhimu sana zama hizi, hatuwezi poteza masaa karibu 20 kwa siku kisa uko safarini, hayo masaa yatumike ktk uzalishaji shughuli zingine.
 
Unadhani kwa maelezo yako hayo ndo viwanda vitajengwa. Nataka ujibu hoja kwa hoja.
Niambie hiyo reli inataka ibebe kitu gani ambacho kimeshindwa kubebeka kwa njia ya barabara,maji na anga.
Huko treni it a be a nini toka Rwanda ambacho ni kizito mno hakibebeki kwa mode of transportation zilizopo.
Mbona reli ya tazara na kati zipo na miundombinu mibovu hamsemi?.
Acha kunihamisha relini mi siwezi kukaa kimya kwa matusi yako nakusubiri hapa ulete hoja ya maana siyo ooo oh ukabila, sijui mange leteni hoja acheni mambo ya udaku kwenye serious issue.

Sisi tunaumizwa nyinyi mnashangilia.
Nitajibu hoja kama utakavyo wewe endapo hoja yenyewe imetolewa na BROAD MINDED person ....

By the way CRITICISM is ACCEPTABLE but not in everything ... muwe mwapinga jambo mkiwa na ENOUGH EVIDENCE to support your arguments .... They always say ... "NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK ..." And we call ourselves GREAT THINKERS ... hili ni tatizo ...
 
Mtoa mada hayo ni maono yako lakini sina uhakika kama umefanya hata research ndogo ndo ukaja na andiko hilo for your information hiyo reli itasaidia sana kwa wafanya biashara na at the same time itasaidia kutokuharibu barabara zetu amabazo zimekuwa zikiharibiwa na ma semi tera ya mizigo yanayo toka Rwanda/Tanzania/Rwanda.Wengine tumeshuhudia uharibifu wa barabara hizo na italahisisha kwa wasafiri ambao hutumia zaidi ya masaa mengi wakiwa barabarani kutoka let say dar to Kigali.
 
Eti tujenge reli pamoja na kenya?kweli ww ni kilaza.
Ni sawa naweza kuwa kilaza kweli lakini naomba unieleze huko Rwanda treni itabeba vitu gani visivyobebeka kwa gari, meli au anga.
Kenya kuna priority nyingi compared to Rwanda.
Kama haitoshi reli za ndani tu zinapumulia mashine. Acha unafiki siku nyingine muwe mnatumia akili zenu kuwaza siyo za kuazima. Rwanda inayozidiwa ukubwa hata na wilaya ya chunya tutapata nini cha ajabu tulichokosa kwa uwepo wa hiyo standard gauge.
Jiulize inajengwa kwa priority ipi kama siyo kurahisisha wizi tu wa mali za tz kwenda Rwanda kutoka migodini mwetu.
 
Nitajibu hoja kama utakavyo wewe endapo hoja yenyewe imetolewa na BROAD MINDED person ....

By the way CRITICISM is ACCEPTABLE but not in everything ... muwe mwapinga jambo mkiwa na ENOUGH EVIDENCE to support your arguments .... They always say ... "NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK ..." And we call ourselves GREAT THINKERS ... hili ni tatizo ...
Nilidhani umeleta hoja kumbe bado unalaumu tu. Basi endelea kulaumu.
Wewe ungekuwa broad minded huwezi kushangilia upuuzi huo.
 
Umeandika maneno Mengi lakini ujinga mtupu,chuki zako dhidi ya maendeleo ya watanzania itakoma lini kwenu wahafidhina?

Umesahau tuna barabara ya lami toka TAnzania hadi Rwanda kwa miaka mingi sasa Mbona hatujayaona madhara hayo?

Unauhuru wa kuandika mawazo yako lakini siyo maneno yanayofanana na sumu! Shindwa na ulegee tunataka viongozi wenye mawazo ya kuwaza kila kukicha kuturahisishia njia za mawasiliano kwenye ulimwengu huu wa sayansi na tekinolojia siyo kutufungia ndani peke yetu.

Ikiwezekana Mhe rais abuni yeye na kiongozi wa Afrika kuiunganisha Nchi yetu na Dunia tuweze kusafiri na kusafirisha bidhaa zetu Kwa unafuu zaidi hayo unayowaza ni mawazo ya kututakia mabaya watanzania.
 
Mtoa mada katoa mada nzuri tu japo kuna wenzi wetu wana mkosoa

Nilivyoelewa point kuu ni kwamba hakatai kujengwa reli, ila ingeangalia ina athari zipi za kiuchumi kwa kuunganisha na nchi hiyo, na ametoa mapendekezo afadhali tungejenga aina hiyo ya reli na Kenya sababu tunafanya nao biashara kubwa kubwa au kukarabati reli ya Tazara na kuwa standard gauge tungelisha ukanda huo wenye mizigo mingi na ni nchi kubwa

Na hofu yake nyingine mtoa mada isije kuwa Rwanda akatumia reli hii kupata rasilimali zetu hapa refer DRC

Mtoa mada ana hoja sema muda unataka tuwe connected na wenzetu labda na inchi nyingine muda ukifika tuta unganishwa nao na bila kusahau reli itasaidia ukanda wa nchi yetu sehemu za kati mpaka magharibi na kuna shughuli nyingi za kiuchumi

Kinachonikera kuhusu haya ma reli na ndege ni kupewa kipaumbele kwa wakati huu wakati maji,umeme,madawa hospitalini,elimu havijakaa sawa tungeimarisha haya ndo turukie hayo
 
Ni sawa naweza kuwa kilaza kweli lakini naomba unieleze huko Rwanda treni itabeba vitu gani visivyobebeka kwa gari, meli au anga.
Kenya kuna priority nyingi compared to Rwanda.
Kama haitoshi reli za ndani tu zinapumulia mashine. Acha unafiki siku nyingine muwe mnatumia akili zenu kuwaza siyo za kuazima. Rwanda inayozidiwa ukubwa hata na wilaya ya chunya tutapata nini cha ajabu tulichokosa kwa uwepo wa hiyo standard gauge.
Jiulize inajengwa kwa priority ipi kama siyo kurahisisha wizi tu wa mali za tz kwenda Rwanda kutoka migodini mwetu.
Haha,wakenya mtakufa kwa pressure, nani alikwambia SGR yetu inaishia Rwanda tu?hizo Mali zinabebeka kwenye train tu?mmeshindwa kufanya electrification kwenye SGR yenu mnaleta propaganda humu.
 
Mtoa mada hayo ni maono yako lakini sina uhakika kama umefanya hata research ndogo ndo ukaja na andiko hilo for your information hiyo reli itasaidia sana kwa wafanya biashara na at the same time itasaidia kutokuharibu barabara zetu amabazo zimekuwa zikiharibiwa na ma semi tera ya mizigo yanayo toka Rwanda/Tanzania/Rwanda.Wengine tumeshuhudia uharibifu wa barabara hizo na italahisisha kwa wasafiri ambao hutumia zaidi ya masaa mengi wakiwa barabarani kutoka let say dar to Kigali.
Reli ni mhimu lakini hoja yangu iko pale pale ujenzi huo uanze na reli za ndani kwa kiwango hicho na kufufua zilizokufa. Pia pamoja na uharibifu wa barabara tambua kuwa nyingi zinajengwa chini ya kiwango hivyo huwezi kukwepa kuharibika kwake hata ikiwa reli itakuwepo.
Malawi, msumbiji kuna transit nyingi mno lakini hamsemi wangeanza huko.
Imagine barabara ya Uyole mbeya to kasumulu boarder inabeba mizigo mingi mno lakini tangu ijengwe huoni palipotitia ndo kusema hakuna mizigo.
Abiria kusafiri Dar to kigali kwa basi ni safe kuliko treni endapo road barriers zitapunguzwa zisizo na maana.
Yaani Rwanda pana nini cha ajabu. Kwa sasa usafiri wa abiria kwa basi na ndege ni bora na unatosha. Watu wenyewe waliopo Rwanda unaweza kuwasombelea na vyombo vyao kwa siku tatu tu wakaisha.
 
Mtoa mada katoa mada nzuri tu japo kuna wenzi wetu wana mkosoa

Nilivyoelewa point kuu ni kwamba hakatai kujengwa reli, ila ingeangalia ina athari zipi za kiuchumi kwa kuunganisha na nchi hiyo, na ametoa mapendekezo afadhali tungejenga aina hiyo ya reli na Kenya sababu tunafanya nao biashara kubwa kubwa au kukarabati reli ya Tazara na kuwa standard gauge tungelisha ukanda huo wenye mizigo mingi na ni nchi kubwa

Na hofu yake nyingine mtoa mada isije kuwa Rwanda akatumia reli hii kupata rasilimali zetu hapa refer DRC

Mtoa mada ana hoja sema muda unataka tuwe connected na wenzetu labda na inchi nyingine muda ukifika tuta unganishwa nao na bila kusahau reli itasaidia ukanda wa nchi yetu sehemu za kati mpaka magharibi na kuna shughuli nyingi za kiuchumi

Kinachonikera kuhusu haya ma reli na ndege ni kupewa kipaumbele kwa wakati huu wakati maji,umeme,madawa hospitalini,elimu havijakaa sawa tungeimarisha haya ndo turukie hayo
Ulichoeleza ndiyo hoja yangu kuu. Wengi wanaona mwisho wa urefu wa pua zao.

Sijakataa reli. Kwa sasa hali ya Kongo huenda ikawa nzuri wakongo man wakadhibiti mianya ya ukwapuaji raslimali zao zinazoilea Rwanda hivyo tayari yuko prepared kwa Tanzania kama alternative yake.
Na ili kufanikisha hilo yeye aweza vuta mali nyingi hasa dhahabu ktk utawala wa magu zikatosha kuilea Rwanda miaka 40 huko.
Akili ya wanyalu ni hatari sana.Walivamia hifadhi za katavi ujangili tuliposhituka tembo walishaisha na kusafirishwa kwa njia ya maji ziwa Tanganyika kabwe, kirando, ikola na karema hadi Rwanda.

Treni inabeba mzigo mkubwa mno na ss ni wazembe mno ktk masuala ya inspection yaani kuhamisha resources zote kwenda kule ni rahisi sana.
Hata sasa zinaenda lakini si kwa kiwango sawa na watakapotumia reli.

Nashukuru kwa kunielewa na kutoa ufafanuzi.
 
Kagame mjanja mjanja sana, bora hiyo reli ingejengwa from dodoma to Arusha - kenya
Unajua unapo argue na mtu ndo unajua ana upeo gani. Rwanda,burundi,congo ni land locked country na uganda so reli ya kati ni muhimu sababu ya manufaa makubwa ya kiuchumi kwa tanzania. Kwa sasa mza dar ni masa 24 ndo ufike. Biashara inakuwa ngumu na gharama ni kubwa. Reli ikiwepo ni masaa saba tu.huoni itasereresha uchumi mbele
 
Aisee kama haujasoma rudi shule kwa kweli khaa so unamaanisha sisi tunajenga reli sabu ya kagame? Idiotic thinking hii... Hahaha unajua faida za reli kwa nchi? Hivi gharama za usafirishaji wa mizigo Kwa njia ya reli ni sawa na njia ya bara bara? Hahaha nacheka kwa dharau sababu haujielewi...afu sijaona hoja why iwe ndio chanzo cha kuanguka uchumi?
Tulitakiwa tuambiwe ujenzi wa hiyo reli utakuwa na manufaa gani na kuna nini ambacho tumekuwa tukikikosa kwa kutokuwepo kwa hiyo reli.

Mfano, kama kuna biashara kuu ambayo inafanyika kati ya hizi nchi mbili au kuna biashara nyingi zinazofanyika na zina manufaa makubwa kwa nchi yetu hapo tungepewa sababu ya kuboresha hizo biashara na kuinua uchumi wa nchi pamoja na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Tuambiwe ni manufaa gani tutapata kama nchi na si kutuambia tu upembuzi yakinifu umefanyika na wanaona itafaa kujenga hiyo reli...
 
wenye akili tumekuelewa ila wengine watakudhihaki,umeuliza vyema kwanini isijengwe standard gauje ya kwenda Kenya?, Kenya ina masoko makubwa ya kimataifa,tungefaidika sana,lakini wacha yapite tu?
 
Back
Top Bottom