Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Reli ya Usambara, Moshi-Tanga ndiyo reli ya kwanza kujengwa ndani ya Tanganyika. Ilijengwa miaka ya 1890's. Reli hiyo ilianza kujengwa na kampuni binafsi na baadaye ikachukuliwa na serikali ambayo iliimalizia hadi Arusha. Lengo kuu lilikuwa kuunganisha bandari ya Tanga na eneo la kaskazini ambako kulikuwa na mashamba makubwa ya wakulima wa Kijerumani. Lakini kwenye plan ilikuwa reli hiyo ifike hadi Mwanza.
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia reli hiyo ilifanya kazi nzuri sana ya kusafirisha wanajeshi kwenda Tanga. Kwenye WWI, vita ya kwanza kabisa kupiganwa ndani ya Tanganyika ilipiganwa Tanga. Inaitwa vita ya Tanga au vita ya nyuki. Kwenye hiyo vita kamanda wa Ujerumani von Lettow-Vorebeck alikuwa amepanga kuwa ili kudeal basi atashambulia sehemu yake nyeti, reli ya Mombasa-Uganda. Hivyo wanajeshi wengi walikuwa wamekusanyika huko Moshi.
Baada ya kusikia kuwa manowari za Uingereza zilikuwepo huko Tanga, akaanzisha oparesheni ya haraka haraka kusafirisha vikosi kuelekea Tanga kwa treni. Kwenye vita hiyo jeshi la Wajerumani na Waafrika 1,000 lilipambana na Waingereza na Wahindi 8,000. Jeshi la Uingereza lilipigwa vibaya sana. Huyu jamaa Vorbeck alikuwa kamanda hasa. Wahindi waliounda sehemu kubwa ya jeshi la Uingereza walichinjwa sana. Inasemwa watu 1,500 walifariki huku wajerumani wakipoteza kama watu 80 hivi. Baadaye jeshi lao likakimbilia Zanzibar kwa aibu kubwa.
Kwenye hiyo vita kulizuka nyuki waliowashambulia askari, hasa wa jeshi la Uingereza. Ndiyo maana inaitwa pia vita ya nyuki.
Tulipopata uhuru serikali ikajenga Coastal Railway ili kuunganisha reli ya Usambara na reli ya kati. Wazo hilo la kuunganisha reli ya Usambara na ya kati alikuwa nalo Lettow Vorbeck. Aliona jinsi ilivyokuwa vigumu kusafirisha wanajeshi kutoka reli ya kati kuelekea maeneo ya kaskazini.
Wajerumani walikuwa watu wa kazi hasa.