Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
- Thread starter
- #41
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe jifunze hiyo lugha unayoiparamia ya Kiingereza kwanza kabla ya kujishaua.
Kwanza kabisa nawasalimia.
Leo napenda kuongelea makundi haya mawili duniani. Dini na Sayansi.
Kumekuwa na mjadala mkubwa mno duniani kuhusu haya makundi. Kwanza kabisa kabla ya kuendelea ninapenda kuongelea kitu kinachoitwa faith. Kila mtu dunia yupo na faith kuanzia mototo mpaka Mzee. Unaweza ukawa na faith na daktari, baba, mke wako, elimu, Mungu nk.
Katika suala la faith haijalishi kuwa mwanasayansi au mtu wa dini wote wanakuwa na faith.
Sasa tunakuja kwenye upande wa dini. Dini zimekuwapo miaka na miaka na zinaendelea kuwepo. Msingi mkubwa wa dini ni kwenye swali la WHY!? Kwanini kuna magonjwa, kwanini jua linatoa mwanga nk. Zipo dini za aina tofauti tofauti zingine zipo za zinazoamini Mungu mmoja, zingine Miungu wengi na zingine haziamini uwepo wa Mungu.
Katika kutafuta kujibu swali la why!? Ndipo zinatokea dini na Imani tofauti tofauti kulingana na ujibuji wa swali hilo.
Kwa upande wa sayansi. Kila mtu ni mwanasayansi tangu akiwa mototo. Msingi mkubwa wa sayansi ni kujibu swali la HOW. Mfano ukipewa USB uchomeke kwenye laptop Utakuwa na observation, utatengeneza Hypothesis, Experiment baadae conclusion. Kama conclusion itakuwa poa utatengeneza theory. Kwamba kumbe kuchomeka USB kwenye Laptop alama inayoonesha logo ya USB inatakiwa kuwa juu.
Sasa basi. Kutokana na maelezo haya ni kwamba mwanasayansi na waumini wa dini hawana ugomvi wowote. Bali ugomvi uliopo ni Dini baina ya Dini au Wanasayansi baina ya Wanasayansi.
Ni hayo tu.
Umerukia kwingine sasa. Lakini umeelewa kuwa sayansi haijibu maswali ya WHY au bado unabisha!?Wewe jifunze hiyo lugha unayoiparamia ya Kiingereza kwanza kabla ya kujishaua.
Complementary ni nini?
Lugha unayotumia tu huijui, sasa mimi nitakuelewaje?
Ninauhakika pale ulipoandika neno dini ulikuwa unamaanisha sayansi.Umetoa mfano wa kutumia USB na ukajiuliza how it work na mambo mengine. Ningependa nikuulize, je ulipokuwa mtoto au unajifunza dini ulipewa nafasi ya kujiuliza kufanya observation, kujenga hypothesis, kufanya experiment na baadaye kuja na conclusion?
Kama ilivyo kwenye comment yangu ya hapo juu.Ukipata nafasi ya kuchunguza maisha ya wanyama, wapo wanaofanya processes zote ulizozitaja kwenye mfano wako wa USB. Kwa mfano nyani wanapotaka kuiba mahindi...wanafanya observations, wanafanya experiment, wanafanya conclusion, na labda wafanya hypothesis zao...je na wao ni wanasayansi...
Kama nilivyosema hapo juu kwamba sayansi ni study of nature siyo wazo.Je hili wazo liwe la kisayansi ni lazima liwe observation, hypothesis, experiment and conclusion. Je haiwezekani kuwa ni la hypothesis na conclusion....
Ninauhakika pale ulipoandika neno dini ulikuwa unamaanisha sayansi.
Kama ulikuwa unamaanisha sayansi basi najibu kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa tunatakiwa tujue science imetokea wapi. Science imetokana na philosophy of Nature au Natural Philosophy.
Kwa kifupi sayansi yenyewe inajihusisha na namna nature inavyofanya kazi.
Sayansi is the study. Siyo kupewa nafasi nawingine ukiwa mtoto uweze kufanya kitu.
Nilipokuwa ninatoa mfano wa kuchomeka USB kwenye laptop nilikuwa naeleza namna sayansi ilivyo. Kwa kulingana na issue hiyo hiyo ya kusoma nature either huyo mtoto aliona siku moja USB imechomekwa na siku nyingine haijachomekwa.
Kwa lengo la kujifunza neture mtoto mtoto akijiuliza kwanini USB haipo kwenye laptop au kwanini imechomekwa atakuwa na mzigo mkubwa sana wa kujibu swali hilo.
Lakini akijiuliza how USB inakuwa kwenye laptop na inakuwa haipo kwenye laptop itakuwa ni simple kwake kuanza practical na kufikia conclusion.
Kama kuna swali jingine katika hili nitajibu.
Kama ilivyo kwenye comment yangu ya hapo juu.
Sayansi is the study.
Ku process why na how haina shida kwa wanyama hao. Lakini sayansi imeepuka burden ya why.
Why inakutaka ujibu reasons.
How inakutaka kutoa methods
Vilevile unatakiwa kujua How ikishakuwa kwenye conclusion nzuri tunapata theory, law au formula.
Tuje kwa nyani anataka kuiba mahindi.
1. Kama nyani tayari huwa anaiba mahindi na amekuta nyani wenzake wakiwa wanaiba mahindi huyo huyo atatumia formula au law aliyoikuta ikewekwa na nyani wa kwanza ya jinsi ya kuimba mahindi. Sasa hebu jaribu kufikiria huyo nyani sasa anajiuliza kwanini ninaiba mahindi!?
2. Kama nyani ni Mara ya kwanza yupo pekee yake hajawahi kuiba mahindi na anataka kuiba mahindi.
Yupo na njaa ameona mahindi na nyani anajua hayo mahindi ni chakula.
(Naweka kwanza assumptions ili tuweze kutengeneza scenario)
Sasa huyo nyani akianza kujiuliza why ninataka kuiba hayo mahindi!? Sidhani nyani huyo kama ataweza kuiba hayo mahindi.
But akijiuliza how ninaweza kuiba hayo mahindi. Tayari ataanza kutengeneza hypothesis na kuzijaribu.
Mwisho sayansi ni study of nature how works but not why. Nature tayari ipo inafanya processes zake. Hatuwezi tukawa na mzigo wa kujiuliza why. Hilo swali linaachwa kwenye dini.
Kama nilivyosema hapo juu kwamba sayansi ni study of nature siyo wazo.
Tunaposoma namna nature inavyo operate siyo wazo. Nature ipo na inaendelea kuwepo. Huwezi ukaleta wazo from no where nje ya nature. Vitu vinavyohusiana na sayansi ni vitu vilivyopo.
Kama nilivyosema Sayansi is the study inakanuni zake. Haiwezekani uruke steps.
Lazima upitie process za kisayansi.
Observation, hypothesis, experiment, conclusion finally (Theory, formula, law or principle)
Haiwezekani ukafanya ukaandika hypotheses kisha ukarukia kwenye conclusion without testing them. Lazima zijaribiwe tuone matokeo ya hizo hypothesis.
Conclusion ipi utaifanya hujafanya testing ya hiyo hypothesis!?
Discipline za dini hazihusiani na process hizo ulizozisema. Dini yenyewe inajihusisha sana na kujibu why.Asante kwa jibu lako. Nilikuwa nauliza dini. Je ulipopata mafunzo ya dini ulipewa nafasi za kufanya observations, kujenga hypothesis kufanya experiments, kutoa conclusion? Nimeuliza hivyo kwa sababu umesema sisi wote ni wanasayansi. Au tusime tunakuwa wanasayansi kwenye mambo yanayofanana na USB, na katika mambo kama ya dini tunapuyanga?
Sina uhakika kama kweli umesoma physics. Sikutegemea swali kama hili.Kwa hiyo Albert Einstein alifanya experiments gani alipokuja na theory of relativity?
Discipline za dini hazihusiani na process hizo ulizozisema. Dini yenyewe inajihusisha sana na kujibu why.
Hebu jaribu kusikiliza hii video kidogo
Wewe jifunze Kiingereza kwanza kabla ya kuparamia habari za "complementary".Umerukia kwingine sasa. Lakini umeelewa kuwa sayansi haijibu maswali ya WHY au bado unabisha!?
Wewe jifunze Kiingereza kwanza kabla ya kuparamia habari za "complementary".
Nimekuwekea list ya maswali muhimu wanayojadikmli wanasayansi.
Kuna swali "Why do we dream".
Kuna swali "Why is there stuff".
Nimekueleza Newton alivyoanza kujiukiza "why do things fall down and not up?".
Haya si maswali ya kisayansi?
We jamaa kwani kila kitu unachoandika hapa ni mawazo yako!?Naona haya mawazo unayatoa kwa sababu mtu au kikundi cha watu kimekushawishi kuwa dini inahusika na why na science inahusika na how? Kama unashindwa kujieleza na kutaka mimi ningalie video, basi vitu unavyotaka kuzungumza sio mawazo yako.
Wewe jifunze Kiingereza kwanza kabla ya kuparamia habari za "complementary".
Nimekuwekea list ya maswali muhimu wanayojadikmli wanasayansi.
Kuna swali "Why do we dream".
Kuna swali "Why is there stuff".
Nimekueleza Newton alivyoanza kujiukiza "why do things fall down and not up?".
Haya si maswali ya kisayansi?
We jamaa kwani kila kitu unachoandika hapa ni mawazo yako!?
Uneongea kuhusu relativity hayo ni mawazo yako!?
Hata hii issue ya sayansi hayo ni mawazo yako!?
Ndio maana watu wanaishi kwa kutegemeana. Kuna mkulima, Mwalimu, mfanyabiashara nk.
Sasa tukianza kila mtu atoe only mawazo yake bila references tutakuwa tunarudi kwenye ujima.
Ndio maana kuna vitabu.
Umeuliza maswali nimekupatia ufafanuzi, na kukueleza theory of relativity ilikuwa na experiments zake.
Sasa unaaza kujadili namna ya uwasikishaji wa mada eti mawazo ya watu vikundi nk!!!
Wewe leta maelezo kuhusu who science answer WHY question.
Twende taratibu sasa.Mimi nilimwekea mfano ambao anaweza ku-relate nao. Wakulima wa mihogo wanaona mazao yao yanakufa kwa sababu zisizojulikana na serikali ikatuma mwanasayansi wa botania, je mwanasayansi huyu anatajibu WHY au HOW? naona karuka swali.
Bro!! Tunabishana vitu simple mno.Kama unajaribu kurusha mistari katika mada ambazo unadai una utaalamu nazo ni lazima ujitosheleze angalau katika basics. Inaonyesha umesoma masoma ya sayansi kwa kufundisha na kwa kutumia models ambazo tayari zimeshafanyiwa kazi na kurahisishwa. Hivyo kwa upande wako unaweza kusema science inajihusisha na HOW.
Lakini kwa wale waliofanya groundbreaking discoveries katika science kama Newton, Einstein na wengine WHY was part of their work.