Religion and Science hazishindani

Religion and Science hazishindani

Yes. Nadhani sasa umeelewa tofauti ya sayansi na dini.
Katika context ya hii thread nadhani nimeeleweka.
Kunatakiwa kusiwepo ugomvi kati ya sayansi na dini maana kila mmoja anakuwa na direction yake.
Dini inahusika na moral wakati sayansi inahusika na kujua nature inavyofanya kazi.
Moral!!!!?? Is it moral kumwambia mtoto wa miaka mi4 kwamba ataenda kuchomwa milele hasipoamini Yesu ni Mungu?
 
Sio kweli kwenye sayansi kuna mambo hayatakiwi kupingwa.... bali unatakiwa kupinga ukiwa na data. No data no right to speak... kaa kimya kama hauna cha kuongea. Sayansi imeweka misingi ya kuendea jambo "hypothesis".. actually unapata umaarufu kwenye sayansi kwa kumpinga tafiti ya mwengine with facts.
Ndugu unajua tunaongelea nini!?
Hapa tunaongelea Religion vs Science.
Nahisi kama upo nje ya mada.
 
Moral!!!!?? Is it moral kumwambia mtoto wa miaka mi4 kwamba ataenda kuchomwa milele hasipoamini Yesu ni Mungu?
Upo out of tune mzee. Soma kwanza ujue tunaongelea nini!?
 
Kwanza:
Tusiongelee wenzangu.
Hapa tupo kwene mjadala. Kila mtu yupo na right ya kuweka mawazo yake.
Siyo kwamba mmoja anakuja Ku validate mawazo ya wengine na kutoa marks.

Nadhani umenielewa hapo.
Turudi kwenye topic.

Hapa topic inahusu relationship kati ya dini na sayansi. Je, kuna tatizo lolote baina yao mpaka upande mmoja una laumu upande mwingine!?
Hiyo ndio context ya hii thread.

Sasa katika context hiyo nimejaribu kueleza kuwa Science yenyewe inajikita kuelezea HOW nature operates wakati upande wa dini unajikita kueleza WHY nature exists.

Hata hii kirahisi tu mnashindwa kuelewa!?
Mkuu tofauti kubwa kati ya dini na sayansi ni hii... dini inakwambia kwenye pango ameingia Simba thats it, you have to believe it if not utakiona cha mtema kuni, but sayansi inakwambia you dont have to believe do the following kujua ukweli kama Simba ameingia kwenye pango kwa kufanya yafuatayo.. 1. Tuchunguze na tujihakikishie kwamba hakuna other exit kwenye pango 2. Tumwage unga kwenye all exist tulizoziona ili akitoka tutaona nyayo zake... 3. Let do that for 5 to 6 days kuwa na uhakika zaidi kwani lazima atatoka kwenda kutafuta chakula 4. Kwa siku hizo hasipotoka basi tujiulize itamchukua muda gani simba kufa na njaa 5. Baada ya huo muda kupita itabidi tuingie ndani ya pango kutafuta mzoga wake kwa kuwa atakuwa amekufa. 6. Tunakuja na conclusion kwamba kwenye pango kulikuwa na Simba au hakukuwa na Simba...

Unadhani ni njia gani inaweza ikakupa uhakika wa jibu sahihi?
 
Ndugu unajua tunaongelea nini!?
Hapa tunaongelea Religion vs Science.
Nahisi kama upo nje ya mada.
"Vivyo hivyo kwenye sayansi kuna mambo mengi tu yamewekwa na hutakiwi kuhoji".. kwenye majibu yako kuna sehemu umeandika hayo maneno na ndio napingana nayo... so usiniambie nipo nje ya mada. Kumbuka maelezo yanaundwa na series of statements... na katika kila statement inaweza ikawa kweli au uongo.
 
Mkuu tofauti kubwa kati ya dini na sayansi ni hii... dini inakwambia kwenye pango ameingia Simba that it you have to believe it if not utakiona cha mtema kuni, but sayansi inakwambia you dont have to believe do the following kujua ukweli kama Simba ameingia kwenye pango kwa kufanya yafuatayo.. 1. Tuchunguze na tujihakikishie kwamba hakuna other exit kwenye pango 2. Tumwage unga kwenye all exist tulizoziona ili akitoka tutaona nyayo zake... 3. Let do that for 5 to 6 days kuwa na uhakika zaidi kwani lazima atatoka kwenda kutafuta chakula 4. Kwa siku hizo hasipotoka basi tujiulize itamchukua muda gani simba kufa na njaa 5. Baada ya huo muda kupita itabidi tuingine ndani ya mpango kutafuta mzoga wako. 6. Tunakuja na conclusion kwamba kwenye pango kulikuwa na Simba au hakukuwa na Simba...

Unadhani ni njia gani inaweza ikakupa uhakika wa jibu sahihi?
Na hapa nakujibu Religion na Science. Kwa kuongezea Religions zinabeba mitazamo ya watu wa kale their experience, culture na mitazamo yao kuhusu vinavyowazunguka... kila generation ilikuwa na namna inavyo-perceive mambo na watu huwa hawafanani mawazo na ndio maana tuna mrundikano wa imani za dini... Sayansi imetokana na kutokubaliana na hizo primitive ideas, unaposema dunia ni flat basi sayansi haikutaki uamini bali uingie field uthibitishe. Unaposema kwamba watu wanaharisha kwasababu wamelaaniwa kwa kutofanya ibada ( hapo mtu ataona dini imejibu swali la why) lakini kwenye dini jibu sio lazima liwe sahihi... kwenye dini kusipokuwa na majibu sahihi hilo ni tatizo kubwa ila kwenye sayansi kusipokuwa na majibu sahihi there is no problem.. kwasababu mitazamo ya sayansi inabadilika kutokana na data zinasemaje.
 
Mkuu tofauti kubwa kati ya dini na sayansi ni hii... dini inakwambia kwenye pango ameingia Simba that it you have to believe it if not utakiona cha mtema kuni, but sayansi inakwambia you dont have to believe do the following kujua ukweli kama Simba ameingia kwenye pango kwa kufanya yafuatayo.. 1. Tuchunguze na tujihakikishie kwamba hakuna other exit kwenye pango 2. Tumwage unga kwenye all exist tulizoziona ili akitoka tutaona nyayo zake... 3. Let do that for 5 to 6 days kuwa na uhakika zaidi kwani lazima atatoka kwenda kutafuta chakula 4. Kwa siku hizo hasipotoka basi tujiulize itamchukua muda gani simba kufa na njaa 5. Baada ya huo muda kupita itabidi tuingine ndani ya mpango kutafuta mzoga wako. 6. Tunakuja na conclusion kwamba kwenye pango kulikuwa na Simba au hakukuwa na Simba...

Unadhani ni njia gani inaweza ikakupa uhakika wa jibu sahihi?
Unarukia mada mzee. Hii topic imezidi limit ya uwezo wako wa kufikiri.
 
"Sayansi na dini hazina ugomvi wowote bali ugomvi upo kati ya dini na dini, wanasayansi kwa wanasayansi" ~ damn go to the science class alafu waambie your nonsense ulimwengu una umri chini ya miaka 10000.. if you think niko nje ya topic usiniquote.
 
Maandiko yote ya dini yamejaa sayansi binadamu tuliambiwa usimuache elimu aende zake ili tuweze kuyafichua hayo maandiko
Ingawa naamin elim ya darasan ni muhim sana ktk maisha haya lkn siyo inayozungumziwa na biblia kuwa mshike sana elimu usimwache aende zake wengi hulitamka fungu hili nusu tuu lkn linasomeka kuwa " mshike sana elim usimwache aende zake maana yeye n uzima wako" uzima unaozungumziwa hapa n wa milele ______utaona hapo kuwa phizikia biolojia chemia historia english kiswahil wakadhalika ndan ya hizo elimu hakuna uzima wowote mule na hata ukisoma hayakupi uzima wa milele (ingawa n muhim tusome kwa maendeleo yetu hapa dunian) ko linapozungumzwa hapo n elim ya neno la MUNGU ambalo litoa uzima wa milele
 
Ni maneno yanayotoka kwenye vyanzo ambavyo sio vya uhakika na hayathibitishiki kua ni ya kweli kama rumors au mtu fulani aliambiwa na fulani kua fulani alifanya jambo fulani
Hapo nimekusoma mkuu
 
Yaani utuambie mtu anazaliwa na mwanamke mwenye bikra alafu isipingane na sayansi?
WANASAYANSI HAWAWEZI KUSHANGAA MWANAMKE BIKRA KUJIFUNGUA..
NI KITU CHA KAWAIDA KABISA, BIKRA KUJIFUNGUA, HII MBONA WALA HAIPINGANI NA SAYANSI.

Kwanza, wengi tunachanganya na kushindwa kutofautisha VIRGINITY na HYMEN.

VIRGINITY (ubikira/bikra) - ni ile hali kwamba uke wa mwanamke haujawahi kushiriki kuingiliwa na uume wa mwanaume wakati wa kufanya mapenzi.

HYMEN - ni ule utando wa misuli laini unaoziba sehemu ya uke.

Mwanamke anaweza kuwa bikra na asiwe na huo utando (hymen)...
Siyo kila bikra basi atakuwa na huo utando.

Kuna wasichana wengine wanazaliwa hawana huo utando, na kuna wengine wanazaliwa nao lakini kadri wanavyokua (grow up) basi ule utando ukatoweka kwa sababu mbalimbali pasipo hata kushiriki ngono na mwanaume.

TURUDI KATIKA BANDIKO LAKO HAPO.

Ndiyo, kisayansi inawezekana kabisaaaaaa mwanamke bikra kupata Ujauzito na kujifungua.

Mimba inatungwa kwa namna nyingi.

Na wala siyo lazma eti uume uingie kwenye uke na kumwaga manii za kurutubisha yai la uzazi la mwanamke na kutunga mimba (fertilization).

Mimba inaweza kutungwa kwa mwanamke bikra kupitia njia mbalimbali mfano:-

• Artificial insemination.
• In Vitro Fertilization (IVF)

Na mwanamke Bikra aliyepata mimba, bado atahesabika kuwa ni Bikra vile vile ikiwa tu kama hakuingiliwa ukeni kwake na uume wa mwanaume.

Rejea tena maana ya VIRGINITY na HYMEN..., kisha jifunze IN VITRO FERTILIZATION (IVF) ni nini? na pia jifunze ARTIFICIAL INSEMINATION ni nini?

Kisha kaa kwa kutulia TAFAKARI halafu nina uhakika utanielewa!

Na utakubali kile nilichokiandika hapa kuwa, "Ndiyo ni kweli inawezekana kabisa mwanamke bikra akabeba mimba na kujifungua mtoto na kisha bado mwanamke huyo akabaki kuwa ni bikra"
 
WANASAYANSI HAWAWEZI KUSHANGAA MWANAMKE BIKRA KUJIFUNGUA..
NI KITU CHA KAWAIDA KABISA, BIKRA KUJIFUNGUA, HII MBONA WALA HAIPINGANI NA SAYANSI.

Kwanza, wengi tunachanganya na kushindwa kutofautisha VIRGINITY na HYMEN.

VIRGINITY (ubikira/bikra) - ni ile hali kwamba uke wa mwanamke haujawahi kushiriki kuingiliwa na uume wa mwanaume wakati wa kufanya mapenzi.

HYMEN - ni ule utando wa misuli laini unaoziba sehemu ya uke.

Mwanamke anaweza kuwa bikra na asiwe na huo utando (hymen)...
Siyo kila bikra basi atakuwa na huo utando.

Kuna wasichana wengine wanazaliwa hawana huo utando, na kuna wengine wanazaliwa nao lakini kadri wanavyokua (grow up) basi ule utando ukatoweka kwa sababu mbalimbali pasipo hata kushiriki ngono na mwanaume.

TURUDI KATIKA BANDIKO LAKO HAPO.

Ndiyo, kisayansi inawezekana kabisaaaaaa mwanamke bikra kupata Ujauzito na kujifungua.

Mimba inatungwa kwa namna nyingi.

Na wala siyo lazma eti uume uingie kwenye uke na kumwaga manii za kurutubisha yai la uzazi la mwanamke na kutunga mimba (fertilization).

Mimba inaweza kutungwa kwa mwanamke bikra kupitia njia mbalimbali mfano:-

• Artificial insemination.
• In Vitro Fertilization (IVF)

Na mwanamke Bikra aliyepata mimba, bado atahesabika kuwa ni Bikra vile vile ikiwa tu kama hakuingiliwa ukeni kwake na uume wa mwanaume.

Rejea tena maana ya VIRGINITY na HYMEN..., kisha jifunze IN VITRO FERTILIZATION (IVF) ni nini? na pia jifunze ARTIFICIAL INSEMINATION ni nini?

Kisha kaa kwa kutulia TAFAKARI halafu nina uhakika utanielewa! Na utakubali kile nilichokiandika hapa.
Kweli, maelezo yangu yalikuwa hayajajitosheleza. But nililenga kumaanisha virgin birth base on miraculous act of the holy spirit.
 
Nimesoma bandiko lako Venus Star, pia nimepitia maoni ya wachangiaji wengine. Lakini nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusiana na mjadala pia kutokana na hiki ulichokieleza hapa.

Umesema kuwa msingi mkubwa wa sayansi ni kujibu swali la HOW. Napo kwa upande wa dini, msingi wake mkubwa ni kujibu swali la WHY. Nafikiri nimenukuu kwa usahihi!

Kwanza kabisa, nakubaliana na hoja kuwa sayansi inatoa majibu na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya HOW. Lakini, sayansi pia inatoa na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya WHY.

Ningependa nianze kwa ufafanuzi mfupi kuhusiana na WHY kabla ya kuizungumzia sayansi, mahala ambapo ndipo nitajikita zaidi.

WHY kama swali laweza kutumika katika namna ama mazingira ya aina mbili:

1) Swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu hasa chanzo kilichopo na kinacho pelekea ama kinacho sababisha kufanyika ama kuzalishwa kwa kitu au jambo fulani. Kwa lugha nyingine CAUSE ama REASON.

Mfano: Why do earthquakes occur? Kwanini tetemeko la ardhi hutokea?

2) Pili; swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo fulani. Kwa lugha nyingine PURPOSE ama INTENTION.

Mfano: Why should you go to school? Kwanini uende shule?

Katika hizo namna mbili za maswali ya WHY, sayansi inaweza kutoa majibu kwa maswali ya namna ya kwanza. Sayansi haitoi na wala si jukumu lake kutoa majibu ya namna ya pili ya maswali ya WHY, maswali ambayo yanauliza nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo.

Maswali ya WHY ya namna ya pili yanahusisha ufahamu ama utashi unaopelekea kuwepo kwa hiyo nia ama kusudi la kufanyika kwa hilo jambo fulani. Ndio maswali yanayowafanya watu wengi kudhani kuwa sayansi haitoi ama haiwezi kutoa majibu ya maswali ya WHY. Si sahihi!

Sayansi ni elimu inayoongozwa na kitu kinachoita curiosity, yaani udadisi. Na katika udadisi, mara nyingi hutawaliwa na maswali ambayo mtu hujiuliza kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimaisha na ya kiasili. Huu ndio mwanzo ama msingi katika sayansi.

Maswali kama:

1) Kwanini kitu fulani hutokea?

2) Kwanini kitu fulani kiko kwa namna fulani?

3) Kwanini kitu fulani ni tofauti na kingine kwa namna fulani? Na kadhalika.

Maswali kama haya huwa ndio msingi katika kutambua ama kusaka majibu ya masuala mbalimbali yenye utata katika sayansi. Maswali haya ni moja ya hatua za awali katika utaratibu wa kisayansi (scientific process).

Katika utafiti wa kisayansi, mwanasayansi hufanya observation kama hatua ya mwanzo juu ya masuala yenye utata yanayohitaji majibu ya kisayansi. Hapa kwenye observation ndipo huambatana na maswali kadha wa kadha kama ambavyo nimekwisha kutoa mifano mitatu iliyopita.

Mwanafizikia Isaac Newton aliyeishi katika karne ya 17 aliwahi kujiuliza swali moja baada ya kulitazama tofaa likianguka ardhini: kwanini tofaa lilianguka moja kwa moja ardhini na halikuelekea mbali na ardhi ama juu zaidi?

Hapa Newton alikuwa akijiuliza swali la namna ile ya kwanza niliyoieleza pale mwanzoni. Alijiuliza kuhusu chanzo kinacho sababisha tofaa kuanguka ardhini. Hakujiuliza kuhusu nia ama kusudi la tofaa kuanguka ardhini, swali ambalo lingehitaji utashi wa tofaa ili kulipatia majibu.

Hii ilikuwa ni observation ya Newton. Ni hatua ya awali kabisa iliyomo katika utaratibu wa utafiti wa kisayansi. Hatua zingine zinazofuata kama vile uundaji wa nadharia na majaribio yake, haviwezi kufanyika kabla ya hatua hii ya awali.

Hapo awali nilisema kuwa sayansi inatoa majibu ya maswali kadha wa kadha ya namna ya kwanza ya maswali ya WHY. Nilitoa mfano wa swali katika kipengele cha kwanza cha maswali ya WHY. Nilisema: Why do earthquakes occur?

Sayansi inalijibu swali hili kama ifuatavyo:
Earthquakes occur because of sudden release of stress along faults in the earth's crust.

Stress inayozungumziwa hapa ni ya kifizikia: "force per unit area."

Swali jingine maarufu sana:
Kwanini vitu huanguka ardhini na si kuelekea mbali na ardhi ama kuelekea juu?

Jibu la kisayansi: ni kwa sababu ya Gravitation. Fullstop! Hapa sayansi inajibu WHY na si HOW.

Swali jingine ambalo tunaweza kujiuliza hivi leo:
Kwanini gari likiwa katika mwendo kasi kisha likasimama ghafla, waliomo ndani husukumwa kuelekea mbele?

Kisayansi: ni kwa sababu ya Inertia. Period!

Hayo ni baadhi tu ya maswali ya WHY ambayo sayansi inayajibu.

La mwisho na la muhimu pia, sayansi ni pana sana na imegawanyika katika matawi ama branches mbalimbali. Ukiachana na fizikia ama sayansi asilia kwa ujumla ukaingia kwenye branches nyinginezo kama vile social sciences, pia utakutana na maswali mengi tu ya namna hiyo yenye kujibiwa kisayansi. Kuna psychology, sociology n.k., zote hizo ni sayansi.

Asante!
 
Mbona umechagua theory moja tu.
Nimeongelea Atomic Structure.

Halafu sijasema kuwa why question linaulizwa na wanasayansi bali nimesema how question.

Nikakuambia methodologies zote za kisayansi ni kujibu swali la how.

Ziwe imani mbovu, maandiko mabovu ya kidini lakini lengo lake ni kujibu why!?
Katika kujibu hivyo haijitaji practical kuthibitisha.

Hata hivyo theories zote za kisayansi zinakuwepo kwa wati fulani kutokana na uelewa wa wakati ule.

Sasa hivi theories kubwa zilizipo ni:-
1. Quantum Mechanics theory. Which deals with small particles

2. General relativity Theory.

Zipo hivyo kwa sasa kwa sababu hakuna tens ugunduzi mpya utakao uondoa huu wa sasa.
Mkuu unatoa wapi hivi vitu, hakuna kufuru katika sayansi.

If you can come up with a better theory on the atomic structure tutaikubali. Kwanza discredit kilichopo then come up with something better.
 
Nimesoma bandiko lako Venus Star, pia nimepitia maoni ya wachangiaji wengine. Lakini nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusiana na mjadala pia kutokana na hiki ulichokieleza hapa.

Umesema kuwa msingi mkubwa wa sayansi ni kujibu swali la HOW. Napo kwa upande wa dini, msingi wake mkubwa ni kujibu swali la WHY. Nafikiri nimenukuu kwa usahihi!

Kwanza kabisa, nakubaliana na hoja kuwa sayansi inatoa majibu na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya HOW. Lakini, sayansi pia inatoa na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya WHY.

Ningependa nianze kwa ufafanuzi mfupi kuhusiana na WHY kabla ya kuizungumzia sayansi, mahala ambapo ndipo nitajikita zaidi.

WHY kama swali laweza kutumika katika namna ama mazingira ya aina mbili:

1) Swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu hasa chanzo kilichopo na kinacho pelekea ama kinacho sababisha kufanyika ama kuzalishwa kwa kitu au jambo fulani. Kwa lugha nyingine CAUSE ama REASON.

Mfano: Why do earthquakes occur? Kwanini tetemeko la ardhi hutokea?

2) Pili; swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo fulani. Kwa lugha nyingine PURPOSE ama INTENTION.

Mfano: Why should you go to school? Kwanini uende shule?

Katika hizo namna mbili za maswali ya WHY, sayansi inaweza kutoa majibu kwa maswali ya namna ya kwanza. Sayansi haitoi na wala si jukumu lake kutoa majibu ya namna ya pili ya maswali ya WHY, maswali ambayo yanauliza nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo.

Maswali ya WHY ya namna ya pili yanahusisha ufahamu ama utashi unaopelekea kuwepo kwa hiyo nia ama kusudi la kufanyika kwa hilo jambo fulani. Ndio maswali yanayowafanya watu wengi kudhani kuwa sayansi haitoi ama haiwezi kutoa majibu ya maswali ya WHY. Si sahihi!

Sayansi ni elimu inayoongozwa na kitu kinachoita curiosity, yaani udadisi. Na katika udadisi, mara nyingi hutawaliwa na maswali ambayo mtu hujiuliza kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimaisha na ya kiasili. Huu ndio mwanzo ama msingi katika sayansi.

Maswali kama:

1) Kwanini kitu fulani hutokea?

2) Kwanini kitu fulani kiko kwa namna fulani?

3) Kwanini kitu fulani ni tofauti na kingine kwa namna fulani? Na kadhalika.

Maswali kama haya huwa ndio msingi katika kutambua ama kusaka majibu ya masuala mbalimbali yenye utata katika sayansi. Maswali haya ni moja ya hatua za awali katika utaratibu wa kisayansi (scientific process).

Katika utafiti wa kisayansi, mwanasayansi hufanya observation kama hatua ya mwanzo juu ya masuala yenye utata yanayohitaji majibu ya kisayansi. Hapa kwenye observation ndipo huambatana na maswali kadha wa kadha kama ambavyo nimekwisha kutoa mifano mitatu iliyopita.

Mwanafizikia Isaac Newton aliyeishi katika karne ya 17 aliwahi kujiuliza swali moja baada ya kulitazama tofaa likianguka ardhini: kwanini tofaa lilianguka moja kwa moja ardhini na halikuelekea mbali na ardhi ama juu zaidi?

Hapa Newton alikuwa akijiuliza swali la namna ile ya kwanza niliyoieleza pale mwanzoni. Alijiuliza kuhusu chanzo kinacho sababisha tofaa kuanguka ardhini. Hakujiuliza kuhusu nia ama kusudi la tofaa kuanguka ardhini, swali ambalo lingehitaji utashi wa tofaa ili kulipatia majibu.

Hii ilikuwa ni observation ya Newton. Ni hatua ya awali kabisa iliyomo katika utaratibu wa utafiti wa kisayansi. Hatua zingine zinazofuata kama vile uundaji wa nadharia na majaribio yake, haviwezi kufanyika kabla ya hatua hii ya awali.

Hapo awali nilisema kuwa sayansi inatoa majibu ya maswali kadha wa kadha ya namna ya kwanza ya maswali ya WHY. Nilitoa mfano wa swali katika kipengele cha kwanza cha maswali ya WHY. Nilisema: Why do earthquakes occur?

Sayansi inalijibu swali hili kama ifuatavyo:
Earthquakes occur because of sudden release of stress along faults in the earth's crust.

Stress inayozungumziwa hapa ni ya kifizikia: "force per unit area."

Swali jingine maarufu sana:
Kwanini vitu huanguka ardhini na si kuelekea mbali na ardhi ama kuelekea juu?

Jibu la kisayansi: ni kwa sababu ya Gravitation. Fullstop! Hapa sayansi inajibu WHY na si HOW.

Swali jingine ambalo tunaweza kujiuliza hivi leo:
Kwanini gari likiwa katika mwendo kasi kisha likasimama ghafla, waliomo ndani husukumwa kuelekea mbele?

Kisayansi: ni kwa sababu ya Inertia. Period!

Hayo ni baadhi tu ya maswali ya WHY ambayo sayansi inayajibu.

La mwisho na la muhimu pia, sayansi ni pana sana na imegawanyika katika matawi ama branches mbalimbali. Ukiachana na fizikia ama sayansi asilia kwa ujumla ukaingia kwenye branches nyinginezo kama vile social sciences, pia utakutana na maswali mengi tu ya namna hiyo yenye kujibiwa kisayansi. Kuna psychology, sociology n.k., zote hizo ni sayansi.

Asante!
Mkuu hapo umemaliza... mtoa uzi anapambana kudefend imani yake.
 
Back
Top Bottom