Nimesoma bandiko lako
Venus Star, pia nimepitia maoni ya wachangiaji wengine. Lakini nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusiana na mjadala pia kutokana na hiki ulichokieleza hapa.
Umesema kuwa msingi mkubwa wa sayansi ni kujibu swali la HOW. Napo kwa upande wa dini, msingi wake mkubwa ni kujibu swali la WHY. Nafikiri nimenukuu kwa usahihi!
Kwanza kabisa, nakubaliana na hoja kuwa sayansi inatoa majibu na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya HOW. Lakini, sayansi pia inatoa na ina wajibu wa kutoa majibu ya maswali ya WHY.
Ningependa nianze kwa ufafanuzi mfupi kuhusiana na WHY kabla ya kuizungumzia sayansi, mahala ambapo ndipo nitajikita zaidi.
WHY kama swali laweza kutumika katika namna ama mazingira ya aina mbili:
1) Swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu hasa chanzo kilichopo na kinacho pelekea ama kinacho sababisha kufanyika ama kuzalishwa kwa kitu au jambo fulani. Kwa lugha nyingine
CAUSE ama
REASON.
Mfano: Why do earthquakes occur? Kwanini tetemeko la ardhi hutokea?
2) Pili; swali WHY laweza kutumika ili kupata kufahamu nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo fulani. Kwa lugha nyingine
PURPOSE ama
INTENTION.
Mfano: Why should you go to school? Kwanini uende shule?
Katika hizo namna mbili za maswali ya WHY, sayansi inaweza kutoa majibu kwa maswali ya namna ya kwanza. Sayansi haitoi na wala si jukumu lake kutoa majibu ya namna ya pili ya maswali ya WHY, maswali ambayo yanauliza nia ama kusudi la kufanywa ama kufanyika kwa jambo.
Maswali ya WHY ya namna ya pili yanahusisha ufahamu ama utashi unaopelekea kuwepo kwa hiyo nia ama kusudi la kufanyika kwa hilo jambo fulani. Ndio maswali yanayowafanya watu wengi kudhani kuwa sayansi haitoi ama haiwezi kutoa majibu ya maswali ya WHY. Si sahihi!
Sayansi ni elimu inayoongozwa na kitu kinachoita curiosity, yaani udadisi. Na katika udadisi, mara nyingi hutawaliwa na maswali ambayo mtu hujiuliza kuhusiana na masuala mbalimbali ya kimaisha na ya kiasili. Huu ndio mwanzo ama msingi katika sayansi.
Maswali kama:
1) Kwanini kitu fulani hutokea?
2) Kwanini kitu fulani kiko kwa namna fulani?
3) Kwanini kitu fulani ni tofauti na kingine kwa namna fulani? Na kadhalika.
Maswali kama haya huwa ndio msingi katika kutambua ama kusaka majibu ya masuala mbalimbali yenye utata katika sayansi. Maswali haya ni moja ya hatua za awali katika utaratibu wa kisayansi (scientific process).
Katika utafiti wa kisayansi, mwanasayansi hufanya observation kama hatua ya mwanzo juu ya masuala yenye utata yanayohitaji majibu ya kisayansi. Hapa kwenye observation ndipo huambatana na maswali kadha wa kadha kama ambavyo nimekwisha kutoa mifano mitatu iliyopita.
Mwanafizikia Isaac Newton aliyeishi katika karne ya 17 aliwahi kujiuliza swali moja baada ya kulitazama tofaa likianguka ardhini: kwanini tofaa lilianguka moja kwa moja ardhini na halikuelekea mbali na ardhi ama juu zaidi?
Hapa Newton alikuwa akijiuliza swali la namna ile ya kwanza niliyoieleza pale mwanzoni. Alijiuliza kuhusu chanzo kinacho sababisha tofaa kuanguka ardhini. Hakujiuliza kuhusu nia ama kusudi la tofaa kuanguka ardhini, swali ambalo lingehitaji utashi wa tofaa ili kulipatia majibu.
Hii ilikuwa ni observation ya Newton. Ni hatua ya awali kabisa iliyomo katika utaratibu wa utafiti wa kisayansi. Hatua zingine zinazofuata kama vile uundaji wa nadharia na majaribio yake, haviwezi kufanyika kabla ya hatua hii ya awali.
Hapo awali nilisema kuwa sayansi inatoa majibu ya maswali kadha wa kadha ya namna ya kwanza ya maswali ya WHY. Nilitoa mfano wa swali katika kipengele cha kwanza cha maswali ya WHY. Nilisema: Why do earthquakes occur?
Sayansi inalijibu swali hili kama ifuatavyo:
Earthquakes occur because of sudden release of stress along faults in the earth's crust.
Stress inayozungumziwa hapa ni ya kifizikia: "force per unit area."
Swali jingine maarufu sana:
Kwanini vitu huanguka ardhini na si kuelekea mbali na ardhi ama kuelekea juu?
Jibu la kisayansi: ni kwa sababu ya Gravitation. Fullstop! Hapa sayansi inajibu WHY na si HOW.
Swali jingine ambalo tunaweza kujiuliza hivi leo:
Kwanini gari likiwa katika mwendo kasi kisha likasimama ghafla, waliomo ndani husukumwa kuelekea mbele?
Kisayansi: ni kwa sababu ya Inertia. Period!
Hayo ni baadhi tu ya maswali ya WHY ambayo sayansi inayajibu.
La mwisho na la muhimu pia, sayansi ni pana sana na imegawanyika katika matawi ama branches mbalimbali. Ukiachana na fizikia ama sayansi asilia kwa ujumla ukaingia kwenye branches nyinginezo kama vile social sciences, pia utakutana na maswali mengi tu ya namna hiyo yenye kujibiwa kisayansi. Kuna psychology, sociology n.k., zote hizo ni sayansi.
Asante!