Eiyer mimi na wewe tulikuwa tunaongelea maovu ya mungu wa Waisraeli, mbona umekuja huku? Anyways.....
Na mimi nakujibu your first Q kwa swali,u as a Christian, unajuaje Allah doesn't exist?
Najua Allah ni nini!
Contradictions:-
Yohana 3:13-hakuna aliyepanda kuingia mbinguni ila yule aliyeshuka kutoka mbunguni, mwana wa binadamu
2 Wafalme 2:11-na Eliya akaanza kupanda katika ile dhoruba ya upepo kuelekea mbimguni
Sio wewe tu walioshindwa kuielewa biblia hata wanaojiita wasomi nao wanatoka kapa kila uchao,huwa nasha ngaa kuwa wanasema hiki ni kitabu kilichoandikwa kwa makosa na watu wa kawaida sana,hivi msomi anashindwaje kuelewa maandishi ya asie msomi?
Nirudi kwenye swali lako:
Unaposoma biblia unahitaji uwe makini sana kama unataka uielewe
Hapo yesu alikuwa anazungumza na watu ambao hawajafika mbinguni na mara nyingi wamekuwa wakimbishia kuhusu yale aliyokuwa anawaambia hivyo hakukosea kuwaambia hakuna aliepanda mbinguni kwani kati yao hakuna aliyepanda kwenda huko isipokuwa Yesu mwenyewe
Hapo hakumaanisha kuwa tangu dunia iumbwe hakuna aliyeenda mbinguni[rejea kauli yake alipokuwa anawaambia kuwa hakuna aliyeisikia sauti ya Mungu wakati Musa alizungumza na Mungu]
Yakobo 1:13-mtu akiwa chini ya jaribu asiseme mungu ananijaribu..kwamaana mungu hawezi kujaribiwa wala yeye mwenyewe hamjaribu yeyote
Mwanzo 22:1-baada ya mambo hayo,mungu wa kweli akamjaribu Abraham.....
Hapa ni kwamba ni kweli Mungu hamjaribu yoyote bali kila mmoja hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe,lakini unatakiwa ujue kuwa kuna mambo Mungu anaweza kuyafanya kwa sababu maalum na mahali maalum
Mungu kumjaribu Ibrahimu kulikuwa kuna sababu maalum,pia kuna mambo Mungu aliyakataza na akaja kuyaruhusu baadhi na mengine aliyaruhusu nyakati maalum na kwa watu maalum tu[rejea Amri ya Mungu kukataza kujifanyia sanam na alipomruhusu Musa kutengeneza nyoka wa shaba]
Kutoka 20:4-usijifanyie sanamu ya kuchongwa wala umbo lililo kama kitu chochote kilicho juu mbinguni wala........
Kutoka 25:18-20-nawe utafanya makerubi wawili wa dhahabu...........
Rejea jibu langu la swali lako la pili!
2 Samweli24:1- Again the anger of the LORD burned against Israel, and he incited David against them, saying, "Go and take a census of Israel and Judah
1 Nyakati 21:1- na shetani akasimama kushindana na Iarael, akachochea Daudi ahesabu Israeli.
*nimeandika kwa English kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu
1Wafalme 15:33-katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme juu ya Israeli yote kule Tirsa kwa miaka 24
(kwahiyo Baasha alikufa mwaka wa 27 wa utawala wa Asa)
2Nyakati 16:1- katika mwaka wa 36 wa utawala ws Asa, Baasha mfalme wa Israeli alikuja kupigana ma Yuda............
Kwenye haya maswali yako kuna utata
Naomba unithibitishie kuwa haya matukio yalitokea wakati mmoja na yalihusu mtu yuleyule
Majina ya Wayahudi yalikuwa yanafanana na kujirudiarudia hivyo unaweza kujichanganya ukidhani biblia imejichanganya[rejea Yuda iskariote na Yuda mwaadilifu wote hawa walikuwa wanafunzi wa Yesu,Yohana mbatizaji na Yohana mwanafunzi wa Yesu,Sauli mfalme na Sauli aliekuja kuitwa Paulo n.k] unapotoa maandiko kufuatia majina inahitajika utoe maelezo ya kutosha kuthibitisha kuwa yanazungumzia mtu mmoja lakini matukio yanakinzana!
Zaburi 58:10- Mwadilifu atashangilia kwasababu ameona kisasi. Ataosha miguu yake katika damu ya waouvu
Methali 24:17- adui yako anapoanguka usishangilie, naye anapokwazwa, moyo wako usiwe na shangwe.
bubbs biblia inaeleweka kama utataka kuielewa
Hapo kuna matukio mawili tofauti
Zaburi inazungumzia hukumu,kama ingekuwa leo tungesema ni hukumu ya kimahakama,hakuna anaechukia mtuhumiwa wake aliemtendea uovu akihukumiwa kwa haki
Mithali inazungumzia kitu kingine na nadhani unajua ni kwanini inaitwa mithali
Hapo inazungumzia baina ya mtu na mtu na sio mtuhumiwa na mahakama!
1 Nyakati 21:11,12-basi Gadi akaja akaingia kwa Daudi, akamwambia: "Yehoca amesema hivi, 'jichagulie moja,; kama kuwe na njaa kwa miaka mitatu, au miezi mitatu wapinzani wako wakufagilie mbali, na upanga wa adui zako ukufikie........
2Samweli 24:13- basi Gadi akaingia kwa Daudi akamwambia: "je njaa ikujie katika nchi yako kwa miaka saba, au miezi mitatu ya wewe kukimbia mbele ya adui zako......
Rejea jibu langu la swali lako la pili!
Mathayo 27:5- basi akatupa vile vipande vya fedha hekaluni akaondoka, akaenda zake kijinyonga
Matendo 1:18-kwa hiyo mtu huyo alinunua shamba kwa mshahara wa ukosefu wa uadilifu, akaanguka kichwa kwanza, akapasuka kwa kelele katikati ya matumbo yake yote yakamwagika nje.
:wave:
Unapoona neno kujinyonga unaelewa nini?