Report ya Makonda ya kutembelea mikoa 20 ikimfikia Rais tutarajie yafuatayo kutolea!

Ni reshafle au watapangiwa kazi zingine? Sasa mbona itakuwa kazi kubwa kupangua na kupanga si ya siku moja.
 
Hapo ndo ujue system yote imeoza!
 
Sidhani Samia anao huo ubavu. She needs to resign herself
 
Watoke tu na sie tukaonyeshe uwezo wetu, kwa kuwatumikia Watanzania wenzetu!
 
Tatizo kubwa ni huyo Rais. Vyote vinaanzia hapo. Ukimuweka mchapakazi, mzalendo, mwenye uchungu, serious person matatizo mengi kama umeme, maji, ardhi, mfumuko wa bei yote yatapata ufumbuzi. SSH anteua wahuni na kutengua wachapakazi.
Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwaondoa Lukuvi upande wa ardhi na Kalemani upande wa nishati!
Bi.Mkubwa amechoka,apumzike!
 
Katika ziara ya Mwenezi tunatakiwa kujifunza kwamba Kuna wahamiaji haramu au Kuna watu wanawasingizia wananchi kwamba siyo raia wa Tanzania endapo unakwenda kinyume na matakwa Yao.

Vyovyote itakavyo kuwa hakuna ubishi kwamba Kuna raia wa nchi zinazotuzunguka wamehamia nchini na kujenga uhalali kiasi ambacho hata MAHAKAMA haziwezi kuamua.

Wahamiaji haramu wamejimilikishia Ardhi kinyume na utaratibu Na hakuna wa kuwagusa.

Nchi Ile tuliyoishi kipindi Kile tulichoshuhudia kila Aina ya uozo kimetudi Kwa kazi.
 
Kwaiyo Makonda hajui majukumu ya RC,DC na DED ilihali alikuwa DC na baadaye RC!
Acha uongo Mkuu!
 
Hivi kulikuwa na sababu gani ya kuwaondoa Lukuvi upande wa ardhi na Kalemani upande wa nishati!
Bi.Mkubwa amechoka,apumzike!
Upuuzi flani hivi, tatizo la umeme, ardhi lilihibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Haki, rushwa mimi ni nani vilipungua unapewa majungu, unayabeba. Wewe ni Rais haungalii takwimu, uhalisia unatumbua na kuteua watu kwa majungu. Nchi ipo kwenye giza unaenda holiday. Tatizo lolote likitokea unaenda kula bata. rushwa imerudi.

Rais ni nani? Kazi yake kwa wananchi wake ni nini, ipi?
 
Itakuwa uwendawazimu kudhani kwamba hata waziri wa nishati au katibu wizara ya nishati unahitajika ushahidi kutoka kwa Kada wa chama ili watenguliwe.

Nchi nzima ni kama ipo gizani hakuna tofauti na watu walioishi hapa 18 century.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…