Kwa nchi yetu chama ndio kinatawala, leo hii wanaCCM wakiamua kusiwe na ukomo wa urais WANAWEZA.
Hakuna mtu anakataa hilo. Na wanaweza kufanya hivyo kwa sababu ya wingi wao Bungeni na sio kwa sababu Rais ni CCM.
Leo CCM ikiamua tuwe na rais wa milele itakuwa hivyo tena kwa utaratibu wa kisheria kabisa.
Kwamba wafute uchaguzi ili turudi tena kwenye siasa ya chama kimoja? Kinadharia wanaweza lakini in reality hawatathubutu maana itakuwa ni kutangaza wazi kuwa hamna demokrasia nchini. Hata nchi zenye mfumo wa kibabe wana vyama vya upinzani.
Sasa kama baadhi ya wana CHADEMA na mwenyekiti wao hawaamini katika ukomo wa uongozi, ni nini kitawashinda wakipewa nchi wasirekebishe sheria na tukawa na rais wa muda wote?
Hawataweza kwa sababu hamna jinsi wataweza kushinda urais na robo tatu za wabunge. Wakifika hapo tutawapinga kama tunavyo wapinga CCM.
Huwa nawashangaa sana watu wanaosema tutofautishe vyama vya siasa na nchi katika mambo ya uongozi.
Kwa sababu hauwaelewi. Kuongoza nchi kama chama cha siasa ndio kumetufikisha tulipo sasa.
Hivi ni wazito kiasi kwamba hamuelewi vyama vya siasa ndio vinaamua nchi iongozwe vipi?
Vyama vya siasa havina ubavu huo ndio maana kila baada ya muda inabidi vitafute kuhalalishwa na wenye nchi. Ukiona chama cha siasa kina uwezo basi ujue kuna tatizo katika Katiba yao.
Tofauti kubwa ni kuwa uongozi wa chama cha siasa unawajibika kwa wanachama wake tu, sio kwa nchi nzima. Ndio maana upigaji kura unaendana na uanachama sio uraia. Kwa sababu hiyo pool ya uongozi katika chama cha siasa inategemea wangapi wanaunga mkono sera zake. Kama ni chama cha upinzani, lengo lake kubwa ni kuchukua dola. Kwa sababu hiyo watu wanaoweza kukiongoza ni wale ambao wataweza kufanikisha lengo hilo. Na kwa vile hawa sio wengi kujiwekea mipaka kuhusu nani ataweza kuwaongoza ni kujifunga mikono. Ukomo unatakiwa uwekwe na wanachama. Wakiona mgombea hatawafaa wana haki ya kumtoa bila kujali kahudumu kwa miaka mingapi. Vile vile mwanachama yeyote anaejiona ana wito wa kugombea uchaguzi anatakiwa aruhusiwe kufanya hivyo ili mradi maslahi maana yameangaliwa.
Mimi simkubali Lissu lakini naamini kuwa ana haki ( hata wajibu) kufanya hivyo kama anaona chama chake kinaelekea kusiko. Ninachopinga ni kufanya juhudi za wazi za kumnyima Mbowe haki yake ya kugombea. Aidha, kutumia lugha za ulaghai na kebehi ( kwa mafumbo na kujificha) kufanikisha azma yake.
Pamoja na maneno mazuri ya Heche, hawana uwezo wa kutibu majeraha ambayo wamekisababishia chama chao. Kwa mfano lugha ya kusema kuwa watawashughulikia wale wachache ambao kwa mtazamo wao wamekifikisha chama kilipo ni ishara kuwa uongozi wao utakuwa wa visasi. Wakianza kwa kuwashughulikia Wenje, Ntobi na Yericko tutajua ni kwa sababu wamediriki kutofautiana nao. Hiyo haitaziba nyufa bali utaziongeza.
Mimi siishiwi hoja, Mkuu.
Amandla...