Zama hizi za sasa si za kuwa na chama kimoja kinaongoza peke yake..yaani kuanzia ma-veo, weo, ma-dc, Ma-rc, mawaziri nk siasa za sasa lazima ziwe jumuishi na shirikishi..kila kura iwe na nguvu ya matokeo, vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi na kupata idadi fulani ya kura lazima viwe na nafasi kwenye uongozi..mambo ya the winner takes all hayajatufikisha popote zaidi ya chama kukumbatia wizi, upendeleo, matumizi mabaya ya madaraka, ufisadi na ubaguzi wa kiitikadi..na hivyo si tu chadema, chama chochote kikipata ridhaa ya kuongoza peke yao hawawezi kubadilisha misingi ya uongozi wa nchi km wanavyotaka..ndio maana lazima yawepo mabadiliko ya katiba sasa!