TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Sijakurupuka.

Wewe jibu swali.
Umekurupuka..maana hujafuatilia mazungumzo yangu na yule member niliyemuuliza swali.
Swali nililomuuliza 'Kwa hiyo kufeli chuo ndio kutokuwa na akili?'. Hivi unashindwaje kuelewa mantiki ya hili swali?
 
Yes Tanzania most of students wanasoma vitu kwa sababu
Hayo yapo Tanzania tu?

Marekani wazazi hawakai chini na watoto kujadili career choices, kwamba e bana eeh, unataka kusoma Art History and Theatric Dancing kaa ukijua unaweza ku lost. Duniani huko hakuna hiyo ?

Halafu sio kila anae pursue passion yake anakuja kufurahia. Wapo walio pursue passion baadae wanajuta kwa kuona haina manufaa. Your blanket singling out of Tanzania is misguided.

Halafu kama system ni mbovu hawa ndio ma genius wa hiyo Tanzania, waingie humo kwenye system wakarekenishe mambo basi, badala kuishia kufundisha ma tuition ya miembeni na kuridhika na vi Alteza vya hapa na pale. Wanataka nani awawarekebishie mambo ????
 
Ndoto nyingi za maskini haziko huru kaka,me nilipenda sana kuwa RUBANI nilifanya kila niliwezalo ili nifikie huko,nilivyofika A-level maajabu ndo yakaanziaga hapo.
Inasikitisha. Maana lisaa limoja tu ni dola nyingi mno. Imagine una masaa mangapi hadi uwe rubani ?Nchi zingine ungepata ufadhili kutoka serikalini ili utimize ndoto zako.
 
Mimi mwaka 2000 nlipata A katika masomo yote matatu ya PCM. kifupi ni kuwa O- Level nilikuwa na B moja tu ya Kiswahili. A- level nikasimamisha misonge masomo yote.

Nilipokuwa Chuo UDSM. nliishi maisha ya manyanyaso sana toka kwa lectures pale Udsm. Nlinyanyasika sana. Mitihani yangu ikawa inasahishwa kwa umakini mkubwa kunitafutia makosa.

Semister ya kwanza nlikuwa na GPA ya 4.9 na pili 4.9

Mwaka wa pili semister ya kwanza 4.9 ya pili 4.8 walimu wakaanza kuwa na nongwa hasa kwa kuwa nlikuwa naonekana sometimes kuwarekebisha wanapokuwa wanafundisha. Nlikuwa mara nyingi napendekeza njia rahisi za ku solve maswali.

Nlidisco ktk mazingira ya kushangaza sana. Kesi yangu ilienda mbele za watu ambao baadaye wengine walikuja omba msamaha. Namkumbuka Prof mmoja ambaye alikuja gombea urais miaka ya nyuma huyu ndo alikuwa akinipambania na kunitia moyo. Huyu aliniwezesha kurudi tena chuo after 4 years. Nlianza na GPA ya 4.7 nikawa napanda.mpaka nimemaliza Chuo nlikuwa na GPA ya 4.8 nenda kawaulize Coet watakupa habari zangu.

Ndo kisa cha wadau kuniita Chizi Maarifa. Mimi nlikuwa napiga vipindi wanachuo wa masters wanakuja kwangu Hall 4 niwape shule.

Nitawasimulia mambo makubwa kwenye uzi wangu. Ila kuna details ntaficha sababu za
pole sana , mimi nakuelewa kwa sababu ilishawai kunikuta but sipo interested kuandika hapa.
labla siku nikiwa tayari nitashusha kamkasa kidogo, hilo linafanya nimuite kiyombo his genius
 
Kufeli kwake hapa naona kumesababishwa na mazingira zaidi. Alikuwa hasomi,muda mwingi anatumia kufundisha tuition,angefaulu vipi ?
Huko kuomba Engneering mara mbili itakuwa wazazi au jamii iliyomzunguka ndo ilimforce,influence akasome Engneering ila yeye moyoni mwake passion yake ilikuwa kufundisha kuandika vitabu.

You don't know that!

Unajuaje alilazimishwa kusoma Engineering na wazazi na jamii?

Alikuwa na passion ya kuandika vitabu ? Kitabu gani kaandika ???

ISBN namba ya vitabu vyake ni ngapi?

Muhammed Said kaandika vitabu vyake vinasema uhuru wetu uliletwa na wajomba zake wa Kariakoo waliobaguliwa, wild and wooly, lakini vina ISBN! Vya marehemu mwamba Elias Kihombo namba zake ngapi ????
 
How is it difficult to follow your passion in Tanzania?

Amesoma PCM, the one and only combination from which you can advance and study anything in college as long as you passed the missing subject in O Level, this according to UDSM admission prospectus.

Ame apply Engeneering mara mbili, kapata, Sasa Tanzania imemnyima nini?

Hapendi vipi Engeneering wakati ame apply mwenyewe mara mbili ????

Eti ana passion ya kufundisha lakini hakutaka kusoma ili awe mwalimu. He academic choices were a mess.

Mwamba wa Physics, tena mwenye passion ya Modern Physics, anafeli vipi Electronic / IT / Communication Engineering? Halafu tunataka kuilaumu Tanzania. Mbona nerds wengine hawafeli chuo?

The guy was unfocused and reckless.
hebu tuanzie hapa, umeshasoma chuo ukajua changamoto za malecture?
unaweza disco tu kwa kutoingia class, lect. anaweza atoe assigment mda usio rasmi kisa ana kisilani na mtu fulani, anaweza weka vikwazo vikwazo hasa wale wanafunzi ambao ni best,
kuna mshikaji aliacha chuo Muhimbili mwaka wa nne siyo kisa alikuwa vibaya bali aliandamwa sana . hadi chuo akakiona kigumu , yupo mwingine tena hapo hapo mwimbili mwaka wa mwisho Nafikiri alikuwa Radiology aliamua kuacha siyo naye alifeli but ni visa vya chuo.
mwaka 2014 , jamaa alikuwa anapiga pindi , wakati anapiga pindi alituelezea kidogo ,alisema vilikuwa ni visa kisa yeye alikuwa hayupo darasani muda mwingi, ndo kilicho mfanya a discont...
 
Leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili.

Tunahitaji kuwa Karibu na Mungu wakati wote kwani safari yetu ipo mikononi mwake.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never forget you My brother.

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were. Rest in peace up in heaven.


-----
Pia soma




ALAMA ALIZOACHA ELIAS KIHOMBO


Imepita miaka takribani miaka 14 sasa, tangia Tanzania ilipopata kumshuhudia mwanafunzi alieshindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were.

Rest in peace up in the heaven

View attachment 1630262
View attachment 1630283
so sorry bro, i wish to hear from other T.O akina William Maro wa Mzumbe, na wengine
 
Mimi mwaka 2000 nlipata A katika masomo yote matatu ya PCM. kifupi ni kuwa O- Level nilikuwa na B moja tu ya Kiswahili. A- level nikasimamisha misonge masomo yote.

Nilipokuwa Chuo UDSM. nliishi maisha ya manyanyaso sana toka kwa lectures pale Udsm. Nlinyanyasika sana. Mitihani yangu ikawa inasahishwa kwa umakini mkubwa kunitafutia makosa.

Semister ya kwanza nlikuwa na GPA ya 4.9 na pili 4.9

Mwaka wa pili semister ya kwanza 4.9 ya pili 4.8 walimu wakaanza kuwa na nongwa hasa kwa kuwa nlikuwa naonekana sometimes kuwarekebisha wanapokuwa wanafundisha. Nlikuwa mara nyingi napendekeza njia rahisi za ku solve maswali.

Nlidisco ktk mazingira ya kushangaza sana. Kesi yangu ilienda mbele za watu ambao baadaye wengine walikuja omba msamaha. Namkumbuka Prof mmoja ambaye alikuja gombea urais miaka ya nyuma huyu ndo alikuwa akinipambania na kunitia moyo. Huyu aliniwezesha kurudi tena chuo after 4 years. Nlianza na GPA ya 4.7 nikawa napanda.mpaka nimemaliza Chuo nlikuwa na GPA ya 4.8 nenda kawaulize Coet watakupa habari zangu.

Ndo kisa cha wadau kuniita Chizi Maarifa. Mimi nlikuwa napiga vipindi wanachuo wa masters wanakuja kwangu Hall 4 niwape shule.

Nitawasimulia mambo makubwa kwenye uzi wangu. Ila kuna details ntaficha sababu za kiusalama.
Dah!..una akili nzuri sana mkuu..
 
Sasa Elias alikua anakupa alternative tatu ya swali moja utasemaje huyo mtu anakariri, Mimi tu physics nilikua sikariri and that made us different

Anyway sijataka kubishana na huyo da Vinci because hamjui

Mimi nmekaa nae nmeishi nae, nmesoma nae pia
Kuna vitu vya kukariri lakini si physics wala hesabu kama hujui hujui na kama unajua unajua tu!
 
Back
Top Bottom