Mkuu,
Umekosea sana kumtukuza mja wa Mungu kama 'The Best Of The Best', hii sio sawa
Ukitaka kujua wanafunzi waliokuwa na akili zisizo za kawaida darasani katika masomo ya sayansi kuanzia sekondari hadi chuo jikite miaka kati ya 1966-1989, baada ya hapo hakuna kitu kwa sababu silabasi tayari zilikuwa zimebadilika na masomo kurahisishwa sana lakini kulikuwa na wigo mpana wa kupata maarifa nje ya mfumo wa darasani hasa mitandao nk.
Msingi mzuri wa mwanafunzi kukuza kipaji kwa matumizi sahihi ya akili ni kufundishwa na mwalimu aliyefaulu daraja la kwanza na masomo anayofundishwa ndio kafauli vizuri hapo ufundishaji ni wa moyo wote kuliko wa leo ambao lengo lao ni kipato tu.
Combination zifuatazo ndizo zilikuwa zinatoa wanafunzi wenye akili sana
1. CBA (Chemistry, Biology & Agriculture) mpaka mwaka 1987 shule ilikuwa ni moja tu chi nzima yenye wanafunzi 24 tu na sharti awe daraja la kwanza kutoka kidato cha nne);
2. PCM (Physics, Chemistry & Advanced Mathematics) wanafunzi wenye akili sana walikuwa wakipatikana kwenye shule maalumu za serikali au seminari; (Kibaha, Ilboru, Old Moshi, Pugu, Tambaza, Minaki, Moshi Tech, Tanga Tech, Galanos, Mkwawa, Mazengo, Weruweru, Ashira nk)
3. PGM (Physics, Geography & Advanced Mathematics) maelezo kama hapo namba 2
4. PCB (Physics, Chemistry & Biology) maelezo kama namba 2
5. CBG (Chemistry, Biology & Geography) maelezo kama namba 2
6. EGM (Economics, Geograph & Advanced Mathematics) maelezo kama namba 2
Kuna watu walipata A za masomo yote kuanzia kidato cha nee, kidato cha sita na chuo daraja la kwanza lakini utashangaa aliokuwa nao na walipata daraja la pili au tatu kwa sasa ni Maprofesa au PhD holders na utafiti kibao for nothing productive for personal or community advancement.
Kuna wengine anaweza asiingie darasani kwa siku kadhaa, haendi prep, hashiriki discussion session na wenzie lakini kwenye mtihani masomo yote anachukua A zote
Fomula ya kujenga ubongo vizuri ili uwe naakili isiyo ya kawaida ni kumsikiliza mwalimu darasani ABC principles anazofundisha kisha changamoto zote na njia sahihi za kukabiliana nazo utaziweza siku zote. Kusoma notisi, kutafuta rejea kwenyye vitabu mbalimbali na kushiriki majadiliano na wenzako ni nyongeza tu.