TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Chuoni mimi nilisoma uhasibu, Martin alisomea uchumi.sasa sababu mimi advance sikosoma uchumi nikamuomba awe ananifundisha uchumi maana kwenye kozi yetu ni lazima usome uchumi.
Jamaa alinifundisha uchumi nikapata A semester ya 1 na A semester ya 2.
Na alinifanya nisiwe na group discussion na wanafunzi wenzangu maana wenzangu waliokuwa wametoka ECA,EGM na HGE ndio walikuwa wanaongoza kufundisha kwenye ma-discussion group ya uchumi.Ila the way Chegere alivyonifundisha nilikuwa nawaona wanaongea pumba tu uchumi hawaujui.
Mimi nikawa ratiba yetu na Martin chegere ni kila jumapili jioni tunasolve maswali yote ya seminar ya uchumi na past papers.
Martin ameniachia alama ya A mbili za uchumi. Mungu ambariki the best TO of Tanzania in all time.
Nyongeza:
Nilichompendea Martin nilikuwa nikimfuata tusome na kusolve maswali alikuwa haniulizi in advance IFRS weekend ijayo tunasoma topic gani? Yeye anakuja na peni tu halafu anasolve maswali yote.
Ndio alipata PhD akiwa mdogo Kuna kipindi nilikuwa namuona udsm
 
Wana calculate hata first semister na mwaka ukiisha gpa inawekwa kabisa then kwenye cheti ndio wanaweka overall GPA, Mimi sijapata cheti Ila nikiingia kwenye ARIS yangu nakuta matokeo na GPA yake ingawa sijapata cheti

I am delighted to see you have quoted my comment, NVM, Akili yangu tokea nikiwa O level i have been dreaming to get good grades. I just got Div 2 in O level and Div 1.9 in A level NECTA exams..! PCB...! Nilitakaga kupata Kijiti cha heshima ila ubongo wangu ukawa umenisaliti [emoji3064] daah hizi akili bhana. Nikisikia mtu alipata kijiti cha Point tatu nawaangaliaga mara mbili nikijaribu kuwaza tu How smart these people are ?? Physics A daah [emoji23][emoji23]
 
Leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili.

Tunahitaji kuwa Karibu na Mungu wakati wote kwani safari yetu ipo mikononi mwake.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never forget you My brother.

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were. Rest in peace up in heaven.


-----
Pia soma




ALAMA ALIZOACHA ELIAS KIHOMBO


Imepita miaka takribani miaka 14 sasa, tangia Tanzania ilipopata kumshuhudia mwanafunzi alieshindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were.

Rest in peace up in the heaven

View attachment 1630262
View attachment 1630283
Nilimkuta library siku moja, yupo chemba aisee ...jamaa nafkiri hachoki kusoma. Wakati mimi natizama movie ya pili yeye bado anakula kitabu hahahaaaa.
 
I am delighted to see you have quoted my comment, NVM, Akili yangu tokea nikiwa O level i have been dreaming to get good grades. I just got Div 2 in O level and Div 1.9 in A level NECTA exams..! PCB...! Nilitakaga kupata Kijiti cha heshima ila ubongo wangu ukawa umenisaliti [emoji3064] daah hizi akili bhana. Nikisikia mtu alipata kijiti cha Point tatu nawaangaliaga mara mbili nikijaribu kuwaza tu How smart these people are ?? Physics A daah [emoji23][emoji23]
Mbona umejitahidi kwa hzo grades vizuri tu, ujue sio lazima tufanane kufaulu, pia duniani ya sasa ili uwe recognized ni wewe kufanya ubunifu na kugusa watu wengi. Mimi nimeridhika na grades zangu nilizopata na maisha yanaenda in our class mwaka wetu Kuna dada aliingia top ten ya kitaifa kwa ufaulu na yeye alikosa A ya somo ambalo Mimi ndio nilipata shule nzima, yupogo tu na maisha yake ya kawaida
 
Mimi mwaka 2000 nlipata A katika masomo yote matatu ya PCM. kifupi ni kuwa O- Level nilikuwa na B moja tu ya Kiswahili. A- level nikasimamisha misonge masomo yote.

Nilipokuwa Chuo UDSM. nliishi maisha ya manyanyaso sana toka kwa lectures pale Udsm. Nlinyanyasika sana. Mitihani yangu ikawa inasahishwa kwa umakini mkubwa kunitafutia makosa.

Semister ya kwanza nlikuwa na GPA ya 4.9 na pili 4.9

Mwaka wa pili semister ya kwanza 4.9 ya pili 4.8 walimu wakaanza kuwa na nongwa hasa kwa kuwa nlikuwa naonekana sometimes kuwarekebisha wanapokuwa wanafundisha. Nlikuwa mara nyingi napendekeza njia rahisi za ku solve maswali.

Nlidisco ktk mazingira ya kushangaza sana. Kesi yangu ilienda mbele za watu ambao baadaye wengine walikuja omba msamaha. Namkumbuka Prof mmoja ambaye alikuja gombea urais miaka ya nyuma huyu ndo alikuwa akinipambania na kunitia moyo. Huyu aliniwezesha kurudi tena chuo after 4 years. Nlianza na GPA ya 4.7 nikawa napanda.mpaka nimemaliza Chuo nlikuwa na GPA ya 4.8 nenda kawaulize Coet watakupa habari zangu.

Ndo kisa cha wadau kuniita Chizi Maarifa. Mimi nlikuwa napiga vipindi wanachuo wa masters wanakuja kwangu Hall 4 niwape shule.

Nitawasimulia mambo makubwa kwenye uzi wangu. Ila kuna details ntaficha sababu za kiusalama.
usisahau kunitag
 
Mbona umejitahidi kwa hzo grades vizuri tu, ujue sio lazima tufanane kufaulu, pia duniani ya sasa ili uwe recognized ni wewe kufanya ubunifu na kugusa watu wengi. Mimi nimeridhika na grades zangu nilizopata na maisha yanaenda in our class mwaka wetu Kuna dada aliingia top ten ya kitaifa kwa ufaulu na yeye alikosa A ya somo ambalo Mimi ndio nilipata shule nzima, yupogo tu na maisha yake ya kawaida

Absolutely correct, dunia inahitaji watu smart wanaokuja na inventions ambazo zinauwezo wa kuboresha maisha ya watu kiujumla. Tatizo jingine ambalo limefichwa sana na Watu tuwaitao Academicians hawa Phd and profs .. Research findings zao tangu waanze kupublish papers sijaona hata zikitumika kuboresha Maisha ya Watanzania kiujumla.
Hata Elias Kiombo huenda alikutana na watu ambao wanahangaika na projects ambazo hazina manufaa kwa jamii yetu walipomuona Jamaa na uwezo wake huenda walikuwa amazed na wenye husda wakamuona hawafai maana jamaa wangemtumia vyema huenda tungefanya au angekuwa na manufaa kwa Jamii yetu ukiachana na ishu zake za kuoiga mapindi mchikichini.
Ila hongera sana Mkuu, Ulipigia Tabora girls au Msalato.! I don’t trust my hunches though
 
Too sad,it is difficult to follow your passion in Tanzania.
How is it difficult to follow your passion in Tanzania?

Amesoma PCM, the one and only combination from which you can advance and study anything in college as long as you passed the missing subject in O Level, this according to UDSM admission prospectus.

Ame apply Engeneering mara mbili, kapata, Sasa Tanzania imemnyima nini?

Hapendi vipi Engeneering wakati ame apply mwenyewe mara mbili ????

Eti ana passion ya kufundisha lakini hakutaka kusoma ili awe mwalimu. He academic choices were a mess.

Mwamba wa Physics, tena mwenye passion ya Modern Physics, anafeli vipi Electronic / IT / Communication Engineering? Halafu tunataka kuilaumu Tanzania. Mbona nerds wengine hawafeli chuo?

The guy was unfocused and reckless.
 
Duh Mungu ampatie pumziko la milele huyu jamaa Mungu alikuwa amempatia kipaji cha kujua physics na mathematics pamoja na chemistry alinifundisha oswald Mang'ombe
 
How is it difficult to follow your passion in Tanzania?

Amesoma PCM, the one and only combination from which you can advance and study anything in college as long as you passed the missing subject in O Level, this according to UDSM admission prospectus.

Ame apply Engeneering mara mbili, kapata, Sasa Tanzania imemnyima nini?

Hapendi vipi Engeneering wakati ame apply mwenyewe mara mbili ????

Eti ana passion ya kufundisha lakini hakutaka kusoma ili awe mwalimu. He academic choices were a mess.

Mwamba wa Physics, tena mwenye passion ya Modern Physics, anafeli vipi Electronic / IT / Communication Engineering? Halafu tunataka kuilaumu Tanzania. Mbona nerds wengine hawafeli chuo?

The guy was unfocused and reckless.
Kufeli kwake hapa naona kumesababishwa na mazingira zaidi. Alikuwa hasomi,muda mwingi anatumia kufundisha tuition,angefaulu vipi ?
Huko kuomba Engneering mara mbili itakuwa wazazi au jamii iliyomzunguka ndo ilimforce,influence akasome Engneering ila yeye moyoni mwake passion yake ilikuwa kufundisha kuandika vitabu.
Yes Tanzania most of students wanasoma vitu kwa sababu kuna mkopo,au ndugu,jamii wamemwambia hiyo cozi ndo ina kazi ,mshahara mkubwa ukimaliza. Wengi hawana furaha na vitu wanasoma.
Ili uwe na furaha kwa kile unafanya. Fanya unachokipenda na utaona kila siku inapita haraka sana.
Na utakuwa na motivation kila siku. Hakuna kitu kizuri hapa duniani kama kuparsue career unayoipenda kutoka moyoni. Siyo kwa kuforciwa sababu ya mkopo au ndo kazi zinakopatikana.
 
Factors my foot. Mbona wengine wanamaliza ?

Kuna mambo hakuyaewa na mengine aliyasahau kila alipoingia chumba cha mtihani chuo. We he really an egghead after all?
Yes factors. Kama darasani alikuwa haingii,anaprefer kwenda kufundisha tuition, hapa anafaulu vipi ?Field anakwenda siku moja kati ya siku 40.Huyo kweli alikuwa na passion na Engneering ?
 
Kufeli kwake hapa naona kumesababishwa na mazingira zaidi. Alikuwa hasomi,muda mwingi anatumia kufundisha tuition,angefaulu vipi ?
Huko kuomba Engneering mara mbili itakuwa wazazi au jamii iliyomzunguka ndo ilimforce,influence akasome Engneering ila yeye moyoni mwake passion yake ilikuwa kufundisha kuandika vitabu.
Yes Tanzania most of students wanasoma vitu kwa sababu kuna mkopo,au ndugu,jamii wamemwambia hiyo cozi ndo ina kazi ,mshahara mkubwa ukimaliza. Wengi hawana furaha na vitu wanasoma.
Ili uwe na furaha kwa kile unafanya. Fanya unachokipenda na utaona kila siku inapita haraka sana.
Na utakuwa na motivation kila siku. Hakuna kitu kizuri hapa duniani kama kuparsue career unayoipenda kutoka moyoni. Siyo kwa kuforciwa sababu ya mkopo au ndo kazi zinakopatikana.
Ndoto nyingi za maskini haziko huru kaka,me nilipenda sana kuwa RUBANI nilifanya kila niliwezalo ili nifikie huko,nilivyofika A-level maajabu ndo yakaanziaga hapo.
 
Mkuu

Naona hatuelewani

Mimi nachopinga ni wewe kusema yeye ndio the best TO all these years

Nikakuuliza una evidence gani to prove that?

Ukasema kwavile kafundisha tuition ya Physics!

Nikakwambia thats nonsense maana sio yeye mwenye impact tu,kuna maTO wenzake wanafanya impact hapa duniani kupitia vitu vingine

Nikaongeza kwa kukwambia kwamba hii kusema marehemu yeye ndio mwenye impact pekee yake zaidi ya wengine wote si kweli ni maoni binafsi ya mtu tu kama wewe..

Kua mwalimu sio evidence kwamba wewe tu ndio mwenye impact hapa duniani

Kudai eti hao wanaofanya operations wamepita kwake si kweli ni baadhi tu,mostly hawajapita kwake...maTO wa nyuma yake hawajapita kwake na ni wengi,maTO wa mbele yake wamepita baadhi...

Nishakuelewa,utakua labda upo sekta ya ualimu ndio maana unavutia kwako kusisitiza ni mwalimu tu hapa duniani ndio ana impact wengine wote ng'ombe!

Hiyo ni mjadala mwingine...kwa hili tuishie hapa kwamba hayo uliyotoa ni maoni tu biased na hakuna research official iliyotoka
NAMBA ZINAONGEA,
kakague matokeo yake ya form 6, inasemekana kiwango chake chake cha ufaulu bado hakijafikiwa.
kingine jamaa kaandika vitabu vya physics . na kama unavyojua physics kitabu topic moja ni sawa history mwaka mzima, hiyo ndo impact kubwa aliyoifanya ukilinganisha na umrin wake naamini ni under 40.
Sasa kama socrate, eistein, plank, newton na wengine wengi
kuelezea impact yake kwamba ni the first na most biggest ever in this republic kwa impact done by any
m
Nimekwambia best sababu ni yeye peke yake aliwahi kuwa
TO 2004 O level
TO 2007 A level
Best student UDSM 2010
Nenda you tube utamkuta mahojiano yake na waandishi tofauti tofauti wa habari
tazamo wangu ni kuwa IQ, ya MR kihombo is unique, kwa fact mbili
masomo aliyochukua, vitabu alivyo andika na aina ya masomo aliyoandikia vitabu,
tatu vision zake, strategy zake na impact yake kwa jamii.
na hilo linajieleza hapa angalia idadi y awatu wanaokwambia wamesaidiwa na huyu mwamba.
 
Back
Top Bottom