TANZIA Rest In Peace Tanzania One (T.O), Elias Kihombo

Acha masihala dada yangu msuli wa PCB ,PCM na PGM haufanani kabisa na masomo yenu ya arts acha kabisa.Yaani kitabu kimoja mf Roger kukimaliza chote ni shughuli si ya kitoto,acha kabisa na hasa sisi tunaosoma shule hizi za serikali acha kabisa.

Mimi huyo jamaa kwangu ni genius,mimi mwenyewe nimesoma PCM advance, washikaji zangu kibao walisoma arts walikuwa wanakula bata na walifaulu vizuri sana advance.

Tena kama hawa PCB ndio daaah,nakumbuka Tanganyika Library kuna jamaa mmoja wa Pugu alikuwa anavipanga vitabu vya Biology,kuanzia kwenye unyayo mpaka magotini.
Mkuu,

Mchepuo uliokuwa mgumu advance miaka ya 1970-1988 ni CBA (Chemistry, Biology na Agriculture) wanafunzi 24 nchi nzima pointi 7 na shule ilikuwa moja tu hapo Shirika la Elimu Kibaha (Kibaha High School) several students were getting mad.

Ugumu wa PCM advanced level ni Chemistry maana inaharibu equilibrium ya kuweka kumbukumbu iliyo sahihi ya kile ulichojifunza ila Physics and Advanced Mathematics yanaleta raha sana maana yanapatana

Ugumu wa PGM ni Geography maana ina maneno mengin ya nadharia (literature ukilinganisha na Physics na Advanced Mathematics ambapo binomial functions, differential functions, integration functions, ietc yanapatikana kote kote.

Ugumu wa PCB ni Physics maana Chemistry na Biology zinawiana na kubebana (Matokeo ya mchanganyiko wa vitu-Chemistry na matokeo ya mchanganyiko asili-Biology)

Watu waliochukua Engineering, Medical Doctor, waheshimiwe daima maana mziki wake sio wa kitoto

Syllabus ya Cambridge ilikuwa ikitumika advanced level kwa masomo ya sayansi ni bora urejeshwe ili kuboresha taaluma
 
Dah huyu mwamba story zake nimesikia sana, Minaki sijui kama alifika ila walipitaga kina Walter tu.

Moody physics alifariki mkuu.. nimesoma sana kwake, notes zake zilikua zinakupa hints ukachimbe zaidi.
Yeahh!! Minaki kaja sana, wakati huo mwaka 2006-08 nipo Alevel katufundisha theory za physics na jinsi ya kufoji practicals..nakumbuka mwaka 2006 alishawahi kunyolewa nywele na mwl chungu alipokutwa bwenini Lumumba wakat ulikuwa mda wa parade, mwl chungu alifikiri n mwanafunzi wa minaki
 
Maisha hayako fair Ndo maana Mimi semister ya kwanza tu pale mipango ikanishinda huyo chap kwenye miradi ya baba mwaka mmoja baadae nikaozeshwa mke WANGU mzuri saiv napush ndinga ya 20+ m mke anapush yake ya maana crown watoto wawili jumba jumba kwel sio kujificha ilimrad pakuche now na 23 age NAKUSHUKURU MUNGU WEWE NDO MTOAJI NA MKADIRIAJI LAKINI POPOTE ULIPO NA HALI YOYOTE USILAUMU MAANA MUNGU ANAMAANA YAKE ANAWEZA KUKUPA ELIMU LAKINI MAISHA MAFUPI TENA YASIYO YA RAHA NA ANAWEZA KUKUPA PESA NYINGI LAKIN HAMNA WATOTO AU NDUGU HATA MMOJA KWAHYO TUSHUKURU KWA KILA KTU MAANA MUNGU ANAMIPANGO DHIDI YETU [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] WABILAH WA TWAIQFU
Planna ulimuacha Zilihona ama nani?? Mie nilimuacha Lifuriro.
Mipango elimu yao kukomoana, kama sekondari
 
Leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili.

Tunahitaji kuwa Karibu na Mungu wakati wote kwani safari yetu ipo mikononi mwake.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never forget you My brother.

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were. Rest in peace up in heaven.

-----
Pia soma

ALAMA ALIZOACHA ELIAS KIHOMBO

Imepita miaka takribani miaka 14 sasa, tangia Tanzania ilipopata kumshuhudia mwanafunzi alieshindikana katika masuala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama Kibaha, Ilboru, Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa Wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga Secondary kuendelea na masomo yake ya Advance Level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)

Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.

Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania, hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo, Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo (tetesi )

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011, 2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake Nyumbu na kuwa na Jeuri zaidi ya Akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amezamilia kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania kuwa na uwezo mkubwa darasani. Nlsikia jinsi ambayo eng elias alikuwa na kipaji cha kufundisha kuanzia asubuhi mpk jioni na kusitokee hata swali moja liliomtolea nje .siku ambayo alisolve maswali kuanzia saa moja hadi saa nne hakuna swali lililo msumbua saa tano hadi saa nane hakuna swali lililo msumbua saa tisa hadi saa kum na mbili hakukua na swali lililo msumbua tuliendelea na mwendo huo kwa muda wa wiki moja . Itabaki historia ktk maisha ya wanafunzi na elimu ya Tanzania kwa ujumla.

Lakin leo tunavyozungumza Elias Kihombo hatunaye tena duniani. Inasemekana kifo chake ni kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili. Tunahitaji kuwa Karbu na Mungu wakati wote kwan safari yetu ipo mikononi mwake. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!

I will never Forget you My brother

You will be missed forever and always. The beautiful moments you shared with me will always speak of a great person that you were.

Rest in peace up in the heaven

View attachment 1630262
View attachment 1630283
R.I.P
 
Mkuu baba swaleh iyo avatar picha yako ni majuzi tu nimegundua jamaa alikuwa anaitwa Nikola Tesla
 
2620126_Tosaboy.jpg
Huyu Tanzania one Elias Kihombo alikuwa kama Iran one Mohsen Fakhrizadeh yule nuclear scientist aliyeuwawa na waisraeli.
 
Elimu yetu haiwapi watu kama hao nafasi waka shine na pia choices za masomo ni chache.

Otherwise angepewa nafasi ya kusoma kitu ambacho anakipenda na anakimudu angemaliza vizuri tu, labda angevumbua na mavitu mengine ya Physics. Very sad.
Ishu inakuja stress za maisha, huku familia inakutegemea huku unahitaji ukae darasani n.k

Maisha ya chuo kikuu cha UDSM yanataka ukomae na madesa muda wote.Sishangai kusikia jamaa alidisco degree yake ya kwanza. Inahitaji utulie sana pale chuoni kwasababu mambo unayotakiwa uyasome ni mengi na muda ni mchache. Watu wengi wameingia UDSM na one zao za form Six ila mwisho wa siku wamedisco au kuambulia GPA za pass tu.
 
Vipi unaikumbuka comment yako #76?
Ndio mkuu wakati huo nilikuwa comment na ID yangu nyingine @mbususu ebthusiast kwasababu hii yangu ya maghayo ilipigwa ban. Nitakutag kwenye iyo ID.

Check page ya 4 comment #64
 
Ishu inakuja stress za maisha, huku familia inakutegemea huku unahitaji ukae darasani n.k

Maisha ya chuo kikuu cha UDSM yanataka ukomae na madesa muda wote.Sishangai kusikia jamaa alidisco degree yake ya kwanza. Inahitaji utulie sana pale chuoni kwasababu mambo unayotakiwa uyasome ni mengi na muda ni mchache. Watu wengi wameingia UDSM na one zao za form Six ila mwisho wa siku wamedisco au kuambulia GPA za pass tu.
Hakudisco kwa sababu ya kufeli, alidisco kwa sababu ya dharau kwa Malecture
 
Rest easy brother,[emoji120] Mungu akurehemu[emoji120] umeacha alama bora duniani, anaonekana alikuwa humble Sana , kupitia picha yake
 
Back
Top Bottom