Reuben Kwagilwa: Wakurugenzi tatueni changamoto msisubiri ziara za viongozi

Reuben Kwagilwa: Wakurugenzi tatueni changamoto msisubiri ziara za viongozi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Reuben Kwagilwa, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuendelea kuwasimamia watendaji walio chini yao ili watatue changamoto za wananchi kwa wakati, badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu ndipo hatua zichukuliwe.
Reuben Kwagilwa.jpeg
Maelekezo hayo yametolewa leo Februari 19, 2026 wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba,baada ya kuzindua jengo la Halmashauri ya Rombo na baadaye mkutano wa hadhara na wananchi kuibua hoja zilizohitaji majibu kutoka kwa viongozi wa ngazi za chini.

“Hoja ambazo zimewasilishwa na wananchi kuanzia hoja ya kwanza zimefika kama 15, na katika hoja hizo 15 hoja 10 ni za TAMISEMI. Hii inaonesha umuhimu wa Wizara yetu katika kuwahudumia wananchi,” amesema Kwagilwa.

Aidha, Mhe. Kwagilwa amesisitiza kuwa watendaji watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kushindwa kuwajibika kwa wananchi watakutana na hatua kali za kinidhamu na akionya kuwa Serikali haitavumilia uzembe unaokwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Reuben Kwagilwa1.jpeg

WhatsApp Image 2026-02-20 at 19.14.56.jpeg
 
Back
Top Bottom