emmarki
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,001
- 1,430
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G
Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu.
Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani
Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?