Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Namimi sikumlazimisha kupokea, kwanini nisimpe mwingine nikampa yeye?? Nilishamwambia mapema sana kuwa akicheza namimi atajuta maisha yake yote, tulikuwa na makubaliano yaani agano, so kwa kuwa amevunja agano basi adhabu hii haiepukiki
 
Kalikologaaa .....kamwaga ugali na wewe malizia mboga hakuna namna
 
ingelikuwa na Mungu analipa kisasi kama unavyolipa wewe binaadamu sote tungekuwa na alama za makovu kila sehemu ya mwili. Hakuna kitu kizuri kama kusamehe na ndio maana mtu anaependa kusamehe Mungu huwakusanya malaika wake na kuwashuhudisha oneni Mtu wangu amefanywa hivi na vile na amesemehe. basi pale pale unapewa cheo cha kuwa shujaa na Mungu anakuandalia malipo makubwa kwa ushujaa wako. Achana na ndoa kwa huyo mwanamke mkuu lakini samehe na utajisikia Amani kubwa moyoni mwako. Na ikiwa hutaki ushauri basi.
 
Mkuu nikuhakikishie, kamwe sitajutia hata siku moja.. kumbuka nilishamwambia mapema, anacheza na moyo wangu boya huyu
 
Nakushauri create group la whatsap kwa familia zote mbili then hiyo tarehe 7 rusha hizo SMS ulizoscreen shot na picha ulizodukua/
 
Pata picha alafu unamkuta ma mwingine, vipi... we ngoja tar.07 si inakuja
Una uhakika gani haingii humu jf, na utakuwa umesha mpa taarifa bila kujua?
Labda hata marafiki zake wamo humu..na event ya 7/1 wanaijuwa wana add 1 & 1.paap..wanamtonya kuhusu mipango yak ya revenge.
Naona hii ni stori tuu umeleta humu.
 
Una uhakika gani haingii humu jf, na utakuwa umesha mpa taarifa bila kujua?
Labda hata marafiki zake wamo humu..na event ya 7/1 wanaijuwa wana add 1 & 1.paap..wanamtonya kuhusu mipango yak ya revenge.
Naona hii ni stori tuu umeleta humu.
This is not blah blah braza.. hayupo jf mzee.
 
Mwisho wa siku anayeumia sana ni mwanamke,
Dunia inavyowachukulia wanawake na wanaume ni tofauti kabisa,
Wewe unaweza kuhisi umemkomoa mwanaume lakini mwisho wa siku unaishi kutumbukia kwenye lindi zito la matatizo.
Inawauma sana ikiwa kwenu, acha mnyooshwe
 
Natamani ningekuwa huyo binti,halafu niwe nimepata hii plan yako hapa. Ningekupiga bonge la suprise hadi ungejiona mjinga
 
Inawauma sana ikiwa kwenu, acha mnyooshwe

Siyo jambo jema kumdanganya mwenza wako,
Japo binafsi huwa siwezi kukosa usingizi kisa mwanamke kanidanganya,
Akichepuka ni kwa hasara yake mwenyewe wala hanikomoi kabisa mimi.

Lakini ukweli ni kwamba kuna mambo akifanya mwanamke wa kitanzania jamii ni lazima istuke na kumdharau.
Jinsi mwanamke wa kitanzania anavyoonekana kwenye jamii, siku akichepuka ni ijulikane wazi basi ajue ndiyo mwisho.
Huu ndiyo ukweli ndugu yangu na kwa faida ya wanawake wote humu (Usichepuke kabisaaa sheria za jamii ziko kukundamiza wewe hata kama unaonewa)
 
Jamii ndo sisi nami nasema mnyooshwe tu teh
 
Namimi sikumlazimisha kupokea, kwanini nisimpe mwingine nikampa yeye?? Nilishamwambia mapema sana kuwa akicheza namimi atajuta maisha yake yote, tulikuwa na makubaliano yaani agano, so kwa kuwa amevunja agano basi adhabu hii haiepukiki
Mkwara mbuzi tu huo.
 
Utatupa feedback
 
Wapo wanaocheat ila binafsi si cheat na niko upande wa wanaume wasiocheat kama mtoa mada. Asikwambie mtu ukiwa loyal kwa mwanamke halafu akakuletea mapicha inauma sana mkuu!
Nakubali kwamba inauma Kama ikiwa nawe hufanyi hayo kwa 100%.

Ila ni lazima tuukubali uhalisia kwamba huyo sio wakwanza na kamwe hatakuwa wamwisho kufanya kitu cha namna hiyo, hivyo hicho anachowaza kukifanya huyu ndugu yetu si salama Kwake na Kwa Familia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…