Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

OMBI: Me ikipita hiyo tarehe siku ya pili naomba namba yake tu
 
Kulipiza kisasi kinawatuliza wengi.

Ningekuwa mimi ninheprint hizo chats zote halafu niweke kwenye bonge la kadi. Ile wananisubiria nawaandaa kabisa tunakuja halafu nampa dereva tax apeleke hiyo zawadi na ageuze chaap.

Nazima simu, wakiona nimechelewa hadi jioni watafungua zawadi tutakuwa tumemalizana juu kwa juu Hahaha
Hiyo nayo imetulia kiaina...
 
Kama nikweli na sio chai, hii itakua mbaya, unaweza kujikuta unajibu kesi ya manslaughter, na ujue atakaeumia sio yeye pekee, utaidhalilisha familia yake ambao hawakumtuma kufanya hayo(they are innocent), utadhalilisha familia yako especially mama na dada zako na mtageuka talk of the town, ila kwa sababu umeamua na bichwa lako limejaa kiburi na revenge utafikiri hiyo K uliambiwa na mganga wako ndiyo itakua ya mwisho kuchovya na hautapata nyingine, Jiandae kutibu kidonda cha majuto unless wewe sio binadamu wakawaida.
 
Umeonaee,wenyewe wanakuwa wachungu kweeli,

Ukimfumania demu wako unaempenda kwa dhati kweli machungu yatakuepo
Na yataisha
Sasa ya mwenzetu hapa kafumania kuwa dem wake analiwa TIGO(tumekusomaa,,!!)
Hapo sio MACHUNGU tu ni pamoja MAUMIVU kuliko hata ya mjamzito anapojifungua[emoji3]
 
Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
Mkuu achana nae tu ,hakuna haja ya kuonesha picha coz hata ww utadhalilika tu,kwann upoteze mda na hela ya nauli na maandalizi?kumuacha ni pigo tosha kwake ,toa taarifa na udhibitisho kwa baba yake mkiwa wawili tu yule ni mwanaume mwenzako ataelewa,mim binafis sina iman na wanawake huwanakula na kusepa since longtime ,kikubwa n kutafuta mtoto tu ili hata siku ukifa uache coppy na ufute laana
 
Duh,,sipati picha hali ya bi harusi ilikuwaje.!

Kavurugwa sana sanaaaa,
Kila mtu anayetaka kumchumbia akipewa ule mkasa basi anachapa rapa asubuhi kweupeeee.
Dada zangu ndiyo wamekuwa mavuvuzela ya kueneza hizi habari kwasababu wanamchukia sanaaaaa.
Ameisha sana yule dada na uzuri wote umepotea, juzi nimerudi Dar nikamkuta ana msongo wa mawazo hadi huruma.
 
Inapendeza kuona mwanaume kaonjeshwa cha mtema kuni...
Cc Heaven Sent

Mwisho wa siku anayeumia sana ni mwanamke,
Dunia inavyowachukulia wanawake na wanaume ni tofauti kabisa,
Wewe unaweza kuhisi umemkomoa mwanaume lakini mwisho wa siku unaishi kutumbukia kwenye lindi zito la matatizo.
 
Mm ni mwanamke, nimeumia sana pale unapompa MTU moyo wako akauchezea.

Wewe uko kama mm nikimpenda MTU nimemaliza, tamaa zote naweka chini, na kipindi hicho nakutana na visu vikali sana, ila najipa moyo kuwa huyu ni shetani hawezi kumzidi bf wangu, kiukweli na huwa no sitowagi

Wakuu hakuna mwaka niliopata vishawishi kama huu, tiyari nishapata Bf yupo mbali nampenda namuheshimu, yaan utafikiri yupo karibu nami,

Kazi ninayoifanya lazima nikutane na high class people, kwenye lift naenda ofisini ndo ysiseme, nakutana na wanaume balaa ila naajipa moyo kuwa L ni the right person.

Juzi nimeenda kutembelea Wateja( marketing) nilikutana na mkaka baadae ya kumuelezea tunachokifanya nikaondoka kabla sijafika mbali akaniita,

' Dada umeolewa, nikajibu,hapana ila Nina mchumba, akauliza tena " a u sure ni the right person kwako? Nikajibu ndio, akasema " mm Niko kwenye maandalizi ya kutafuta mchumba ambae unataka niwe nae kwenye mahusiano miezi 6 afu nioe kama mambo yataenda sawa, maana kila.kitu nimeshafanya, kama umenidanganya nakupa dk 10 jitafakari unipe no, nikamjibu hapana kaka Nina mchumba, kaondoa ndinga yake kaondoka.

Imagine haya yoteee na mengine ambayo sijasema najibana, kwa ajiri yake Leo MTU akifanyie ujinga??

Sijawahi kucheat nikiwa tiyari kwenye mahusiano mungu ndo shahidi.

Mleta mada revenge 100× MTU kuchezea moyo wako ni ujinga, yaani una full support yangu, kama ni kutafuta petrol mm nakupa kiberit,(kidding) tho usifanye hivi

Go go go gooo trh 7 mrejesho plz

Mhhhhhh,
Lakini hiyo adhabu ni nzito sana aisee!
Yani itamtia huyo dada kovu la maishaa.
Hata kuolewa kwake kutakuwa kugumu sana endapo jamaa atamwaga kila kitu.
 
Back
Top Bottom