Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
========

UPDATE: Mrejesho tayari fuatilia

Kufuatilia mrejesho wa tukio hili bonyeza link hapo chini

Mrejesho: Sehemu ya kwanza
Mrejesho: Sehemu ya pili

Mrejesho: Sehemu ya tatu
Mrejesho: Sehemu ya nne

Mrejesho: Sehemu ya tano
Mrejesho: Sehemu ya sita

Mrejesho: Sehemu ya saba
Mwisho
Sasa kama hutaki ushauri yanini kutuwekea huu upuuzi. Utakapopigwa visu ndo utakumbuka maneno haya. Achana naye ana maisha yake nawe una yako
 
Alifanya ukatili sana ategemee malipo na yeye kwann hakumuacha tu na maisha yake? Atakuwa na matendo magumu sana atajikuta anaoa kila siku......anafanya ivo ukute ata mtu anayemuita baba ake sio biological faza ata maza ake alikuwa na mazambi vilevile
Nakukubali Sana we msweet ila kwa comment hii umeniangusha

Mtu ukimchukia haimaanishi kua ukimuombea mabaya ndo yatamkuta

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
[emoji28][emoji28][emoji28] Kuna vinasaba vya gahawa humu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kuna kipande kimeniacha hoi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Baba wa binti akaongea mengi km kunilauma mim, nikaon ananiletea uhuni, nikamchana kwamba nilishamweleza kwamba akifanya ushenzi namim nitafanya ushenz na hizo msg kwenye simu zipo na kama binti atakataa nazionesha vile vile jinsi tulivyokubaliana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni binti kutaka kutoa 0713
Unajua mimi sikubaliani na binti kufanya usaliti,amefanya udanganyifu na udanganyifu ni dhambi.
Na jamaa alikuwa na haki ya kumuacha kabisa, hata ingekuwa mimi..mtu msaliti siwezi kuendelea naye hata iweje.

Shida ni namna alivyomuacha,
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kumdharirisha hivyo?
Kwanini asimuonyeshe tu vithibitisho na kumuacha pasi na kwenda hadi kwao kama baba yake alivyosema kwamba kwanini hakusema tu ili wapige simu kwamba hawataenda kuonekana.

Namna alivyomuacha ndicho kitu tunakiongelea hapa.
Imemgharimu binti na matokeo yake hayo madhara naye anaanza kuyasuffer..si yeye kwamba yupo salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Big up, msimamo ndo kila kitu. Ila huyo demu kula tu, hana madhara, na ikiwezekana weka ndani kabisa maana anajua misimamo yako
 
Usikute mtoa mada ni mtu mpole sana na huenda akawa ndiyo yule mwanachuo muoaji aliyependa vya kunyonga.

Kama ilivyo title za thredi nyingine tu... Mfano

"Hebu mshauri huyu rafiki yangu" (kumbe ni yeye mtoa mada anahitaji ushauri)

Ila nimependa upole wa mtoa mada na msimamo wa yule jamaa mwingine.
 
Back
Top Bottom