Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Mkuu, nimepata nafasi ya kusoma huu mkasa wako kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa umakini sana. Ni wa kusisimua sana. Nina haya ya kusema.
1.Kama yote ambayo umeyaandika yana ukweli (ikiwa na pamoja na kwamba wewe huwezi kuwa na mahusiano ya kingono au kugonga wanawake wawili kwa wakati mmoja) basi itoshe kusema kwamba wewe ni mmoja kati ya wanaume wachache sana duniani ambao wanaelewa hasa na kuiishi maana ya commitment ya kingono.
2.Aliesema kwamba ukianza safari ya kulipa kisasi basi uchimbe makaburi mawili kwanza, hakukosea. I hope umeshaandaa hayo makaburi, naona yakienda kuhitajika muda si mrefu ujao.
3.Huyo rafiki wa huyo binti ni tatizo kubwa sana kwako (ni weak link, au wahuni wanaita "loose end"), kuna uwezekano mkubwa sana yeye akawa kiungo muhimu kwenye kuhitajika makaburi mawili niliyotaja hapo juu. Kama unaweza, kata mawasiliano ya aina yote na yeye before it is too late.
4.Sometimes, we learn the most important lessons in life the hard way. I hope you wont have to.
Nina shida moja katika maisha yangu, nayo kuwa tayari kupokea ninachostahili, kuna kosa nililifanya kwenye project moja hivi ikanisababishia nipoteze mamilioni ya pesa wala sikwenda kuomba msamaha wala kubargain nilipoteza ile fedha, namimi huwa nampa mtu anachostahili lakin natahadharisha kabla, kwahiyo akisema aje na kisasi nayeye, asee balaa lake sijui litakuwaje, ngoja tusubiri tuone, of course mimi mwenyewe sio mwepesi sana, anyway ngoja tusubiri tuone.
 
Nina shida moja katika maisha yangu, nayo kuwa tayari kupokea ninachostahili, kuna kosa nililifanya kwenye project moja hivi ikanisababishia nipoteze mamilioni ya pesa wala sikwenda kuomba msamaha wala kubargain nilipoteza ile fedha, namimi huwa nampa mtu anachostahili lakin natahadharisha kabla, kwahiyo akisema aje na kisasi nayeye, asee balaa lake sijui litakuwaje, ngoja tusubiri tuone, of course mimi mwenyewe sio mwepesi sana, anyway ngoja tusubiri tuone.
Aiseee[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
We mwamba[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
========

UPDATE: Mrejesho tayari fuatilia

Kufuatilia mrejesho wa tukio hili bonyeza link hapo chini

Mrejesho: Sehemu ya kwanza
Mrejesho: Sehemu ya pili

Mrejesho: Sehemu ya tatu
Mrejesho: Sehemu ya nne

Mrejesho: Sehemu ya tano
Mrejesho: Sehemu ya sita

Mrejesho: Sehemu ya saba
Mwisho
mkuu utauwa mtu
 
Wote wanaotetea tabia za huyo dada nao ni wasaliti tu kwa waume wao. Kama una mwanaume na anakuhudumia kwa kila kitu kwanini unakubali kitumbua chako kiliwe na mwanaume mwengine, huo kwangu ni ushamba tena wa kiwango cha standard gauge. Mimi mtu msaliti simpendi na sipo tayari awe pamoja nami kwenye maisha yangu iwe rafiki,ndugu au mume wangu. Nikishakujua msaliti nakukwepa nakaa mbali na ww. Tuwe waaminifu jamaniiii
Tena kinaliwa kwa Pesa maana yake kauza (malaya) pili inavyoonyesha alikuwa anaenda kutoa side B apo ni Zaid ya uzinzi na uasherat

Muda mwingine watu wanatetea upuuzi tu.

Uzuri jamaa alimuonya kabisa demu, so mwnmke alishindwa kujizuia kuendekeza Tamaa

Mwisho kabisa jamaa ww ni Zaidi ya mwnAume Big up sana ww ni Amir jeshi mkuu
 
Una roho mbaya shetani anasubiri.Sijui wewe ni mpagani maana hata neno la msamaha kwako limekupita kushoto utadhani hujawahi kutenda dhambi.Wanawake wenzangu ombeni sana Mungu msipate na mijianaume kama hii haishindwi kukuchoma na gunia tano za mkaa.Kisasi gani hicho kisichokwisha?
Mbona yupo sawa tu roho mbaya gani hiyo na kwani inasemaje
 
Kuna watu humu wananiita mimi katili lakin wanasahau ukatili niliifanyiwa na huyu binti, mazee huyu binti nimewahi kumpa million 1 na laki 2 kwaajili ya kumsaidia kweny msala fulan, nikiona itafaa nitaujumuisha huko mbele. Nilimpenda na kumpa good life la viwango vya juu. Acheni nyie
Mi nakuelewa sana aseeh!sijui kwa nini sipendagi mtu amsaliti MTU!!nachukia sana usaliti!
 
TUENDELEE...


Nikaona mambo yasiwe mengi, nikamwambia poa aende akamrudishe rafiki yake kwenye ndoa yake and mimi nitamfkiria kuhusu ombi lake, nilishajua tayari ashakuwa dhaifu kwangu so hawezi kunizid maujanja, hata km anasema uongo bado hauwez kuniathiri maana lazima nimzid akili, kwanza ananipenda kimapenz hivyo tayari yupo kwenye ugonjwa wa akili hawezi kushindana namimi mwenye akili timamu, and nikapanga kabisa kwamba siwezi kuwa naye yule manzi.

Akaenda akamdanganya kwamba nimepata ajali na nina hali mbaya nimekimbizwa India, na kwa jinsi hali ilivyo sijui km nikipona nitabaki na uwezo wa kufanya chochote Kwahiyo akamwambia rafiki yake akakomae tu na ndoa yake, na akaishi na yule mwanaume maana kwangu tena maji yameshamwagika, binti akaona hakuna jinsi akarudi kwa mume wake, jamaa ndo hivyo akampokea maana ndo km anakopatia ridhiki, nasikia kumbe kipindi anakuja huku alikuwa tayari kanasa ujauzito wa mshikaji, ndo huyu rafiki yake akawa ananiambia alikuja kugundua baadaye km ni mjamzito means km mimi ningejichangnya kuwa naye kipind hiki basi ningetupiwa hilo zigo kumbe la mume wake huko.

Japo binti hana amani kwenye ndoa ile so dizain km anapanga mbinu amtoroke aende akaishi maisha yake peke yake. Huyu rafiki yake akaniambia yupo kwenye process ya kutoa ile mimba maana hataki kuzaa na mshkaji wake, then apotee kokote akaishi mwenyewe. By the way hainuhusu hiyo sasa, azae asizae, aishi au aondole anajua yeye.

Maisha yangu yameanza upya na dizain km yule demu karidhika na kuamin kwamba sipo nchini nipo India kwa matibabu, maana baadaye ikanilazimu nibadili tena namba za simu, sasa mtihan ninao kwa huyu rafiki yake maana ananipenda na anataka nitimize ahad maana kazi ameshaifanya. Hadi leo sijamla na sitamla, na hili kwangu ni dogo sana na nitalimaliza tu kirahisi.

Nimepata aman sana na sikumbuki ubaya na maumivu yote aliyonitendea yule binti, nimeridhika kwa hiki.

Yapo mambo mengine nimeyaexclude maana stori ingekuwa ndefu sana, ahsanten kwa kunifuatilia tangu mwaka 2017 hadi leo 2021.

MWISHO,
Mkuu inafaa kutolea movie kabs hii story yako
 
Back
Top Bottom