Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Unajua mimi sikubaliani na binti kufanya usaliti,amefanya udanganyifu na udanganyifu ni dhambi.
Na jamaa alikuwa na haki ya kumuacha kabisa, hata ingekuwa mimi..mtu msaliti siwezi kuendelea naye hata iweje.

Shida ni namna alivyomuacha,
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kumdharirisha hivyo?
Kwanini asimuonyeshe tu vithibitisho na kumuacha pasi na kwenda hadi kwao kama baba yake alivyosema kwamba kwanini hakusema tu ili wapige simu kwamba hawataenda kuonekana.

Namna alivyomuacha ndicho kitu tunakiongelea hapa.
Imemgharimu binti na matokeo yake hayo madhara naye anaanza kuyasuffer..si yeye kwamba yupo salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani wakati binti anafanya usaliti hakufikiria jinsi inavyomgharimu jamaa?, acha utetezi wa ovyo. Jasho la mwanaume liliwe na bado mwanamke afanye usaliti njenje?, kingine mhusika aliambiwa akiri kosa lake mbele ya wazazi ila akazidi kukaza kuwa hakufanya kosa lolote, hakuna kitu kibaya sana kinachokera kama mtu muongo anayejitetea kwa uongo wakati tayari ushahidi upo. Ni kumchoma tu na ushahidi aone mapuuza yake mbele ya watu

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Nimegundua kupitia comment wengi humu si waaminifu, mnapenda sana kusamehewa mkijiwekea kinga mkikosea nanyinyi msamehewe, ukikosea utalipia na ndo kanuni ya maisha ilivyo, kabla sijafanya lolote nilimtahadharisha huyu binti, wala haikuwa surprise kwa kilichotokea, alafu mbaya zaidi kuna wanaume humu nao wanasema eti mimi katili, ndo wonder mnapelekeshwa na wanawake zenu, malofa kweli.
Exactly mkuu ndio uhalisia wao, utakuta hata misimamo hawana kabisa aiseee

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Dada Kama siyo Muhusika Basi unachotetea siyo sawa katika Wanawake wote waliofuatilia Huu Uzi wewe umekugusa Sana kwa alichokifanya na unaona Ni sawa alichokifanya Mwenzio kutoa tigo ilihali anadanganya uaminifu wa kuolewa. Tigo Ni dhambi na afanye hasitahiri huruma yoyote. Sasa angeolewa angefanyaje kuzuia yatokanayo na utowajo wa tigo
Nionyeshe sehemu niliyosema alichofanya binti ni sawa.
Nasubiri hapa, unionyeshe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wakati binti anafanya usaliti hakufikiria jinsi inavyomgharimu jamaa?, acha utetezi wa ovyo. Jasho la mwanaume liliwe na bado mwanamke afanye usaliti njenje?, kingine mhusika aliambiwa akiri kosa lake mbele ya wazazi ila akazidi kukaza kuwa hakufanya kosa lolote, hakuna kitu kibaya sana kinachokera kama mtu muongo anayejitetea kwa uongo wakati tayari ushahidi upo. Ni kumchoma tu na ushahidi aone mapuuza yake mbele ya watu

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, nimepata nafasi ya kusoma huu mkasa wako kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa umakini sana. Ni wa kusisimua sana. Nina haya ya kusema.
1.Kama yote ambayo umeyaandika yana ukweli (ikiwa na pamoja na kwamba wewe huwezi kuwa na mahusiano ya kingono au kugonga wanawake wawili kwa wakati mmoja) basi itoshe kusema kwamba wewe ni mmoja kati ya wanaume wachache sana duniani ambao wanaelewa hasa na kuiishi maana ya commitment ya kingono.
2.Aliesema kwamba ukianza safari ya kulipa kisasi basi uchimbe makaburi mawili kwanza, hakukosea. I hope umeshaandaa hayo makaburi, naona yakienda kuhitajika muda si mrefu ujao.
3.Huyo rafiki wa huyo binti ni tatizo kubwa sana kwako (ni weak link, au wahuni wanaita "loose end"), kuna uwezekano mkubwa sana yeye akawa kiungo muhimu kwenye kuhitajika makaburi mawili niliyotaja hapo juu. Kama unaweza, kata mawasiliano ya aina yote na yeye before it is too late.
4.Sometimes, we learn the most important lessons in life the hard way. I hope you wont have to.
Exactly mkuu ukp sahihi kabisa. As usual to tie all loose ends

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Wote wanaotetea tabia za huyo dada nao ni wasaliti tu kwa waume wao. Kama una mwanaume na anakuhudumia kwa kila kitu kwanini unakubali kitumbua chako kiliwe na mwanaume mwengine, huo kwangu ni ushamba tena wa kiwango cha standard gauge. Mimi mtu msaliti simpendi na sipo tayari awe pamoja nami kwenye maisha yangu iwe rafiki,ndugu au mume wangu. Nikishakujua msaliti nakukwepa nakaa mbali na ww. Tuwe waaminifu jamaniiii
Si ndio hapo mkuu nawashangaa sana hawa wadada wanaomtetea mwanamke mwenzao [emoji2] ukute nao pia ndio tabia na hulka zao hawaoni shida hata

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu sisi hatujapinga huyo binti kuachwa,usaliti ni kitu kibaya na sidhani kama kuna mtu anatetea usaliti.
Tunachosema sisi ni namna uliyomuacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jino kwa jino lazima kiumane, kwani huyo binti alipokuwa akihudumiwa vyote hivyo na bado akamsaliti limuacha jamaa namna gani? Acha kutetea upande mmoja

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu kutendwa nimewahi,kusalitiwa nimewahi na hasara niliyoipata ni ya muda wangu..lakini sikuhangaika kulipa kisasi,Mungu mwenyewe alilipa.Ni swala la muda tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa siku upate hasara ya vyote, usalitiwe, upotezewe muda, upptezewe rasilimali na jasho lako ndio utaelewa [emoji851] mahusiano mengi mwanamke ndiye mnufaika mkuu

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Katika hii hadithi ni kweli kabisa mwanaume hakuwa msaliti na namsifu sana kwa kuwa na msimamo huo kwani ni wanaume wachache sana kama si pekeyake mwenye huo msimamo dunia yetu ya leo.

Mwanamke/binti amefanya usaliti na simtetei kwa kufanya usaliti kwa sababu ni tabia mbaya,pia ni halali yake kuachwa.

Shida ni namna mwamba alivyomuacha huyo binti,
Kulikuwa na ulazima gani wa kumdharirisha??

Sent using Jamii Forums mobile app
Na je kulikuwa na ulazima gani kwa binti kukana mashtaka hata baada ya kupewa nafasi kwa kuulizwa na akajitetea ujinga kuwa hakufanya usaliti wowote?, aliyechangia huo moto kuwa mkubwa ni binti yeye mwenyewe tu.

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Jino kwa jino lazima kiumane, kwani huyo binti alipokuwa akihudumiwa vyote hivyo na bado akamsaliti limuacha jamaa namna gani? Acha kutetea upande mmoja

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
Sijatetea upande mmoja boss.

Nimesema pia kwamba binti kwa aliyoyafanya anastahili kuachwa.
Nachukia sana usaliti & udanganyifu..hata ningekuwa mimi,nikimkamata mtu ananisaliti namuacha.
Hiyo jino kwa jino ndiyo ambayo mm sikubaliani nayo...naamini Mungu huwa analipa vizuri.

Lakini anyway,huenda alifanya hayo maamuzi akiwa na hasira..mtu akishakuwa na hasira basi anaweza fanya lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona tatizo lipo hapa.
Mkuu wangu siku nyingine jitahidi kufwata hii kanuni[emoji116]

9. Epuka kumhonga mchumba vitu vya thamani kubwa, kumsomesha nk.
Usiwekeze Sana kwa mchumba. Lakini Kama unadhani uchumba ukivunjika hutaumia mpe ila Kama unaona uchumba ukivunjika utaumia usimpe.

Simaanishi wachumba wasisaidiane, kuna viwango vya kusaidiana wachumba. Mengine hayo ukitaka kuyafanya weka ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hili tunaelewana sasa [emoji41]

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Sasa siku upate hasara ya vyote, usalitiwe, upotezewe muda, upptezewe rasilimali na jasho lako ndio utaelewa [emoji851] mahusiano mengi mwanamke ndiye mnufaika mkuu

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119].

9. Epuka kumhonga mchumba vitu vya thamani kubwa, kumsomesha nk.
Usiwekeze Sana kwa mchumba. Lakini Kama unadhani uchumba ukivunjika hutaumia mpe ila Kama unaona uchumba ukivunjika utaumia usimpe.

Simaanishi wachumba wasisaidiane, kuna viwango vya kusaidiana wachumba. Mengine hayo ukitaka kuyafanya weka ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okee.
Sawa haina shida kama ulivyosema.
Lakini mkuu kwa mfano ungemuacha tu bila kufanya hivyo,ungejisikiaje?
Na je, unajisikiaje sasa kumuona yupo katika hiyo hali kama kichaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Asingejisikia vizuri maana maumivu ya kusalitiwa na bado mhusika akakufanya mjinga mbele za watu huwa hayafutiki kirahisi hivyo, mimi naamini kama binti angekiri kumsaliti jamaa mbele ya familia nzima na kuomba msamaha walau jamaa asingeonyesha ushahidi wa zile texts etc walau nafsi yake ingetulia na kumaliza hilo jambo kiubinadamu kabisa. Shida ni mtu kapewa nafasi ya kukiri na badp akakaza kuwa hana kosa, kingine ni baba wa binti moto aliouchochea ndio huo jamaa akatoa ushahidi wote. Acheni kuyakandia maamuzi ya jamaa zingatieni mambo yaliyochochea hadi akaweka ushahidi hadharani.

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
 
Na je kulikuwa na ulazima gani kwa binti kukana mashtaka hata baada ya kupewa nafasi kwa kuulizwa na akajitetea ujinga kuwa hakufanya usaliti wowote?, aliyechangia huo moto kuwa mkubwa ni binti yeye mwenyewe tu.

Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app
Matatizo yote chanzo chake ni binti..hilo najua.
Ila kwa mazingira aliyokuwa nayo,si rahisi sana namna hiyo kukiri hilo kosa pale.

Ila haya mambo ni magumu sana,
Kuna wanawake hawajui wanataka nini maishani.
Kuna wanaume pia hawajui wanataka nini maishani... though upande wangu naona ningeacha tu bila kulipiza kisasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom