KipajiTz
JF-Expert Member
- Sep 15, 2016
- 743
- 880
Kwani wakati binti anafanya usaliti hakufikiria jinsi inavyomgharimu jamaa?, acha utetezi wa ovyo. Jasho la mwanaume liliwe na bado mwanamke afanye usaliti njenje?, kingine mhusika aliambiwa akiri kosa lake mbele ya wazazi ila akazidi kukaza kuwa hakufanya kosa lolote, hakuna kitu kibaya sana kinachokera kama mtu muongo anayejitetea kwa uongo wakati tayari ushahidi upo. Ni kumchoma tu na ushahidi aone mapuuza yake mbele ya watuUnajua mimi sikubaliani na binti kufanya usaliti,amefanya udanganyifu na udanganyifu ni dhambi.
Na jamaa alikuwa na haki ya kumuacha kabisa, hata ingekuwa mimi..mtu msaliti siwezi kuendelea naye hata iweje.
Shida ni namna alivyomuacha,
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kumdharirisha hivyo?
Kwanini asimuonyeshe tu vithibitisho na kumuacha pasi na kwenda hadi kwao kama baba yake alivyosema kwamba kwanini hakusema tu ili wapige simu kwamba hawataenda kuonekana.
Namna alivyomuacha ndicho kitu tunakiongelea hapa.
Imemgharimu binti na matokeo yake hayo madhara naye anaanza kuyasuffer..si yeye kwamba yupo salama.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent from my AMN-LX9 using JamiiForums mobile app