Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

Riba za mikopo kwa watumishi, CRDB na NMB

naomba nichangie kwa sehemu cha kwanza ni njia ambayo inatumika kupata riba ni ipi?kuna straight line na reducing hapo utagundua mkopo mmoja lakin utalipa riba tofaut kutokana na njia anayotumia kucharge riba.Pili kuna suala la bima inalipwa kila mwez au mara moja wakati wa kukupa mkopo.Mfano bank x wao riba ni 17% na bima wanakata kila mwez 2% so hapo watasema riba tu ila hlo la bima hawakwambii utakuta kiukwel unalipa 20% kwa mwaka na bank y wao riba ni 20% bima wanachaji unapopata mkopo tu. So suala la wap riba kubwa inategmeana pia na gharama zinazo ambatana na mkopo huo,Ieleweke ya kwamba ukikaa na hela za mkopo muda mfupi riba ni ndogo na ukikaa nazo muda mrefu na riba ni kubwa.Tulilamike riba kubwa tu je na hizo hela tunakaa nazo muda gan.
Hvi mkopo wa miaka mitano unaruhusiwa kurejesha kwa.mwaka mmoja?.
 
Hvi mkopo wa miaka mitano unaruhusiwa kurejesha kwa.mwaka mmoja?.
nachojua kulipa mkopo haikatazwi ikiwa umepata hela sema kuna baadhi ya taasisi aisee mpaka wakubali ni issue na watakulipisha na fine, kwa mabank nadhan iko sawa utalipa only principal plus accrued interest
 
nachojua kulipa mkopo haikatazwi ikiwa umepata hela sema kuna baadhi ya taasisi aisee mpaka wakubali ni issue na watakulipisha na fine, kwa mabank nadhan iko sawa utalipa only principal plus accrued interest
Hapo kwenye kidhungu umeniacha mkuu,.
mfano nimekopa 6,000,000/= Kwa miaka5 natakiwa kulipa 10,000,000/=.Je nikiamua kuachana na huo mkopo wa 6,000,000/=kwa mwaka mmoja nitalipia riba ya mwaka pekeyake?.au kutakuwa na ghara zingine?
 
mk
Piga hesabu za marejesho yote toa hiyo hela uliyopokea kinachobaki ndio riba kwa ujumla wake halafu angalia ni kiasi gani
mkuu sio kweli unacho kisema, hiyo tofauti unayo isema sio riba, fafanua vizuri watu wakuelewe
 
riba I = PRT/100
kama R= 17%
p= 12000000
T= 5
12000000x0.17x5= 10200000
riba kwa miaka mitano= 10200000
kwa hiyo ukichukua 12,000,000
riba kwa mwaka 10200000/5=2040000/=

utarudisha hela za watu 22200000/=
kwa miaka mitano
Lazima ujue is it compound interest or?
 
kitu ambacho ujue ni kwamba kias cha bima kiko subjected kwa muda wa mkopo sio fixed amount,nilichojifunza mie ktk mikopo hyo ni kwamba bima wana calculate hivi:

1)wanaochaji pale unapo pata mkpo ni
kiasi x asilimia ya bima x muda(mwaka 1,2,34 n.k)

2.wanachaji katika kiasi kilichobaki cha mkopo na utagundua hapa utaanza na makato ya riba makubwa na kadri mkopo ulishuka na bima inashuka

Na karibia taasisi zote zinazokopesha zina hii gharama ya bima
Nmb hawana redusing balance kaka utakachoanza kukatwa ndo hcho mpaka umalixe.
 
CRDB na NMB mikopo kwa watumishi ni asilimia 18 kwa mwaka..ukichukua milion kumi kwa miaka mitano utarejesha sh milion kumi na nne..kwa mwez watakukata wastani wa sh laki mbili na nusu.
 
Mm niliomba m20 kwa basic ya 1091000 wakanipa m13 kwa marejesho ya 316000 hivyo sijakamilisha lengo hao ni nmb
 
Mkuu 17% gawanya kwa 12 annually=1.4 ambayo ni monthly. Sasa ukiaza ku calculate mfano umechukua 12m kwa mda 5yrs 12,000,000 x 12/100 =168000 riba ya kwa mwezi. Sasa chukua 12000000/5=2400,000/12=200,000. So riba kwa mwez inakua 200,000 +168000=368,000. Sasa chukua hii hela mara miez 60 kwa maana ya miaka 5. Twende, 368,000 x 60 =22,080,000/=. Jamani si ndo hivi au mm nakosea.
Nijuavyo asilimia 17 amabyo ni riba, ukikopa Tsh 1 utalipa Tsh1+0.17, yaani 1.17. So kwa million 12 basi utakazopaswa kulipa ni 12,000,000*1.17.
So monthly REPAYMENT KWA MIAKA MITANO NI

12,000,000*1.17/60
 
duuuh mikopo hela nyingi sana unarudisha kwa hali hii siwezi kopa..!!!!
 
Nmb hawana redusing balance kaka utakachoanza kukatwa ndo hcho mpaka umalixe.
swaga zetu tunapoongelea reducing balance hatuongelei rejesho la mwezi tunaongelea riba yaan kwa mfano wa reducing balance ni kwamba rejesho la kwanza ulilipa riba elfu moja,la pili utalipa riba mia tisa mpaka mwisho utakuta may b umelipa sh moja,kwa upande wa straight line ni kwamba ukianza na riba ya elfu moja utalipa rejesho la kwanza mpaka la mwisho hyo hyo elfu moja

sasa kwanini unaona rejsho halibadiliki ni kwasababu riba ikipungua principal(hela yao waliokukopesha) inaongezeka kwa hyo unakuta zinaji offset kwa mfano
principal interest inst
rejesho la kwanza 120 10 130
rejesho la pili 121 9 130
rejesho la tatu 122 8 130
hyo ni reducing balance

princ inte inst
straight line 120 10 130
120 10 130
120 10 130

utagundua mtu wa reducing balance kwa miez mitatu kalipa riba ya 27 na wastraigt riba 30. hope umeelewa so kwa repayment za hao nmb na crdb wanatumia reducing
 
Hapo kwenye kidhungu umeniacha mkuu,.
mfano nimekopa 6,000,000/= Kwa miaka5 natakiwa kulipa 10,000,000/=.Je nikiamua kuachana na huo mkopo wa 6,000,000/=kwa mwaka mmoja nitalipia riba ya mwaka pekeyake?.au kutakuwa na ghara zingine?
kwa kawaida umekaa na hela mwaka mmoja umerudisha lazima ulipe riba ya mwaka mmoja japo hapo inategemeana na taasisi au bwnki husika wana policy gan katika kulipa madeni.Hapo narudia kusema kuna wengine utalipa mpaka penalty miez mitatu ktu ambacho sio sahihi na hapo inatokana na ufahamu wa mteja.NITOE RAI KWA WADAU WA HII MADA WAKOPAJI WENGI HAWASOMI MIKATABA YA MIKOPO WAMAPOCHUKUA NA HII INASABABISHA BAADHI YA WAKOPAJI KUWEKA VIFUNGU VYA AJABU AMBAVYO NI MZIGO KWA MKOPAJI KAMARIBA KUBWA TOFAUT NA ALICHOKWAMBIA KWA MDOMO NA UKISAINI MAANA YAKE UTALIPA TU.KUKUBALI HZO ADHABU UKILIPA MKOPO KABLA YA MUDA
 
mkakope saccoss bank mateso tu... siku hizi kila ofisi ina saccoss
 
Kama ni mfanyakazi wa serikali kuna hazina saccoss cheki na watu wa hazina wana saccoss yao riba asilimia 2
 
Au kopa kidogokidogo bank zinaumiza mno unakopa mpaka unatoka damu
 
UAE riba Ni 3% . Na ukiamua kurejesha mkopo wote within 6month. Hutalipa chochote zaidi.
 
Bayport financial service ndio suluhisho la riba karibuni Bayport acheni woga!!!
 
Back
Top Bottom