Uchaguzi 2020 Richard Kasesela ajitosa kuutaka Ubunge wa Jimbo la Kawe

Uchaguzi 2020 Richard Kasesela ajitosa kuutaka Ubunge wa Jimbo la Kawe

Ngoja tuone kama Makamanda mtakubali kirahisi kumuachia Kasesera hilo Jimbo. Ni wakati pia kama Taifa kuangalia mishahara, posho na kiinua mgongo cha Wabunge wetu.

Haiwezekani wanaccm wapigane vikumbo kwa kiwango hiki. Wako radhi kubwaga manyanga ya Ukuu wa Mkoa na Wilaya! Kisa Ubunge!!
Muache aje watu wanze kufukua makaburi juu ya kale katabia kake
 
Wa Kwanza Tukamtia Cross
Wa Pili Tukamtia Cross
Wa Tatu Tukamtia Cross
Wa Nne Tukampa
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania


*Viongozi Ninaowateua Waridhike Na Nafasi Zao
 
Huo mbuyu siku hizi umekuwa mchicha. Hata mtoto wa miaka miwili anung'oa bila shida..
 
Pamoja na Kauli ya Mwenyekiti wa ccm ya kuwataka viongozi wa kuteuliwa kuridhika na vyeo vyao , lakini taarifa za leo kutoka EA TV zinadokeza kwamba Mkuu wa Wilaya ya Iringa Ndugu Richard Kasesera ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kawe la Jijini Dar es Salaam.

Kwa kipindi cha miaka 10 jimbo hilo limeongozwa na Mbunge wa Chadema Mh Halima Mdee ambaye amepachikwa jina jipya la " MBUYU "

Swali ni Je Kasesera ataweza kuung'oa Mbuyu au anatafuta njia ya kuukimbia U-DC ili kukwepa kutumwatumwa ?
Ushauri kwa Kasesela, maadam yeye ni Mhe. DC, ajitulize tuu huko Iringa, wana Kawe wapo wa kutosha.

Japo ni kweli Halima Mdee ni ubuyu, ila hata ubuyu, ulianza kama mchicha!.
P
 
Mdee lazima afungashwe virago awe na CCM au chama chochote
 
Back
Top Bottom