Richard Temu, mlanguzi wa kakao Kyela anayepambana kuua Ushirika ili apate bei ya chini toka kwa wakulima moja kwa moja

Richard Temu, mlanguzi wa kakao Kyela anayepambana kuua Ushirika ili apate bei ya chini toka kwa wakulima moja kwa moja

Katika mfumo wa stakabadhi ghalani mkulima analipwa ndani ya masaa 48 baada ya mnada kufanyika. Na hizo pesa zinalipwa moja kwa moja. Hivyo uboreshaji uliopo wa sasa hakuna kuchelewesha malipo
Mnada unafanyika mara ngapi kwa mwezi ili tuone hizo saa 48 zako
 
Wewe umekosa mtaji wa kulangua,

Mimi sioni kosa La Richard Temu!! Biashara siku hizi ni huria!! Kuna chama na kuna wanunuzi binafsi!!

Mkulima yupo huru kuuza popote anapotaka!! Akitaka kuuza kwenye chama cha Ushirika au wafanyabiashara AKA walanguzi kama ulivyowaita ni wao wenyewe!!

Inavyooneekana kwenye hicho chama cha ushirika kuna uwalakini kwenye mauzo ya wakulima ndo maana wanakimbilia kwa hao walanguzi. Hicho chama wajikague kwanza wana mapungufu gani mpaka wakulima wanaenda kwa walanguzi!!

Siamnini kwamba chama kina terms nzuri then mkulima aache kuuza mazao yake hapo na badala yake aende kwa mfanyabiasha binafsi!!

All in all sioni kosa la huyo Richard Temu, labda kama halipi kodi kwa serikali then serikali imfuatilie!!
Minada yao ni longolongo sana , atuambie ni minada ngapi zinafanyika kwa mwezi , watu wanataka kunywa UBWALWA halafu wewe umlipe baada ya miezi , walanguzi wataendelea kutamba tu
 
Ushirika nao ni wizi tu. Ushirika wa kweli ni ule ambao wananchi wanaunda wenyewe kwa hiyari. Kungekuwa na ushirika mwingi tu, si mmoja wilaya nzima.
Tafuta taarifa ndio uongee haya. Ushirika wa mahala husika unaundwa na Wakulima wa zao husika. Na bodi ya huo Ushirika inaundwa na wakulima waliochaguliwa na wakulima wenyewe. Na bodi hiyo ndio ina mamlaka na maamuzi ya mambo yote katika ushirika. Na siku ya mnada wakulima ndio wanaamua bei ya kuuza zao kutokana na kampuni iliyoweka bei kubwa. Wasiporidhika mnada unaahirishwa kwa siku mbili.
 
Minada yao ni longolongo sana , atuambie ni minada ngapi zinafanyika kwa mwezi , watu wanataka kunywa UBWALWA halafu wewe umlipe baada ya miezi , walanguzi wataendelea kutamba tu
Mnada unafanyika mara moja kwa kila wiki ambayo ni siku ya jumatatu. Kama wakulima hawataafiki bei basi mnada unarudiwa siku ya jumatano inayofuata.
 
Tafuta taarifa ndio uongee haya. Ushirika wa mahala husika unaundwa na Wakulima wa zao husika. Na bodi ya huo Ushirika inaundwa na wakulima waliochaguliwa na wakulima wenyewe. Na bodi hiyo ndio ina mamlaka na maamuzi ya mambo yote katika ushirika. Na siku ya mnada wakulima ndio wanaamua bei ya kuuza zao kutokana na kampuni iliyoweka bei kubwa. Wasiporidhika mnada unaahirishwa kwa siku mbili.
Mtu anahiyari ya kutokuwa ndani ya huo ushirika? Kunawezekana hapo kyela kukawa na vyama 5 au 10 vya wakulima wa kakao?
 
Zao hili ni mti. Ukipanda unaanza kuvuna baada ya miaka mitatu. Na utavuna kwa hadi miaka 50. Na zao hili halina msimu, kwa maana kuwa unavuna kila wiki. Tofauti tu kuna muda uzalishaji uko juu na wakati mwingine uko chini. Lakini ukilima una uhakika wa kupata pesa kila wiki kama wachezaji wa mpira wa Ulaya. Kiufupi ni kilimo kizuri. Hata Mvomero tayari hivi sasa wanavuna na kuuza kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Anasumbua sababu anajitapa mbele za watu kuwa anammudu Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Ushirika KYECU wasio waamimifu.
Atakuwa na madaraka ndani ya CCM
 
Mtu anahiyari ya kutokuwa ndani ya huo ushirika? Kunawezekana hapo kyela kukawa na vyama 5 au 10 vya wakulima wa kakao?
Mfumo wa ushirika unasaidia sana hata ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Lakini zaidi unalenga kuboresha maisha ya wakulima na kuhakikisha wanapata bei bora ya mazao. Serikali huweka bei elekezi kulingana na bei ya soko la dunia.
Sasa mara nyingi wakulima wa vijijini hawajui bei ya soko la dunia. Hivyo ni rahisi kuwanyonya na wakati mwingine wanajidai wamegoma kununua hadi mnawapa kwa bei wanayotaka. Na wengi wanaofanya haya ni watanzania wasio na uzalendo wanaotumiwa na wahindi.

Sasa Serikali ikiweka utaratibu maana yake ni kuwa katika wilaya husika basi mzigo wote lazima upitie katika huo mfumo.

Lakini pia kupitia vyama vya msingi AMCOS kama wakipata mteja moja kwa moja mwenye bei nzuri basi wanaruhusiwa pia kuuza moja kwa moja bila kupitia stakabadhi ghalani. Bado lengo ni kuuza katika umoja ili kuwa na nguvu ya bargaining.

Mfano kila mtu akiruhusiwa kuuza atakavyo ni rahisi kuwachezea na kuwagawa na hatimaye kuwanyonya.
 
Nyuma yake kuna mtu anaitwa MO na bila Shaka unajua nyuma ya MO kuna akina nani, kila la heri katika mapambano yenu!!!
 
Mtu anahiyari ya kutokuwa ndani ya huo ushirika? Kunawezekana hapo kyela kukawa na vyama 5 au 10 vya wakulima wa kakao?
Kuna vyama vya msingi. Ambavyo vinaweza kuundwa na wakulima kuanzia watano na kuendelea. Kisha kinakuwepo Chama cha Ushirika Cha wilaya. Mfano Kyela kuna vyama vya msingi takribani 39.
 
Nyuma yake kuna mtu anaitwa MO na bila Shaka unajua nyuma ya MO kuna akina nani, kila la heri katika mapambano yenu!!!
Sina hakika na MO lakini kuna wahindi anaowanunulia. Sasa sababu ya maslahi yao kibiashara sioni vyema kutaja kampuni yao hapa. Naamini watajirekebisha maana tunaheshimu wadau wote. Muhimu wafuate sheria za nchi.
 
Mpaka sasa hivi hakuna comment ya kuwashambulia Wachagga? JF imekuaje?
Hapa labda washambuliwe wahindi wanaomtumia Richard.

Wahindi ndio wamekuwa wanufaika wakubwa wa kilimo cha Tanzania huku wakulima wakinyonywa kwa kupewa bei ya chini sana.
 
Richard Temu, ni mfanyabiashara mlanguzi wa kakao katika Wilaya ya Kyela, ambaye hulangua kwa bei ya chini toka kwa Wakulima na kuziuza kwa mfumo uliowekwa na Serikali wa Stakabadhi ghalani. Akishazipeleka pia hutumiwa na kampuni za wahindi kupeleka bid yao katika mnada ili waweze kununua na kuzipeleka nje ya nchi.

Yeye na wahindi wanaomtumia wanaona Chama Cha Ushirika cha KYECU na mfumo uliowekwa na Bodi ya Maghala ya Serikali (WRRB) ni kikwazo kwa sababu bei elekezi ya Serikali ya kakao kwa kilo moja ni Tshs. 4200.

Na kabla ya mfumo huo kuwepo walikuwa wakiwalangua wakulima kwa bei chini ya 1000 kwa kilo. Na iwapo mfumo huu watafanikiwa kuua na wakulima wakakosa soko la uhakika wao watawapangia bei ya kununua zao hilo sababu Mkulima hatakuwa na namna nyingine.

Na hiyo bei elekezi ya 4200 ni minimum kuanzia mnada, na kuna wakati kakao inanunuliwa hadi kwa zaidi ya 5000 kwa kilo moja. Hivyo kuwafanya walanguzi hawa kukosa kupiga margins kubwa zaidi huku wakiwanyonga na kuwanyonga Wakulima.

Richard Temu na wafanyabiashara wanaomtumia wanapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu ili kuzuia hujuma wanazofanya ili kuua Ushirika jambo litalopelekea Serikali kukosa kodi ya uhakika na wakulima kukosa bei nzuri na soko la uhakika.

Kwenu Taasisi za Umma.
Suluhisho muhimu katika mambo kama haya yanayohusu juhudi za wananchi ni pamoja na kuwapa elimu wakulima ili waweze kutambua hujuma zinapotumika kuwanyima haki zao.

Serikali ina wajibu wa kulisimamia hili. Mkulima mweye kujua mwenendo mzima wa soko la mazao yake hawezi kamwe kuhadaiwa na hao walanguzi.
 
Back
Top Bottom