Tetesi: Ridhiwan Kikwete, Freeman Mbowe, Halima Mdee, miongoni mwa wadaiwa Twiga Bancorp

Tetesi: Ridhiwan Kikwete, Freeman Mbowe, Halima Mdee, miongoni mwa wadaiwa Twiga Bancorp

Hoja nyingine za hovyo kabisa !umewahi kuona wapi kudaiwa na benki ni dhambi?!! Au mwanasiasa haruhisiwi kuwa na biahara/investments?!

Hao akina Mbowe ,Mdee na Ridhiwani wangekuwa wame-default masharti ya mkopo mara baada ya benki hiyo kuchukuliwa na benki kuu Mali zilizowekwa dhamana kwa mikopo ya watu hao zingeshapigwa mnada.Sasa iweje wewe uje hapa ukishadadie eti wanadaiwa Mara eti ndio wameifilisi twiga..huu ni upuuzi ulipitiliza
 
he hivi wewe umesoma mleta mada alivyoandika au unakurupouka//// umesomalakini waliochukua mikopo.umesoam lakini ni kiasi gani. unajualakini ni lini wamechukua. yaani hii nchi sasa unamlaani aliyeibua. hivi kweli akiliikosawakweli. au wewe ndio mkopaji nini. kama ndio basi mtaweweseka sana .mh magufuli hana mcheo wala urafiki na mtu lipeni nchi isonge mbele.
Sikua namjibu mleta mada kwenye andiko langu, nilikua namjibu niliemnukuu hapo juu ambae aliuliza swali. Hato meengine unaleta wewe. Usipende kudakia mambo. Soma post ya niliyomnukuu niliemjibu.
 
Kumbe ndio maana niliona akimsifia Lowassa maji yamefika shingoni?.....

Kweli kama Magufuli atawashugulia hawa ndio mafisadi sasa Wa nchi hii sio wakuchekea hata kidogo.

Magufuli washugulikie kweli kweli hawa ndio tatizo la nchi hii.....
Wadai hawajawahi kuwa wahujumu uchumi!
hapa kifupi raisi anafeli, yaani kama sera zake zinaweza kuwafanya wafanyabiashara kama Mbowe ashindwe kulipa deni, sasa wale watu wa vicoba we una dhani wana hali gani?
mtu akikopa bank anapaswa kusifiwa na sio kubezwa, tambua kuwa riba ni pato la bank!
 
Mi sidhani kama tatizo ni wadaiwa bali ni menejimenti tu mbovu ya benki hiyo...hivi kwani kila benki si ina ukomo wa fedha ambayo wanaweza kukopesha wateja wao??? Sasa kwanini wao waliendelea tu kukopesha hata walipofikia huo ukomo???

Ni ujinga tu na haisaidii basi kuanza kutaka kudhalilisha wakopaji baada ya kujiendesha kimagufuligufuli kwa miaka yote hiyo!
 
Walikuwa wanagawana nchi kama vigogo wakawaida walikula ratio 7:0 kwa 2:3 je, vigogo wakubwa watagawanaje may be 100:45 billions
 
Sasa mbona jamaa kasahau kuwa kupata kwake kulitokana na msaada wa kambi ya EL. Shukrani ya punda ni mateke?
 
Jamani naona wengine wanachanganya mambo. Huwezi kumwita mtu fisadi kwa kuwa ekopa kutoka benki. Kazi za benki ni kukopwa. Hata kama wameshindwa kulipa bado ni kawaida.
 
shigongo alipewa maji ya kunywa na mama meghji apunguze uchungu,hivi jamani uchungu wa hela unapozwa kwa maji ya kilimanjaro?

Ndio Maji yanasaidia asipatwe na mshituko wa moyo au kiharusi mama Meghji ni mzoefu nadhani
 
Kudaiwa ni kitu cha kawaida jaman.

Sijaona jambo la ajabu hapa wala sijaona cha kushangaa.
 
Kumbe ndio maana niliona akimsifia Lowassa maji yamefika shingoni?.....

Kweli kama Magufuli atawashugulia hawa ndio mafisadi sasa Wa nchi hii sio wakuchekea hata kidogo.

Magufuli washugulikie kweli kweli hawa ndio tatizo la nchi hii.....
WEWE HUELEWEKI,MARA JPM SAFI,MARA JPM HAFAI WE VIPI BANA?
 
Mimi nina wasiwasi hata ile pesa ya kampeni kumnadi mtukufu akiwa na wakata viuno stejini ilikopwa huku!
 
Wekeni ushahidi wa Mbowe na Halima kudaiwa sio kuja na porojo hapa , na kama kweli wanadaiwa ni miongoni mwa waliokiuka masharti ? Acheni kuchafua watu kwa sababu za kisiasa , mmeona jina la Ridhiwani likienda peke yake halina mvuto sio ?

Wekeni ushahidi sio kuandika kwa taarifa nilizonazo kwani hata mimi nina taarifa kuwa Songoro Mnyonge naye ni mdaiwa sugu //......
 
Si mlimwita Ridhiwani tajiri na kila jengo zuri nchi hii ni lake.. Si mlisema Ridhiwani ni Trillionea??

Si mlisema JK na Family walikuwa wanajichotea tu pesa kule Hazina?? Sasa kama walikuwa wanachota pesa tu ilikuwaje Ridhiwani akope benki ya biashara na ashindwe kulipa? Hapa ndipo tunaona wanasiasa walivyo wanafki na waongo..
Aisee nimeipenda hii. Kweli binadamu sisi ni wachochezi.
 
HII NI DHARAU KUBWA KWA WATZ......HV KWELI MTU KAMA RIDHIWANI, NI WA KUSHINDWA KULIPA DENI?????? VP KAMA ANGESHINDA BERNARD MEMBE, HAYA MAMBO TUNGEYAJUA???? AMA KWELI "BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA"
Hapi ndipo unatakiwa ujue kuwa Ridhwani ni mtu wa kawaida kabisa na hivyo umma ulivyokuwa ukiaminishwa hapo kabla.
 
Zamani nilikuwa shabiki Mkubwa wa habari za mabaya ya wenzangu lkn kwa kadri siku zinavyokwenda najilaumu kushabikia matatizo ya wenzangu..nimekoma kabisa maana hatuelewi tunapopelekwa.
U'r matured.
 
Back
Top Bottom