Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Joined
May 7, 2013
Posts
49
Reaction score
10
Mbunge wa Chalinze kupitia chama cha mapinduzi Ridhiwani Kikwete ametoa kauli zinazooneshwa wazi kutothamini wala kujali michango inayofanywa na vyombo vya habari nchini.

Alipokuwa akiwahutubia wanafunzi wana CCM wanaohitimu vyuo vikuu na vya kati katika bwalo la Umwema morogoro, alianza kwa kusema ''nipisheni hapo sikuja kuzungumza na nyie nimekuja kuongea na wana vyuo''

Pia katikati ya hotuba yake akasema namnukuu''wakati tunalipokuwa tunaelekea kujadili bajeti ya wizara ya nishati na madini wizara ambayo imefanya mambo mazuri kwa nchi hii cha ajabu magazeti yakaandika waziri Muhongo kikaangoni, kwa lipi?

Ndiyo aina ya magazeti tuliyonayo CCM hoyee'' Kisha akaendelea kuwashambulia waandishi wa habari''magazeti haya yanaandika andika tu hadi mimi mwenyewe nashindwa kuelewa, juzi tulipokuwa tunajadili wizara ya habari makelele yakaanza tunataka mjandala, tunataka waandishi walio huru mimi nikawa najisemea moyoni tukileta huo mswaada kesho waandishi wa habari hawatalia kwa sababu asilimia kubwa ya waandishi tulionao ni makanjanja wanapokaa katika meza zao wanaandika andika tu vitu yaani mtu anapikapika tu vitu''

NINA HARAKA KIDOGO NAMUWAHI KUMSIKILIZA MWIGURU ANAMKUTANO MUDAA HUU.

VIDEO KESHO TUVUMILIANE MAJUKUMU NI MENGI ILA TUHESHIMU KAZI ZA WENGINE HATA KAMA SISI MAISHAYETU NI MAZURI HADI KUFA .

UKISHIBA USIMZALAU MWENYE NJAA MAANA HAKUNA AJUAE KESHO ITAKUWAJE.

ASANTE KWA MUDA WAKO
 
Mi mwenyewe!! Lol! Haya na iwe kweli kasema hayo vinginevyo umbea hauna posho
 
Tatizo mlimpigia debe sana,sasa lazima awaonyeshe yeye ni mtoto wa Mkullu,na yupo pale si kwa ajili ya kutetea wanachalinze bali hadhi yake na familia yake.Poleni kama mmekwazika na hilo hamkulijua.Anatengeneza jina.Kwenye chama chetu bila kutukana hauwezi kupata uwaziri,mwache autafute kwa kasi kabla baba hajatoka.

Aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Mbunge wa chalinze kupitia chama cha mapinduzi Ridhiwani Kikwete ametoa kauli zinazoonyeshwa wazi kutothamini wala kujali michango inayofanywa na vyombo vya habari nchini, alipokuwa akiwahutubia wanafunzi wana CCM wanaohitimu vyuo vikuu na vya kati katika bwalo la umwema morogoro alianza kwa kusema ''nipisheni hapo sikuja kuzungumza na nyie nimekuja kuongea na wana vyuo'' alafu katikati ya hotuba yake akasema namnukuu''wakati tunalipokuwa tunaelekea kujadili bajeti ya wizara ya nishati na madini wizara ambayo imefanya mambo mazuri kwa nchi hii cha ajabu magazeti yakaandika waziri Mhongo kikaangoni kwa lipi ndiyo aina ya magazeti tuliyonayo CCM hoyee'' kisha akaendelea kuwashambulia waandishi wa habari''magazeti haya yanaandika andika tu hadi mimi mwenyewe nashindwa kuelewa juzi tulipokuwa tunajadili wizara ya habari makelele yakaanza tunataka mjandala, tunataka waandishi walio huru mimi nikawa najisemea moyoni tukileta huo mswaada keho waandishi wa habari hawatalia kwa sababu asilimia kubwa ya waandishi tulionao ni makanjanja wanapokaa katika meza zao wanaandika andika tu vitu yaani mtu anapikapika tu vitu''

NINA HARAKA KIDOGO NAMUWAHI KUMSIKILIZA MWIGURU ANAMKUTANO MUDAA HUU ...VIDEO KESHO TUVUMILIANE MAJUKUMU NI MENGI ILA TUHESHIMU KAZI ZA WENGINE HATA KAMA SISI MAISHAYETU NI MAZURI HADI KUFA .UKISHIBA USIMZALAU MWENYE NJAA MAANA HAKUNA AJUAE KESHO ITAKUWAJE....AXANTE KWA MUDA WAKO

Lowasa alushasema waabdishi wa Tanzania hawana weledi!me nakubaliana na wote wenye mtazamo huo.waandishi wetu ni vichwa Maji.
 
Waandishibwa habari kwa mahaba niue! Kama ni mwandishi nzuri lazma uwe na maadui kwa kuandika unbiased stories.
 
Waandishi wapo makundi makundi ni tatizo
 
Wengi wao ni mamluki kazi yao kubwa kufukuzia bahasha!!!
 
Ridhiwan-Kikwete-June18-2014.jpg

Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.

"Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu," alisema.

Alisema siyo dhamira yake kuwasema vibaya wanahabari, lakini waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na weledi wa siasa zao jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika hawezi kulisifia badala yake kazi yake kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.

"Mimi ningependa sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi, hatusemi kuwa watu wanapofanya mabovu wanyamaziwe, hapana, wabovu waandikwe na mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe ili kuendelea kutiana moyo katika kulijenga taifa," alisema.

Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.

Alisema wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2014/15, mambo yaliyofanywa na wizara hiyo katika kipindi cha 2013/2014 ni mazuri sana, lakini cha ajabu siku moja kabla ya kuanza kwa mjadala wa wizara hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.

"Kikaango hicho kipi, haya ndiyo magazeti tuliyonayo, yanaandika andika tu yaani mpaka wakati mwingine nashindwa kuelewa," alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulizuka kelele kwa baadhi ya watu kwamba wanataka waandishi wawe huru, lakini yeye (Ridiwani) akawa anajiuliza moyoni hivi huo muswada wa habari ukipelekwa Bungeni hawatalia?

Wakati Ridhiwani akiwashambulia waandishi wa habari, amekuwa mwanasiasa kijana ambaye kila anakokwenda kwenye shughuli za kisiasa anafuatana na msururu wa waandishi ambao humpamba kwa habari nzuri.

Miongoni mwao, ni kikosi kikubwa cha waandishi alichokuwa nacho wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu.

Katika harakati zake za kisiasa amekuwa akitumia waandishi wa habari kumpamba kwa nia ya kujijenga kisiasa kama ambavyo wamekuwa wakifanya wanasiasa wengi, wakiwamo ambao anawachukulia kama mfano wa kuigwa.

Source: Nipashe

 
Riz yupo sahihi kabisa waandishi ni makanjanja asilimia kubwa

Huenda anapoona hawanunuliki tena anawageuka, alipowahitaji aliwanyenyekea, na sasa baada ya kupata kile alichokichuchumia hana haja nao na hata zile bahasha za kaki hawapi tena.
 
Waandishi wa tanzania makanjanja wengi na wala sio siri wanafanyakazi kwa maslahi ya watu tu tena tumewachoka sana wanatakiwa wajue hilo . Wanafanyakazi kwa kununuliwa , angalia NIPASHE , Mwananchi hayafai kabisa .Ukitaka uandikwe habari zako lazima uwape Fedha ni rushwa rushwa tu
 
Safi sana, acha awapake hao jamaa manake wengi wao wanajipendekeza sana hasa kwa wakubwa!!!!!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom