Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Ridhiwani Kikwete: Asilimia kubwa ya waandishi wa Habari ni makanjanja

Waandishi kweli ni makanjanja.......Ridhwani yuko sahihi.....waandishi wangapi walioandika habari hii kama si ukanjanja? Wangapi waliomuonya huyu dogo kwa kauli zake za kuwananga kwa ujumla namna hii?

Ridhwani yuko sahihi kabisa......waandishi wa habari wengi ni MAKANJANJA kazi kujipendekeza tu.....:der:
 
Kasema kweli wanahabari wengi wa tanzania ni wachumia tumbo tu.
 
Kuna habari unaisoma kwenye gazeti halafu unajiuliza hivi huyu ni mwandishi aliyefanya utafiti wa kina kwa ajili ya alichoandika? Riz yuko sahihi kwa waandishi makanjanja, sio wote ila ni wengi
 
Kaongea ukweli mtupu !!!
Ujumbe umewafikia TBC, Habari Leo, Uhuru, Kiu, Risasi na Tazama
 
Ridhiwan-Kikwete-June18-2014.jpg

Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete

Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.

"Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu," alisema.

Alisema siyo dhamira yake kuwasema vibaya wanahabari, lakini waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na weledi wa siasa zao jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika hawezi kulisifia badala yake kazi yake kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.

"Mimi ningependa sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi, hatusemi kuwa watu wanapofanya mabovu wanyamaziwe, hapana, wabovu waandikwe na mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe ili kuendelea kutiana moyo katika kulijenga taifa," alisema.

Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.

Alisema wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2014/15, mambo yaliyofanywa na wizara hiyo katika kipindi cha 2013/2014 ni mazuri sana, lakini cha ajabu siku moja kabla ya kuanza kwa mjadala wa wizara hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.

"Kikaango hicho kipi, haya ndiyo magazeti tuliyonayo, yanaandika andika tu yaani mpaka wakati mwingine nashindwa kuelewa," alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulizuka kelele kwa baadhi ya watu kwamba wanataka waandishi wawe huru, lakini yeye (Ridiwani) akawa anajiuliza moyoni hivi huo muswada wa habari ukipelekwa Bungeni hawatalia?

Wakati Ridhiwani akiwashambulia waandishi wa habari, amekuwa mwanasiasa kijana ambaye kila anakokwenda kwenye shughuli za kisiasa anafuatana na msururu wa waandishi ambao humpamba kwa habari nzuri.

Miongoni mwao, ni kikosi kikubwa cha waandishi alichokuwa nacho wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu.

Katika harakati zake za kisiasa amekuwa akitumia waandishi wa habari kumpamba kwa nia ya kujijenga kisiasa kama ambavyo wamekuwa wakifanya wanasiasa wengi, wakiwamo ambao anawachukulia kama mfano wa kuigwa.

Source: Nipashe


Haya maneno ya huyu mtoto yanamuumbua Pasco na kupenda bahasha za khaki na kuzigawa .Pasco yuko humu humu muumini mzuri wa bahasha ili kuandika ukanjanja .Haya kazi kwenu akina Pasco .
 
Atuambie kwanza kama ameacha kusafirisha madawa ya kulevya. Vinginevyo naye ni kanjanja nguli.
 
Atwambie na watendaji kule Ikulu, ni asilimia gani ni makajanja!?
 
kwani wanaacha ga izo mishe? hiyo ni mwanzo mwsho!!

Sasa aache kuropoka mataputapu ya ukoo wao wakati yeye ni drug dealer aliyetuingiza mkenge kwa Wachina baada ya sakata lake kubumbuluka.
 
Amani anayo yeye kwa kuibuka na utajiri ghafla pasipo utaratibu,huku akizicontrol na kuyumbisha uchumi wa nchi atakavyo.
 
Back
Top Bottom