Mhunzi De Volunteer
Member
- Apr 28, 2014
- 23
- 4
Sure waandshi wengne myeyusho na wazinguaj wapo kwaaili ya manufaa ya watu fulanfulan
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yupo Wapi JACTON MANYERERE Aje Hapa Huu Uzi Unamuhusu.
Waandishi ni kama Waalim katika nchi hii wanatukanwa, wanadhalilishwa lakini hatimaye wakiitwa kula ubwabwa na kupewa shilingi kidogo unaona wanapayuka kupamba watu hata wasio na sifa. Acha Riz awatukane maana jioni atawapoza na ubeche halafu kesho wanaanza kumpamba
nasikia rizwani anataka kuinunua chadema
Naunga mkono hoja
Haya maneno ya huyu mtoto yanamuumbua Pasco na kupenda bahasha za khaki na kuzigawa .Pasco yuko humu humu muumini mzuri wa bahasha ili kuandika ukanjanja .Haya kazi kwenu akina Pasco .
Huenda anapoona hawanunuliki tena anawageuka, alipowahitaji aliwanyenyekea, na sasa baada ya kupata kile alichokichuchumia hana haja nao na hata zile bahasha za kaki hawapi tena.
Kweli yupo sahihi kuita makanjanja maana yeye mwenyewe ni miongoni mwa watu wanaowatumia wanasiasa kwa masilahi yao yaani kama upo kwenye msafara wake lazima uandike ya kumpamba kwa kuwa amekulipa na ndio maana vyombo vya habari hasa magazeti yanatakiwa wajitegemee kila kitu pindi wanapokwenda kuandika habari ili ku-balance, mfano mzuri waandishi wa magazeti ya mwananchi walikuwa wanafukuzwa kwenye kampeni za JK those days na kulikuwa na mratibu ambae anafanya uhakikiRiz yupo sahihi kabisa waandishi ni makanjanja asilimia kubwa
![]()
Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.
Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.
Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu, alisema.
Alisema siyo dhamira yake kuwasema vibaya wanahabari, lakini waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na weledi wa siasa zao jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa.
Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika hawezi kulisifia badala yake kazi yake kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.
Mimi ningependa sana kuwasihi waandishi wetu hebu kidogo tuandike vitu vinavyofanana na hali halisi, hatusemi kuwa watu wanapofanya mabovu wanyamaziwe, hapana, wabovu waandikwe na mabovu yao, wanapofanya mazuri wasifiwe ili kuendelea kutiana moyo katika kulijenga taifa, alisema.
Ridhiwani alisema Watanzania jambo kubwa wanalolihitaji ni amani na kwamba wasomi watambue kuwa nchi ipo mahali pazuri sana na amani inazidi kutawala tofauti na inavyoripotiwa na magazeti.
Alisema wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2014/15, mambo yaliyofanywa na wizara hiyo katika kipindi cha 2013/2014 ni mazuri sana, lakini cha ajabu siku moja kabla ya kuanza kwa mjadala wa wizara hiyo, magazeti yaliandika Waziri Muhongo kikaangoni.
Kikaango hicho kipi, haya ndiyo magazeti tuliyonayo, yanaandika andika tu yaani mpaka wakati mwingine nashindwa kuelewa, alisema Ridhiwani.
Aliongeza kuwa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulizuka kelele kwa baadhi ya watu kwamba wanataka waandishi wawe huru, lakini yeye (Ridiwani) akawa anajiuliza moyoni hivi huo muswada wa habari ukipelekwa Bungeni hawatalia?
Wakati Ridhiwani akiwashambulia waandishi wa habari, amekuwa mwanasiasa kijana ambaye kila anakokwenda kwenye shughuli za kisiasa anafuatana na msururu wa waandishi ambao humpamba kwa habari nzuri.
Miongoni mwao, ni kikosi kikubwa cha waandishi alichokuwa nacho wakati wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Chalinze Aprili mwaka huu.
Katika harakati zake za kisiasa amekuwa akitumia waandishi wa habari kumpamba kwa nia ya kujijenga kisiasa kama ambavyo wamekuwa wakifanya wanasiasa wengi, wakiwamo ambao anawachukulia kama mfano wa kuigwa.
Source: Nipashe
Ohooo!![]()
Mbunge wa Chalinze (CCM),Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amewashambulia wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.
Ridhiwani alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro yaliyofanyika katika ukumbi wa bwalo la Umwema mjini humo.
Asilimia kubwa ya waandishi tuliokuwa nao ni makanjanja, ni ukweli kabisa wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapokaa kwenye ofisi zao wanaandika vitu tu, yaani mtu anapikapika tu vitu, alisema.
Haya maneno ya huyu mtoto yanamuumbua Pasco na kupenda bahasha za khaki na kuzigawa .Pasco yuko humu humu muumini mzuri wa bahasha ili kuandika ukanjanja .Haya kazi kwenu akina Pasco .
Waandishi wa tanzania makanjanja wengi na wala sio siri wanafanyakazi kwa maslahi ya watu tu tena tumewachoka sana wanatakiwa wajue hilo . Wanafanyakazi kwa kununuliwa , angalia NIPASHE , Mwananchi hayafai kabisa .Ukitaka uandikwe habari zako lazima uwape Fedha ni rushwa rushwa tu
Pasco njoo huku njaa yako imeanikwa.