Ridhiwani Kikwete kachukizwa na kitendo cha Nape kumpa bendera Diamond Platnumz?

Ridhiwani Kikwete kachukizwa na kitendo cha Nape kumpa bendera Diamond Platnumz?

Hakuna lolote apewe bendera au asipewe maisha ya watz ni yaleyale
 
Watanzania tunapenda kuconcentrate na tulipo angukia sio pale tulipojikwaa. Hii ni kasumba ya jamii yoyote yenye elimu duni duniani kote. We dont care abbout the cause rather than effect. Ridhiwani alichokisema msikipotoshe kwa chuki binafsi. Yeye alimaanisha badala ya kutoa bendera kwa timu ya Taifa leo tunatoa bendera kwa Mtumbuizaji wa ufunguzi wa kuanza kwa mashindano. Sio kwamba kachukizwa na Daimond kupewa bendera ila alitamani bendera hiyo wapewe Taifa starz kama washiriki wa Afcon. Nimependa alichomanisha Riz big up.
 
Sijaona tatizo kwenye huo ujumbe.


UJUMBE WA RITZ UPO SAHIHI KABISA,HAPA ANAWASIMANGA TFF KWAMBA WANASHINDWA KUENDELEZA MPIRA NDIO MAANA TIMU ZETU ZINASHINDWA KUPATA NAFASI YA KUWAKILISHA NCHI,MPAKA INAFIKIA WASANII WANAPATA NAFASI NA KUKABIDHIWA BENDERA ,SIJUI KWANINI IMEKUWA VIGUMU WATU KUIELEWA KAULI HII YA RITZ?
 
9f3989c1d544f24d181a8d479bbcb7a4.jpg


Kayasema Hayo Kwenye Account Yake Ya Instagram...

Je Ni chuki?.... Kutomkubali Nape ?.. kutomkubali Diamond au Basi Tu
Ukijua maan ya TFF rudi tujadili..
Japo ile wizara inakusanya na sanaa pia..
 
Ila watanzania ni majuha sana wakiongozwa na viongozi wao hivi mtu anaenda kuimba dakika mbili tu na ananufaika yeye mwenyewe et anapewa bendera awakilishe watanzania, ingekuwa taifa stars si wangewapa na wake zao wakaenda nao kabisa huko gabon?!!
 
katumia kanuni ya ccm ya kumsema mtu hata kama kakosea,basi unamsema kwa kupindisha pindisha maneno na kukwepesha ukweli.sasa hapo tff wamehusikaje?.
 
Naomba nisiukizwe maswali ya wajinga wawili kwenye mambo ya kitaifa
 
Aache Maneno aweke music. Kukariri sio vizuri. If plan A didn't work plan B is the best option
 
Ni aibu kwenda kuburudisha wanamichezo wengine ambao sisi tulipaswa kuwa sehemu yao. Diamond anakwendabkibiashara ila si kwenda kuwakiliaha taifa kwa wimbo wa unanitekenyaga ukinyonga salome. Hakupaswa kupewa bendera Ridhiwani yupo sahihi
Kwni samata kule alipo akifanikia atkua atakua anawakilisha taifa?
 
Duh !! Yan watu kime Wauma Diamond kwenda Kuperfom Kukiko Taifa Starz Kukosa Kushiriki. Mpira Hatuuuwez Na daima itakuwa hvyo hvyoo !!
 
Hiyo bendera haikupaswa kutolewa na tff hayo ni maajabu ya kuku miatamia mauai ya bata kwanza huyo dogo sio mcheza kabumbu wala mwanamuziki ni msaniiii sikunyingine muniulize niwape tofauti ya mwanamuziki na msaniii pumba tu hizo sisikazi yetu ni kusindiza tu
Mkuu umemaliza, alitakiwa apewe bendera na basata na si TFF
 
Sasa hapo Ridhiwani kakosea nn? Mleta mada ni mchochezi.

Kingine tusilazimishe mambo, kama mpira unagoma ni kuukazania IPO cku nasi tutasonga tu.
 
TFF kweli ni aibu sana......badala kumpa Samatta bendera tunajisifia kumpa mkata mauno bendera ya nchi na tunaisifia!! Shame kwenu TFF
 
Back
Top Bottom