Responded Ridhiwani Kikwete: Naelekeza Waajiri tengeni bajeti kuwalipa Fedha za Kujikimu Waajiriwa Wapya

Responded Ridhiwani Kikwete: Naelekeza Waajiri tengeni bajeti kuwalipa Fedha za Kujikimu Waajiriwa Wapya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewaagiza waajiri kuhakikisha wanatenga bajeti ya kulipa stahiki za waajiriwa wapya kabla ya kuwasilisha maombi ya kuongezewa watumishi.

Akizungumza Septemba 23, 2026, jijini Dodoma katika Mkutano wa 14 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA), Kikwete amesema kumekuwa na malalamiko ya waajiriwa wapya wanaopangiwa vituo vya kazi, kuripoti na kuanza majukumu bila kulipwa stahiki zao, ikiwemo fedha za kujikimu.

Amesema Ofisi ya Rais, Utumishi haiwezi kupeleka waajiriwa wapya katika ofisi ambazo hazijajipanga na hazijatenga bajeti ya kutosha kulipa stahiki zao.

Ameeleza kuwa hali hiyo huathiri morali ya kazi na kusisitiza maafisa utumishi pamoja na wakurugenzi kuhakikisha fedha zinatengwa kabla ya kuomba watumishi wapya.

Kikwete ameonya kuwa kuendelea kuomba waajiriwa wapya bila kutenga fedha za kulipa stahiki zao, ikiwemo posho za kujikimu, kunaongeza deni la Serikali, jambo ambalo si lengo la Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma:

-Kuchelewa kwa Fedha za Kujikimu — Waajiriwa Wapya Ifakara TC
-Waziri wa TAMISEMI shughulikia tatizo la ajira mpya katika Halmashauri mbalimbali kutolipwa fedha za kujikimu
-Waajiriwa wapya wa Wilaya ya Ileje, tumelipwa fedha kidogo sana za kujikimu kuliko tunachostahili
- Uchunguzi ufanyike kuhusu stahiki za kujikimu za Walimu wapya, wengi tunaambiwa tuandike fedha pungufu
 
Back
Top Bottom