Ridhiwani Kikwete: Serikali haina bajeti ya kuendeleza taasisi za wenza wa viongozi

Ridhiwani Kikwete: Serikali haina bajeti ya kuendeleza taasisi za wenza wa viongozi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 2 leo Aprili 5, 2023.



RIDHIWANI: SERIKALI HAINA BAJETI YA KUENDELEZA TAASISI ZA WENZA WA VIONGOZI
Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga ameuliza kama Serikali ina mpango wa kuendeleza Taasisi za wenza wa viongozi wakuu Nchini ambazo zinapotea baada ya kutoka madarakani.

Naibu Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amejibu “Hakuna Sheria wala muongozo wa kuwa na Bajeti kwa ajili ya taasisi hizo, kuchukua fedha za umma kupeleka kwenye taasisi za watu binafsi, hilo jambo halijakaa sawa.”
 
Siwezi kupoteza muda kufuatilia maigizo ambayo hayana faida bora niangalie Azam sports kuna marudio ya mechi
 
Bunge kibogoyo! Yaani ni kama mkutano tu wa makada wa ccm.

Halina hata chembe ya mvuto.
 
Na wakitoka kujadili upuuzi hapo, watakuja na azimio la kumpongeza no 1,na kila mmoja wapo ni kicheko all the way to bank, 12M+TSHS,kila mmoja wapo na hapa JF ni mwendo wa kujadili sports na ngono!!
 
"Viongozi wote wa Serikali, dini, mila na vyama vya siasa wakemee kwa nguvu zote ushiriki wa sehemu yoyote ya jamii katika matendo yasiyoendana na mila, tamaduni na desturi za Watanzania.

Hii ni pamoja na wazazi na walezi wote kushiriki kikamilifu katika makuzi na malezi bora ya watoto yatakayosaidia kuwaepusha na vitendo viovu"
Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu JMT
Alipokuwa akihutubia bunge kuhusu

MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2023/2024
 
Back
Top Bottom