Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
TUKISIMAMIA HAKI NA SHERIA,TUTAONDOA UVAMIZI - RIDHIWANI KIKWETE
Maneno hayo ameyasema Mh. Mbunge na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipofanya Ziara ya siku moja katika kata ya Lugoba ambapo migogoro ya Uvamizi wa Ardhi za Vijiji inaonekana kuanza kushamiri. Katika ziara hiyo Ndg. Kikwete ameendele kuwaasa wananchi kuheshimu taratibu na sheria kwani huo ndiyo msingi utakaoleta Amani katika jamii yetu.