Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Ukifuatilia utagundua ni nadra au haiwezekani wadau na mastaa wa michezo hasa wa mpira wa miguu kujitenga na utawala au watawala wowote wale hata wawe madikteta katili kiasi gani.
Sijajua sababu ya jambo hili ni nini ila kwa kiasi kikubwa mpira wa miguu una mafungamano makubwa sana na watawala wa aina yoyote dunia, labda sababu ya pesa na sifa.
Kagame pamoja na matatizo yake yote bado Rwanda ina mikataba mikubwa ya matangazo na klabu kubwa za Ulaya kuitangaza. Dikteta katili Teodoro Nguema wa Guinea ni kipenzi cha CAF na FIFA. Roman Abramovich rafiki mkubwa wa Putin alikuwa mmiliki wa Chelsea. Mesi na Ronaldo walienda kujikomba kwa Trump. Hakuna chombo chochote cha mpira kilichojaribu kujitenga na Israel mpaka sasa hata baada ya genocide ya Gaza.
Saudi Arabia, Qatar na UAE wamefanikiwa sana kutumia mpira kujiosha katika ulimwengu wa magharibi.
Sitashangaa hata Ronaldo au Messi wakija Tanzania kwa uratibu wa Bashite, hiyo ndio nature ya mpira ulivyo.