Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwe nimefurahi sana kuona "Refugee team" kwenye olympic.
Nitakuwa nawafuatilia. Hivi wa TZ wanacheza michezo gani kwenye Olympic?
Na pia nasubiri kwa hamu kuangalia Rugby sevens.
Asante kwa kufungua thread BAK.
Shukrani sana afrodenzi. Nimeshangaa sana hata Burundi pamoja na matatizo yao yote ya machafuko ndani ya nchi na kutokuwa na rasilimali nyingi kama Tanzania wamepeleka wanariadha 10 na population yao ni 10 million, sisi wenye polupation ya 49 million na rasilimali chungu nzima walionyesha tumepekeleka wanariadha 7 tu. Kama sikosei idadi ya wanariadha wetu walioenda Rio tumewazidi Somalia kwa wanariadha wawili au watatu hata Somalia jamani!!!! Duh!!!! Kweli nchi hii michezo haipewi kipaumbele kabisa. Najua wewe mpenda Rugby huu mchezo nimejaribu kuufahamu lakini umenipiga chenga. Ukanifunga kamba kwamba utanipa tuition ya nguvu ili niufahamu lakini hadi hii leo bado sijaujua lol!
Na mi-jacket ya baridi au mvua sijui, si wangevaa basi kama wamasai au wahehe au wapemba au ...au...au....nk. nk.Yaani mi imenibidi nitafute nchi nyingine ya Ku support TZ wameniudhi sana. Halafu walivyo vaa matisheti makubwa
ya njano nchi nyingine nyingi wamevaa nguo zao za Traditional wamependeza kweli. Ila Tanzania aibu tu kwa kweli.
Kuhusu rugby lol kesho nitakufundisha maana leo niko busy hahahahahhaha lol
Ni super rugby final leo Hurricanes (NZ) VS Lions (RSA). na nikisahau hakikisha unanifuata
kule mahali. Maana world cup ikianza nataka uwe umeelewa kila kitu ili nikianzisha thread
kuwe na mtu wa ku comment lol😀😀😀😀😀😀😀
Kuwaona wanaingia uwanjani nimewaona lakini picha nimetafuta sana sijafanikiwa, nikiipata nitaiweka hapa Best.
Tanzania Rio 2016Na mi-jacket ya baridi au mvua sijui, si wangevaa basi kama wamasai au wahehe au wapemba au ...au...au....nk. nk.