Duh! Inasikitisha sana huyu genious kututoka. Nilisoma na mdogo wake. Huyu bwana alikuwa neurosurgeon wa kwanza Tanzania. Enzi zake, alimaliza form 6 na division one ya kipekee akipata Physics A, Chemistry A, Biolology A.
Alipigania Jeshi kuwa na chuo kikuu chake hata akasababisha wanajeshi wengi kusoma kwa kiwango cha juu. Alikuwa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Science na Tekinolojia.
RIP professor. Mungu awajalie moyo wa hekima ya Mungu ili wayapokee mapenzi yake kwa moyo wa unyenyekevu na imani.
Makono rafiki yangu upo wapi, tumepoteana. Kama unaingia humu au mtu yeyote ana mawasiliano naye, tuwasiliane.
Najua Kamanda Siro hatakosekana kwenye msiba huu, maana wote wanatoka Ikizu kule Musoma.
Pole sana kwa kifo cha Kaka yetu.
Mwenye taarifa za taratibu za maziko, tafadhali atuwekee hapa ili tuliopo mbali tuanze kuangalia kama tutaweza kushiriki kumsindikiza huyu ndugu yetu.